Header Ads

NJIA 3 ZA KUSAIDIA KUONDOA HARUFU YA KWAPA NA WEUSI

Inner thighs/mapaja ya ndani na makwapa hutokea weusi kutokana na msuguano wa ngozi kwasababu ya mapaja kugusana, hata ngozi iliyokauka pia inaleta weusi katika ngozi.
Hivyo nimekuletea njia natural ya kuondoa weusi huo bila kutumia madawa makali.

1.TUMIA MAFUTA YA NAZI NA NDIMU.
Mafuta ya nazi yanatumikakulainisha ngozi lakini unaweza kutumia pia katika kuondoa weusi ukichanyanya na ndimu..

Fata step hizi::

Chukua vijiko 3 vya mafuta ya nazi changanya na ndimu nusu
Paka sehemu yenye weusi katika mapaja huku ukisugua kama unafanya massage kwa dakika 15.
Kisha osha na maji ya uvuguvugu na kausha kwa kitambaa kilaini na kisafi.


2.TUMIA MCHANGANYIKO WA SUKARI ASALI NA NDIMU.
Mchanganyiko huu pia unaweza ukaondoa weusi katika mapaja na makwapa, fuata step hizi::

Changanya kijiko kimoja cha asali, ndimu nusu na kijiko kimoja cha sukari.
Paka sehemu yenye weusi na sugua kawaida hadi sukari ipotee.
Acha ikae kama dakika 10 kisha osha na maji ya uvuguvugu.


3.GANDA LA CHUNGWA NA ASALI
Kama mnavyojua machungwa yana vitamin C, na hivyo ukichukua ganda la chungwa pamoja na asali, mchanganyiko wake pia unaondoa weusi.

 Fuata step hizi::

Chukua ganda la chungwa na kijiko kimoja cha asali.
Kamua hilo ganda maji yake yangie kwenye asali.
Kausha nakusaga hilo ganda kisha poda yake ichanganye na asali
Paka mchanganyiko huo katika sehemu yenye weusi, kaa kwa muda wa dakika 15
Osha na maji ya kawaida hadi kugandaganda kupotee.

No comments

Powered by Blogger.