Header Ads

BODI YA TANZANIA YATOA HATMA YA ML.KILIMANJARO.

Bodi ya Utalii Tanzania imetoa taarifa kufafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.

Shirika hilo lilikuwa likiripoti kuhusu kifo cha Guguleth Zulu, raia wa Afrika Kusini, aliyefariki akikwea Mlima Kilimanjaro.
  • Bi Odinga: Nilikosea, Olduvai Gorge iko Tanzania
  • Odinga: Magufuli ataifaa Tanzania
“Tungependa kusahihisha habari za kupotosha zilizochapishwa na Miami Herald, kwamba Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,” taarifa iliyotiwa saini na meneja mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ilisema.

Bodi hiyo inasema imeliandikia barua gazeti hilo na kulitaka lichapishe sahihisho.

No comments

Powered by Blogger.