Header Ads

KIJANA MWINGINE AMTUKANA MAGUFULI KWENYE NOAH MWANZA

Mgomo wa daladala Jijini Mwanza umesababisha kijana mmoja Jijini humo kutamka lugha chafu ndani ya gari ambayo alipewa lifti limemsababishia kuishia mikononi kwa sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast dereva wa wa gari likitoa lifti Hassan Bushagama mkazi wa Buhongwa Jijini Mwanza asema alipofika eneo la Buhongwa akiwa na usafiri wake aina ya Toyota Noah kutokana mgomo wa daladala aliamua kutoa lifti kwa abiria aliowakuta hapo.

"Walipanda watu kama nane ambapo Dada mmoja akasema watu walivyo hawatakawia kusema Rais Magufuli ndiye anatakiwa aulizwe,kijana mmoja wa umri wa miaka kama 27 au 28 hivi akadakia akasema Rais ni '******** 'mzee mmoja akamwambia kijana tengua kauli lakini akakataa na kusisitiza ,abiria wakataka kumpiga nikawaambia mwacheni tumpeleke 'polisi " Amesema Bwana Bushagama.

Bushagama ameendelea kusema kwamba "Baada ya hapo niliendesha gari langu hadi kituo cha polisi tulipofika pale nikawaambia polisi hali halisi askari akawahoji abiria wakaelezea hali hiyo na yeye alipoulizwa akasema ,amesema hivyo lakini hakujua kama ingepelekea kufika huko.

Aidha Bushagama ameongeza kuwa wameamua kusitisha kazi zao na kuonesha uzalendo ili kuonesha kwamba Rais hawezi kutukanwa namna hiyo.

Kwa upande wake Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwama kijana huyo amejitetea na kusema kwamba alisema alimaanisha wanaogoma wanajifanya wapumbavu lakini Rais ni ******** zaidi yao jambo liliwakasirisha wenzake na kuamua kumfikisha kituo cha Polisi.

Kamanda ameongeza kuwa suala hilo tayari limefikishwa Polisi kitachoendelea ni ushahidi ukitosheleza kijana huyo atapelekwa mahakamani.

No comments

Powered by Blogger.