Header Ads

KUMBE SHAMSA FORD ANAKARIBIWA KUCHUMBIWA NA CHIDI MAPENZI

UBUYU uliokolea rangi jijini ni kwamba staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford anadaiwa kuchumbiwa na mfanyabiashara maarufu Bongo, Chid Mapenzi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na mwanaume huyo kilieleza kuwa, wawili hao wapo kwenye mipango lukuki ya kufunga pingu za maisha na mwanzoni mwa wiki hii Chid alifunga safari hadi ukweni mkoani Dodoma kutoa mahari ambayo haikufahamika ni kiasi gani cha fedha.

Baada ya kuunasa ubuyu huo, shushushu wetu alitafuta ‘kontakti’ za msanii huyo aliyewahi kujizolea umaarufu na Filamu ya Chausiku, alipoulizwa alionesha mshktuko na kuangua kicheko;
 “Khaa! Huo ubuyu kiboko, hakuna kitu kama hicho jamani, mimi yule ni mtu wangu wa karibu tu isitoshe kwetu siyo Dodoma, watu bwana!”
JE? ulipitwa na taarifa yoyote na bado unatamani kuijua Zaidi basi Karibu bado unanafasi  ya kupitia yote hayo kwakuwa blog yako imekukumbuka na kukuifadhia mambo haya muhimu.Pitia account hizi ili Uwe karibu zaidi na habari zote Zinapotoka Zikufikie Hapo kwa papo.
FACEBOOK PAGE ....INSTARGRAM....TWITTER.

No comments

Powered by Blogger.