Header Ads

WASTARA, NUSURU MIMBA INITOE ROHO

Siku chache zilizopita, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma alikiri na kufunguka kuwa ni mama kijacho baada ya kunasa ujauzito lakini taarifa za kusikitisha zilizolifikia gazeti hili mapema wiki hii zimedai kwamba, mimba hiyo imechoropoka katika mazingira ambayo yalitaka kuutoa uhai wake.

Chanzo makini ambacho ni ndugu wa mwigizaji huyo kilichoomba hifadhi ya jina kilidai kuwa, kweli Wastara alikuwa na mimba lakini haikuwa riziki kwani imechoropoka katika mazingira ya ajabu.

“Baada ya kuzinguana na Sadifa (Khamis Juma) Wastara aliamua kuchukua hamsini zake. Baadaye aligundua amenasa na tulipomuuliza alisema si ya mtu mwingine zaidi ya mumewe Sadifa.

“Sasa, hivi karibuni alikwenda Msumbiji kufanya biashara zake za madini. Akiwa kule, akajiwa na hali f’lani mbaya ambayo ilimuweka kwenye wakati mgumu sana.

“Alichodai ni kwamba mimba imemsumbua sana na nusura imuue, tukamuuliza ameamua kuitoa au imetoka yenyewe? Hakutujibu chochote,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:

“Siku chache baadaye alinitumia SMS na kuniambia anamshukuru Mungu anaendelea vizuri. Hata alipotua Bongo, sikumsikia tena akizungumzia habari ya mimba na hata kwa kumuangalia tu ilionesha kwamba imechoropoka.

IJUMAA LAMSAKA WASTARA

Baada ya kunasa ubuyu huo, Jumatatu iliyopita, Ijumaa lilifanya jitihada za kumsaka Wastara kupitia simu yake ya kiganjani lakini mara kadhaa ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Siku iliyofuatia paparazi wetu alimpigia tena. Pia haikupokelewa na baadaye msanii huyo akatuma SMS aliyoandika ‘tuma meseji’.

Ijumaa: Mimi ni Mwandishi wa Ijumaa, naitwa (mwandishi anajitambulisha), kuna habari kuwa mimba yako ambayo ilikuwa inadaiwa ni ya aliyekuwa mumeo imetoka, kuna ukweli wowote?

Wastara: Nani kawaletea hizo habari?

Ijumaa: Ni vyazo vyetu, tukaona ni busara kukuuliza wewe ili kupata ukweli.

Wastara: Jamani niseme tu kwamba napitia kipindi kigumu sana kwa hiyo naomba uniache.

Ijumaa: Kipindi gani kigumu? Au ndiyo kutokana na mimba hiyo kuchoropoka?

Wastara: Hujui niko kwenye hali gani, kwa hiyo niache, muda wa kulizungumzia hilo ukifika nitasema.

Chanzo:GPL

No comments

Powered by Blogger.