MFUNGWA MKONGWE DUNIANI AACHIWA HURU.
Mwanamke mmoja raia wa Bangladesh ambaye anakisiwa kuwa ndiye mfungwa mkongwe zaidi ameachiwa huru.
Ohidunessa
mwenye umri wa miaka 100 alihukumiwa kifungo cha maisha jela kimakosa
kwa mauaji ya mwanafamilia wake yapata miaka 20 iliyopita.
Bi kizee huyo hata hivyo alipata afueni baada ya jaji mkuu wa nchi hiyo Surendra Kumar Sinha, kuingilia kati.
Bibi huyo alifaulu kuishawishi mahakama ya rufaa kumuachilia.
Ohidunessa kwa sasa haoni kwa hivyo anahitaji msaada kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Kufikia sasa ametumikia miaka 20 ya kifungo chake cha maiasha
Post a Comment