Header Ads

CHADEMA WATANGAZA KUPAMBANA NA UDIKTEKTA (UKUTA)

Leo Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya kikao chake katika Hoteli ya Bahari Beach Ledger Plaza.
Mojawapo ya Maazimio ya Kikao hicho ni kuundwa kwa kile walichokiita Umoja Wa Kupinga Udikteta Tanzania(UKUTA). Tuweke Kumbukumbu sahihi, Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoketi siyo Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Hii ina maana kwamba maazimio ya kuundwa kwa UKUTA ni matakwa ya Chama kimoja yaani CHADEMA. Ikumbukwe kuwa UKAWA uliundwa kwa makubaliano ya vyama vinne vya CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD. Hakuna namna yoyote ya kuwashawishi Watanzania kuwa hiki wanachokiita UKUTA ni Umoja, Umoja lazima ushirikishe pande watu zaidi ya mmoja au zaidi ya vikundi viwili au zaidi ya vyama viwili.

Mtazamo: Kabla ya UKAWA, Kambi rasmi ya Upinzani iliundwa na chama kimoja cha CHADEMA. Ni katika kipindi hicho ambapo Chadema na CUF walikuwa na msuguano mkubwa hadi kupelekea CHADEMA kuwaita CUF , CCM B huku CUF wakiwaita CHADEMA chama cha MASHOGA.

Baada ya Chadema kuondokewa na Makada wake maarufu walioshiriki kikamikifu kukijenga chama wakiongozwa na Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, CHADEMA kiliyumba sana na kutafuta kila namna ya kukinusuru na anguko kuu. Ndipo Mungu aliposikiliza maombi yao na bila kutarajia, Ibrahim Harouna Lipumba akaibuka na wazo la kuundwa kwa UKAWA wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

CHADEMA wakaingia kwenye umoja huu kwa malengo makubwa ya kufufuka jambo ambalo CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD hawakujua. Haraka sana, Mbowe akaenda kutangaza kulivunja baraza kivuli lililokuwa na Wabunge wa Chadema pekee na kuunda jipya lenye kujumuisha Wabunge wa UKAWA. Ni katika umoja huo wa wajanja CHADEMA na mambumbumbu wa CUF, NCCR na NLD uliokipaisha chadema na kwa ujanjajanja hio CUF, NCCR na NLD wakajikuta wanamuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA huku viongozi wa CUF, NCCR na NLD wakitumiwa kama vibaraka na wale wa CHADEMA. NCCR, NLD na CUF vimebaki majina.

Uamuzi wa CHADEMA leo wa kuuda UKUTA si chochote wala si lolote. Hizi ni hila tu vinafanyiwa vyama vya NCCR, CUF na NLD. Chadema wameona wameshajiweza, wanaamua kujivua GAMBA kutoka katika mikono ya UKAWA ili wajitegemee
Swali ni je CUF, NCCR na NLD wanalijua hilo? Wako tayari kuitwa washirika wa UKUTA wakati UKUTA umetokana na maazimio ya KAMATI KUU YA CHADEMA? Je UKUTA hautawapoteza viongozi makini kama ambavyo UKAWA ukiwapoteza akina Dr. Slaa na Prof. Ibrahim Harouna Lipumba

No comments

Powered by Blogger.