Header Ads

NEWS:RAISI MAGUFULI AAHIDI KUJENGA BARABARA YA UBUNGO MAENEO Y...............(SOMA ZAIDI)

Rais MAGUFULI aahidi kujenga barabara ya UBUNGO KIBANGU
Rais JOHN MAGUFULI ameahidi kuifanyia matengenezo Barabara ya UBUNGO EXTERNAL kwenda UBUNGO KIBANGU Jijini DSM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabara inayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside
Rais JOHN MAGUFULI ameahidi kuifanyia matengenezo Barabara ya UBUNGO EXTERNAL kwenda UBUNGO KIBANGU Jijini DSM ili kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi wa maeneo hayo.

Akizungumza na waumini wa Kanisa la MAOMBEZI, lililopo UBUNGO KIBANGU, Rais MAGUFULI amesema ujenzi wa barabara hiyo utaanza baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Rais MAGUFULI ambaye ametembelea Kanisa hilo la MAOMBEZI akiongozana na Mkewe Mama JANETH MAGUFULI, amesema ataendelea kuwa Mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu huku akisisitiza kuwatumikia Watanzania bila kujali tofauti zao za kidini.

Mchungaji Mkuu wa Kanisa la MAOMBEZI, ANTHONY LUSEKELO ameipongeza hatua ya Rais MAGUFULI ya kuifanyia matengenezo Barabara ya UBUNGO EXTERNAL kwenda UBUNGO KIBANGU kwani itasaidia kuondoa kero ya usafiri kwa Wakazi wa eneo hilo.

Baadhi ya Waumini wa kanisa hilo wamesema wamefarijika kupata ugeni wa Rais MAGUFULI na kuahidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili afanikishe mipango yake ya kuliendeleza taifa hasa katika kukuza uchumi na kuondoa kero zinazowakabili wananchi.


No comments

Powered by Blogger.