Header Ads

NEWS: STEVE NYERERE AWAPONGEZA WAKINA HARMONIZE NA MOZE IYOBO KWA KUW.........(SOMA ZAIDI)

Kiongozi wa zamani wa Bongo Movie Unit,  Steve Nyerere amempongeza msanii wa muziki, Harmonize pamoja na dancer wa Diamond, Mosei Iyobo kwa kuwapa utulivu wasanii wenzake wa filamu Aunt Ezekiel na Jacqueline wolper.
Muigizaji huyo ambaye alikuwa MC katika iftar ya GSM iliyofanyika Kigamboni weekend hii na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, alisema anawashukuru wasanii hao wa muziki kwa uwamuzi wa kuwahifadhi dada zake hao.

“Mimi nashukuru wasanii wa bongofleva kwa kuwahifadhi dada zetu, Aunt yupo poa, na Wolper naona safi,” alisema Steve Nyerere huku akicheka.

Wolper na Harmonize kwa sasa ni wapenzi na kila mmoja anaonyesha anampenda mwenzake, na Aunt Ezekiel na Mose Iyobo ni wapenzi wa muda mrefu na wanaishi kama familia na mtoto wao mmoja aitwae Cookie.

No comments

Powered by Blogger.