MKURUGENZI wa kundi la Wanaume Family na Yamoto bendi, Saidi Fella
maarufu Mkubwa Fella, amesema yeye na meneja wa msanii, Diamond
Platnumz, Babu Tale, wameamua kumsaidia mkali wa rapu, Rashid Makwiro
‘Chid Benz’, arudi katika sanaa yake na si kujiunga na kundi lolote.
Fella alisema msanii huyo kwa sasa wamemwanzishia mazoezi maalumu ya
kumwezesha kurudisha mwili wake na pumzi ili aweze kurudisha makali yake
katika uimbaji bila kuchoka.
“Chid Benzi hawezi kujiunga na Wasafi kwa sasa mimi na Babu Tale
tumekubaliana tumsaidie yeye kama yeye na si kujiunga na kundi lolote
lakini kama anataka kujiunga na lebo yoyote hilo litakuwa la kwake,” alifafanua Mkubwa Fella.
Post a Comment