Baada ya kupost picha akiwa na Mwana FA baada ya kuoa na kuandika maneno
yanayoashiria naye hivi karibuni atafuata nyayo za Mwana Fa, Dully
Sykes ameruka viunzi na kusema hana mpango wa kuvuta jiko leo wala
kesho.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully amesema yeye
kwake kuoa ni sawa na maji kufuata mkondo, kwana hata marehemu baba yake
hakuwahi kuoa wakati wa uhai wake.
“Kila mtu ana mipango yake, maji hufuata mkondo, wewe nafikiri mzazi
wako alioa, mi baba yangu hakuwahi kuoa”, alisikika Dully akielezea
sababu ya yeye kutoamua kuoa mpaka leo.
Pamoja na hayo Dully amesema akiona kuna umuhimu na ikiwezekana ataoa,
hivyo amewataka wadau wake wamuombee ili aweze kuwa na mawazo ya kuoa na
kuwa na mke rasmi.
“Kama inawezekana naweza kuvuta jiko, na kama haitowezekana sitavuta
jiko, kwa sababu sijafikiria bado, mniombee nipate mawazo ya kuchukua
jiko, sio kwa vile FA amefanya basi ndo uone inawezekana, nina sababu
zangu tu mwenyewe, nikikwambia ntakuvunja moyo kama umeoa wewe”, alisema
Dully Sykes
Post a Comment