Header Ads

JADA WA BONGO MOVIE, APOTEZA KUMBUKUMBU....Watanzania waombwa kumuombea.

Msanii aliekuwa anachipukia na kuja kwa kasi kwenye tasnia ya uigizaji hapa nchini JADA.amepoteza kumbukumbu zake akiwa anashoot.

Mtunzi na msimamizi wa video nyingi za maigizo Leah Mwendamseke maarufu kama Lamata,aliyazungumza hayo wakati akihojiwa kwenye kipicha cha redio ya Magic Fm.

"Tulikuwa tumesha maliza vipande vyake na muda kidogo aliomba kwenda msalani hata hata baada ya yeye kwenda alichukua muda mrefu huko,tulipoenda kumuangalia tulimkuta ni kama mtu aliezimia na muda huo alikuwa ameanguka kwenye mlango wa choo.Baada ya kumpeleka kituo cha afya na baada ya kufumbua macho hakuyutambua kabisa na hata jina lake pia hakulijua. Hali yake bado haijawa sawa japo tunasubiri majibu ya dokta kutujuza zaidi,Mi nawaomba watanzania wamuombee zaidi ili rudi kwenye hali yake ya kawaida.

No comments

Powered by Blogger.