Header Ads

NEWS;WABUNGE WAPYA WALIOTEULIWA NA NEC HAWA HAPA NA HABARI ZAIDI {SOMA ZAIDI}

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ulifanyika huku baadhi ya majimbo ya uchaguzi, uchaguzi uliahirishwa kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali. Tume ya Uchaguzi iliteua jumla ya Wabunge wanawake wa viti maalum 110 kati ya 113 ambapo viti vitatu vilibakizwa kusubiri uchaguzi wa majimbo nane ambayo uchaguzi wake uliahirishwa.
Chama cha Mapinduzi ‘CCM’, Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ na Chama cha Wananchi ‘CUF’ ndivyo vimetajwa kuendelea kuhusishwa kwenye mchakato wa kugawanywa viti 3 vilivyobaki kutokana na kupata angalau asilimia 5 ya kura halali za ubunge.
Leo March 24 2016 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ‘NEC’ imewateua ndugu Ritha Enespher Kabati na Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ na ndugu Lucy Fidelis Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kuwa wabunge Wanawake wa viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uteuzi huo umefuata mtiririko wa orodha iliyowasilishwa na katibu wa Chama husika ambapo CCM iliwasilisha majina nambari 65 na 66
65.Ritha Enespher Kabati
66.Oliver Daniel Semuguruka
Katika Orodha iliyowasilishwa na CHADEMA jina nambari 37

No comments

Powered by Blogger.