Pages

6/29/2016

NEWS; BASATA WAIKATAA CHURA PART 2 SNURAA AMMUA KUM.........(SOMA ZAIDI).(

Bodi ya filamu Tanzania imeikataa script mpya ya video ya Chura ya Snura.

Mwezi na nusu uliopita, Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo iliifungia video ya wimbo huo na kumwagiza Snura awasilishe script mpya ambayo hata hivyo baada ya kufanya hivyo nayo imekataliwa.

Akiongea na 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, Snura alidai kuwa baada ya bodi hiyo kukaa kwenye kikao iliona kuwa bado script mpya inataka kufanana na video iliyopigwa marufuku na kumkataza kushoot.

Amedai kuwa jibu hilo lilimchanganya na kumrudisha nyumba na kwamba video ya pili alipanga kuwepo mwenyewe na wala hatocheza zaidi kutembea.


‘’Nilipeleka script a video mpya ta Chura bodi ya filamu ilichukua muda kidogo kuipitia nilifuatilia sana ndio nikapewa majibu baada ya wao kukaa kikao na kupitia wakaniambia kuwa ile script hwajaikubali nishuti kwasababu wanasema maudhui yake yanataka kufanana na ile video ya mwanzo.

Nilishindwa kuelewa kwasababu kwa uelewa wangu niliona nimeandika kitu tofauti kwasababu video ya mwanzo ilikuwa imechezwa kwenye maji na wanawake ndio walikuwa wanacheza lakini video hiyo ambayo niliyokuwa nimeiandika ilikuwa ni mimi mwenyewe ndio nitakuwepo kwenye hiyo video halafu sichezi natembea huku naimba.

Halafu watu wananiona mie natembea huku naimba na wao wananifuata kwa nyuma huku wanacheza naenda napanda daladala na wao wanapanda nikishuka na wao wanashuka huku wakicheza’’ Alisema Snura

6/28/2016

NEWS:TRAFIKI ALIE TUKANWA NA MKE WA WAZIRI APAN......(SOMA ZAIDI)

Deogratius Mbango, askari wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki) ambaye hivi karibuni alitukanwa na mke wa waziri wa serikali ya awamu ya tano (jina kapuni), baada ya kulikamata gari lake kwa kuvunja sheria za barabarani, hatimaye amepandishwa cheo ikiwa ni maagizo ya Rais Dk. John Magufuli.

Habari kutoka chanzo cha uhakika, zinasema kuwa askari huyo ambaye alilikamata gari la mke wa waziri huyo baada ya kuvuka sehemu ya waendao kwa miguu eneo la Namanga jijini Dar es Salaam, amepandishwa hatua moja mbele, kutoka koplo hadi sajenti.

Kitendo hicho cha kulikamata gari hilo, bila kujali utambulisho na matusi ya mwanamke aliyedai kuwa mke wa waziri, kilimfanya Rais Magufuli kumsifu na kumuona kuwa jasiri kazini kwake, hivyo kuliagiza jeshi la Polisi kumpa promosheni mara moja.

Juzi Jumapili, Uwazi lilimkuta trafiki huyo akiongoza magari maeneo ya Makumbusho katika lango la kuingilia daladala akiwa na cheo kipya cha usajenti.

Alipoulizwa kuhusu kuula huko, Mbango alikiri kutokea kwa jambo hilo na kumshukuru Mungu pamoja na uongozi wa Jeshi la Polisi kwa kumkumbuka, huku pia akilishukuru gazeti hili kwa kukumbushia katika toleo lake Na 993 lililoripoti juu ya kutotekelezwa kwa amri ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NEWS; DOGO JANJA AWAAMBIA KUKOSA TUZO KWA DIAMONDI ISIWE SABABU Y.........(SOMA ZAIDI)



Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amewataka mashabiki katika mitandao ya kijamii kuacha kuandika maneno ya kumbeza Diamond Platnumz baada ya kukosa tuzo ya BET na kuchukuliwa na Black Coffee kutoka Afrika Kusini.

Rapper huyo ambaye ameachia remix ya wimbo ‘My Life’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha Radio & Weasel kutoka Uganda, ameiambia Bongo5 kuwa hatua aliyoifikia Diamond kimataifa ni kubwa hivyo anapaswa kupongezwa.


“Unajua watu walikuwa wanamatarajio makubwa sana na tuzo lakini mwisho wa siku tukubali matokeo ya kushinda na kushindwa,” alisema Dogo Janja.

Aliongeza,

“Diamond bado ni mshindi, alikuwa mtanzania pekee, kwa hiyo huu sio wakati wakumbeza, tumtie moyo ili aendelee kupambana zaidi,”

Diamond ni msanii pekee wa Tanzania ambaye alikuwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo hiyo ambayo ilichukuliwa na msanii kutoka Afrika Kusini.

6/27/2016

NEWS: HIKI NDIO KILICHO MFANYA DIAMOND PLATNUMZ KUKOSA..........(SOMA ZAIDI)

Ni masikitiko yangu makubwa kuikosa Tuzo hii ya kimataifa kupitia msanii wetu pekee na Brand ya Afrika mashariki.
Bila kupoteza muda
Na hizi ni sababu zilimfanya Chibu Dangote

1) Hakuwa na kazi inayoeleweka ambayo ingemfanya aongeleke au jina lake lizunguke vichwani mwa watu

2) Kumanage wasanii kwake limekua pigo kubwa maana imemfanya aache kusonga mbele akiamini amefika na ni muda wa kusaidia wengine.

3) Kukosa baraka za mzazi mwenzake mama Tiffah kutokana na usaliti aliomfanyia mwenzake.

4) Kurise up kwa Alikiba.

5) Kuridhika na mafanikio

Hivyo Chibu ajipange upya upya ili arudi kwenye mstari.

 

NEWS: AFARIKI BAADA YA KUPIGWA VIBOKO NA WAZEE WA FAMIL.....(SOMA ZAIDI)

Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Kandashi, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro, Abedi Akyo (53), amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchapwa viboko na wazee wa kimila kwa tuhuma ya kujihusisha na wizi wa kuku.
Akielezea mazingira ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilfred Mutafungwa amedai kuwa Akyo alichapwa viboko 70 na wazee hao wa kimila wa Kimeru na Kimasai.

Mutafungwa amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwezi uliopita  wakazi wa Kata ya Karansi wilayani hapa  walitoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.

 

NEWS:SHAGGY, ALIKIBA ALITAKA KUNIUWA KWA MAPENZI KIAS A........(SOMA ZAIDI)

MSANII anayefanya muziki na filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kwa kinywa chake kuwa penzi la mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Ali Salehe Kiba ‘Alikiba’ lilitaka kutoa uhai wake kwani hakuna mwanaume aliyemshika mtima wake zaidi yake.


Akizungumza na gazeti hili juzikati, Sabby anayedai ana historia ya kutendwa na wanaume alisema kuwa amewahi ‘kudate’ na wanaume wapatao saba lakini kati yao hakuna aliyemdatisha zaidi ya Kiba ila jamaa huyo alitaka kusababisha ajitoe uhai.


“Jamani haya mapenzi yaacheni hivihivi, huwezi kuamini Alikiba alitaka kuniua kwa penzi lake, nilimpenda sana na alinidatisha kiasi kwamba nilipokuwa nikihisi ananisaliti, niliumia roho na wakati mwingine kupata presha.
“Achilia mbali hilo, kuna wakati nilitaka kujiua kwa sababu yake maana kuna kitu kilitokea, nikaumia sana hadi nikahisi sina umuhimu wa kuishi,” alisema mdada huyo.

Inadaiwa Sabby na Kiba waliwahi kuwa wapenzi kwa siri na haikuchukua muda mrefu wakamwagana kwa sababu ambazo wanazijua wenyewe.
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Kiba angalau agusie kidogo uhusiano wake na binti huyo ulivyokuwa lakini hakuweza kupatikana mara moja.

NEWS:SIMBA WAMTUMIA HAJI MANARA KUWAJIBU YANGA KWA KI........(SOMA ZAIDI)

Awali ya yote klabu inaendelea kutoa pongezi kwa ndugu zetu Waislaam wanaoendelea kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani tunaamini Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kwa ibada hiyo muhimu.

Ndugu wanahabari katika siku za karibuni hususan kuelekea mchezo wa Yanga na klabu kutoka Congo DRC  TP Mazembe Englebert kumekuwa na maneno mengi kutoka klabu ya Yanga yakiishutumu klabu yetu kuhusiana na kutokutoa ruhusa kwa mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ na pia kuhusiana na namna mashabiki watakavyokaa majukwaani siku ya mchezo huo Jumanne ya wiki hii.

Klabu ya Simba kwa maksudi kabisa inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na mambo hayo mawili yanayoleta sintofahamu miongoni mwa wadau wa mchezo huu murua wa kandanda.

Hakuna barua yoyote ambayo klabu ya Yanga imetuandikia kuhusiana na suala la mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ pia hakuna hata mazungumzo yaliyofanyika baina ya viongozi wa vilabu hivi ili kutuomba walau kwa mdomo kama taratibu zinavyotaka.
Ikumbukwe Simba huwa haina tatizo kuruhusu matakwa binafsi ya mchezaji na nyote mnajua utamaduni huo wa klabu yetu.

Kwa wasiofahamu mwaka 1998 klabu ya Simba iliwaazima wachezaji watatu Yanga ili wacheze hatua ya makundi kama hii ya klabu bingwa Afrika wachezaji hao ni Shaban Ramadhani Monja Liseki na Alphonse Modest sasa jiulize kama tuliweza kuwaazima wachezaji vipi tushindwe kumruhusu mchezaji waliyemsaini? Pamoja na maneno yao ya kuudhi Simba ni waungwana wa kutosha na wao wasitumie ukimya wetu kuwapotosha wanachama na washabiki wao eti tumewakatalia kuwajibu barua ya Hassan Ramadhani ‘Kessy’
Msimamo wetu kuhusiana na jambo hili inategemea uungwana wao tu.

Pia Yanga kupitia msemaji wao wamenukuliwa kuwa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe watakaa kwenye majukwaa yote hata yale ambayo kwa utamaduni wa uwanja wa taifa hukaliwa na mashabiki wa klabu yetu.

Tunafahamu kuwa kauli hii ina nia ya kuchochea vurugu kubwa kwenye mchezo huo na sote tunajua athari ya vurugu michezoni tunawashauri Yanga wasijaribu kuleta mashabiki wao kwenye majukwaa wanayokaa washabiki wa Simba ili kuleta amani siku hyo ya mchezo.matarajio yetu vyombo vinavyohusika vitasimamia kwa ukaribu jambo hilo.

Mwisho ingawa si kwa umuhimu klabu haimzuii yoyote kushangilia timu yoyote siku ya mchezo huo kama zilivyo desturi ya wao Yanga kushangilia klabu yoyote inayocheza na Simba hususan wageni toka nje.kama ilivyokuwa miaka michache nyuma ambapo walishangilia na kuvaa jezi za TP Mazembe.

Waarabu wana msemo wao maarufu “KAMA TUDINI TUDANI” kama ulivyofanya na wewe utafanyiwa hivyohivyo.

Imetolewa na
Haji S Manara
Mkuu wa habari
Simba Sports Club

NEWS: DIAMOND AKOSA TUZO ZA BET AWARDS NA HUYU NDO ALIE.......(SOMA ZAIDI)

Mwanamuziki Diamond usiku wa jana ameikosa Tuzo ya BET ya Best International Act Afrika aliyokuwa akiiwania, Tuzo hiyo imeenda Kwa DJ, Black Coffee wa South Africa.


 

NEWS: WAALIMU WENYE VYETI FEKI WAOBWA KUJISALIMISHWA MIKONONI MW.......(SOMA ZAIDI)

Nimekutana na hii "barua" mahali.Inavyoonekana muda si mrefu wenye vyeti "vya hapa na pale" wataanza kutafutana.
Likisimamiwa vizuri ni zoezi zuri na lenye tija kwa Taifa. Ila kwa upande mwingine tujiandae kwa "deficity" ya wale watakao "katwa"

 

NEWS; UKIMWI SASA KUPIMWA NYUMBA HADI NYUMBA KWA KUW........(SOMA ZAIDI)

Gazeti la JamboLEO limeripoti kuwa Serikali inakusudia kufanya utafiti kwa kupima virusi vya UKIMWI (VVU) nyumba kwa nyumba kuanzia ngazi ya kaya, ili kupata takwimu sahihi kuhusu hali ya maambukizi mapya ya ugojwa huo ulivyo sasa nchini.

Aidha gazeti hilo limeongeza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa ambapo alisema utafiti huo utakaotumia teknolojia ya kisasa, unalenga kupima viashiria na matokeo ya UKIMWI nchini, ili kujua ni kiwango gani Tanzania imepiga hatua katika kupamban na ugonjwa huo.

Gazeti hilo limemnukuu Dk Albina Chuwa akisema

”utafiti huo utafanyika kwa kutumia sampuli wakilishi ya kaya takribani 15, 800 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa kufikia walengwa 40, 000 wakiwamo watoto wasiopungua 8, 000′

NEWS: PAUL MAKONDA KUWAPA ZA USO WAKANDARASI WENYE KUT.....(SOMA ZAIDI)

SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam, imeifutia  kibali kampuni ya Ukandarasi ya Ishinomya  cha  kufanya ujenzi wa  barabara za halmshauri zote za jiji la Dar es Salaam kutokana kujenga barabara chini ya kiwango huku kampuni tatu zimetakiwa zisipewe zabuni mpaka pale watakapojiridhisha.

Akizungumza na waandishi habari jijini  Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kampuni zimekuwa ukandarasi zimekuwa zikifanya kazi chini ya kiwango ili barabara iharibike kwa ajili ya kupata zabuni nyingine.

Amesema kuwa hatuwezi kufika kwakuwa na barabara zenye kiwango cha chini  na kuendelea kuwepo kwa kampuni hizo ambazo zinajenga barabara chini ya kiwango na wanapofika mwisho nyuma zimeharibika.
Amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam barabara zina mashimo kutokana na kampuni kufanya kazi kwa mazoea.

Kampuni ambazo zimesimamishwa kufanya ukandarasi wa barabara mpaka wajiridhishe ni Germinex,  Delmonte  pamoja na Skol .
Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam ndani ya mwezi mmoja kuwe hakuna barabara inayokuwa na mashimo na ni agizo  ambalo wanatakiwa kutekeleza.

6/26/2016

NEWS: IDADI WA MADADA WANAO TEMBEA BILA KUVAA NGUO ZA NDANI YAONGEZEKA KWA........(SOMA ZAIDI)

Dada zetu siku hizi hawapendi kuvaa chupi kabisa.Wenyewe wanadai wanataka wapigwe upepo kunako. 
Sasa wengine nguo wanazovaa ni hatari tupu,unakuta kavaa nguo laini na mzigo kajaliwa huo mtikisiko sasa mpaka presha zinatupanda. 
Na wengine mpaka tamu yote inaonekana. Dada zetu hembu tuoneeni huruma sisi watoto wa watu. Tunajua ni utandawazi lakini sasa mmezidisha.

NEWS:HIVI HAPA VYAKULA VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME KWA.......(SOMA ZAIDI)

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.

Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.

Sababu za kukosa nguvu za kiume

 Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema,utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?

Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:

Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya TestosteroneKupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.



1. Blueberry



Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.



2. Mtini (Figs)



Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)



Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.

Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.

4. Karanga

 

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

5. Vitunguu saumu



Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.



6. Ndizi



Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).

7. Chocolate



Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vyaphenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.



Vyakula ni bora kuliko madawa makali

Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.

Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.

Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.

Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.

NEWS: JAMAA AOWA WANAWAKE WANNE KWA WAKATI MMOJA AMESEMA AMEFAN......(SOMA ZAIDI)

Mwanaume mmoja nchini kuwaiti jana ameweka rekodi ya peke yake baada ya kuamua kufunga pingu za maisha kwa kufunga ndo hiyo kwa wanawake wanne tofauti amabo nao piawalikuwa wakifurahia kitendo hcho alicokifanya mme wao huyo mpya.

NEWS:SHILOLE AANZISHA LEBO YAKE AAMUA KUMSAJILI HUYU ALIEK........(SOMA ZAIDI)

Msanii wa muziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameanzisha label yake mpya ‘Shilole Entertainment’ ambapo pia amemsaini msanii chipukizi aitwae ‘Amaselly’.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘SayMyName’, amekiambia kipindi cha Clouds E kinachoruka katika runinga ya Clouds TV, kuwa ameamua kuanzisha label hiyo ili kuwasaidia wasanii wenye vipaji lakini hawapati nafasi.

“Yeah nimemsani Amaselly aka Gaucho, kwa sababu ni msanii mwenye heshima, amenitafuta kwa muda mrefu, Shilole nisaidie nisaidie, kwa hiyo nikajifikiria, nikaamua kumsaidia,” alisema Shilole
Pia Shilole amesema amemsaini msanii huyo kupitia label yake mpya iitwayo Shilole Entertainment.
Kwa upande wa Amasely alimshukuru Shilole kwa uwamuzi wa kumsaidia huku akihaidi mambo mazuri

NEWS: CHIDI BENZI ATOA YA MOYONI ASEMA KILICHOMFANAYA ATUMIE MADAWA.........(SOMA ZAIDI)

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Chidi Benz amefunguka na kueleza jinsi wadau wa muziki nchini wanavyosababisha wasanii wa muziki kuingia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya.


Rapper huyo ambaye ameachana na matumizi ya Madawa ya kulevya hivi karibuni, ameiambia BBC kuwa wasanii wengi wanaingia kwenye Madawa ya kulevya baada ya kupata stress za kubaniwa kwenye muziki.

“Watu wanamsongo wa mawazo, mashabiki wetu hawajui sisi jinsi tunavyodeal na watu ambao wanatufikisha kwao, wadau wa muziki, wadau wa muziki ni watu tofauti sana na wanafanya vitu vibaya sana,” alisema Chidi. “Wachache wapo wanaosaidia vizuri, lakini ni wengi wanaoharibu na wanaharibu sana sana, yaani mtu anakuwa na kisasi na wewe na yupo tayari kukufanyia kitu chochote, akushushe, akupinguze mpaka umalize pesa zote na usipingwe hata wimbo wako mmoja,”

Pia rapper huyo alisema wasanii wengi wanabaniwa kutokana na migongano ya kimaslahi katika kazi au kushare mademu na wadau wa muziki.

“Huu muziki tunaoufanya na haya maneno tunayoyaimba, kuna wale ambao wanachukulia starehe na kuna wengine wanachukulia unawasema au mabinti zao wanatupenda sisi wasanii. Unakuta kuna binti amekupenda wewe msanii, kumbe yule ana mtu mwingine au mdau, sasa huyo mtu akisikia kwamba Chidi Benz anadeal na mtu wake, hawezi kuelewa kwamba mtu wake ndio anamfuata Chidi Benz, ila yeye atakufanya kitu chochote kile ili akuumize au akuharibu na ‘akustopishe’ maendeleo yako. Na inawezekana yule mtu wewe haukudeal naye ila anakupenda tu kishabiki na anawaambia marafiki zake hivyo lakini marafiki zake inatokea wakaibadilisha na wakaiweka kimapenzi, tayari una vita na mtu wake ambaye anamwangalia,” alisema Chidi.

Pia rapper huyo amedai kilichomwingiza yeye kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya ni kutochezwa kwa ngoma zake kwenye redio na runinga hali ambayo ilimfanya ajione mpweke

6/25/2016

NEWS: KAJALA MIMI NA MSAMI TULISHA MALIZANA LAKINI KWA.......(SOMA ZAIDI)

Msanii wa filamu Kajala Masanja amekanusha tetesi za kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na mkali wa wimbo ‘Mabawa’, Msami.
kajala

Mwingizaji huyo ambaye hivi karibuni ilisambaa video inayomuonyesha akidendeka na rapa Quick Rocka, ameiambia Clouds Fm kuwa Msami ni mshkaji wake wa karibu sana na sio mpenzi wake.

“Unajua kuna watu wanaweza wakawa labda ni washikaji au wana vitu vingi pembeni lakini watu wengine hawajui, mi na Msami ni washkaji sana,” alisema Kajala.

Aliongeza, “Halafu sio kila siku watu watakuwa wanatuona barabarani au tunapostiana picha kwenye Instagram, lakini mimi na yeye tunaongea vitu vingi, kwa hiyo imekuwa rahisi mimi kuacha usingizi wangu kuja kwa Msami, sina uhusiano naye na vitu vingine mtavijua baadaye.”

Wawili hayo wamekuwa wakioneka wakiwa pamoja mara nyingi hali ambayo imeibua hisia huenda wakawa wanatoka kimapenzi.

NEWS; ZARI AMPA BARAKA ZA MWISHO DIAMOND PLATNUMZ KWAAJIL.......(SOMA ZAIDI)

Hakuna baraka za muhimu kuzipata kama zile za mzazi wako na zile za mtu umpendaye.

Kwa mwanaume baraka kutoka kwa mke wake zina nguvu mno hasa kwakuwa maandiko matakatifu yanasema kuwa mwanamke alitokana na ubavu wa mwanaume. Mrs Nasib Abdul, Zari amempa baraka zake mpenzi wake Diamond ambaye amesafiri kwenda Los Angeles, Marekani kwenye tuzo za BET. Diamond ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa.

“Safari njema. May the Good Lord be with you all the way. Praying you bring the BET Award back to East Africa…. xoxo😍 @diamondplatnumz,” ameandika Zari kwenye Instagram.

Hata hivyo kipengele hicho kina upinzani mkubwa mwaka huu. Msanii pekee ambaye ni tishio kwa Mond ni Wizkid. Staa huyo wa Nigeria mwaka huu amefanya mambo makubwa ikiwemo kushirikishwa na Drake kwenye wimbo ‘One Dance’ ulioshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 kwa wiki sita mfululizo. Pia amezunguka na Chris Brown kwenye ziara yake ya One Hell of A Nite’ barani Ulaya.

Wasanii wengine wanaowania kipengele hicho ni AKA, Cassper Nyovest, Yemi Alade na wengine.

NEWS:NUH MZIWANDA MAFANIKIO YANGU YANAMPA MAUMIVU- SHILOLE

Vita vya maneno kati ya Nuh Mziwanda na ex wake Shilole haviishi.

Hata hivyo ni Nuh Mziwanda ndiye anayeonekana kuendelea kurusha makombora mengi zaidi kumzidi mwenzake.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka, Nuh ameibuka na jingine kuwa kusema kuwa mafanikio aliyonayo sasa yanampa stress Shishi.

“Haamini ndani ya moyo wake ndio maana ameanza kupanick, lakini inabidi akubali matokeo kuwa mimi ni mwanamuziki na yeye ni mcheza show,” alisema Nuh.

Muimbaji huyo wa Jike Shupa amedai kuwa baada ya kuachana, Shilole aliamini kuwa maisha yatamwendekea kombo Nuh. Hata hivyo Nuh anasema anatamani ex wake huyo asingekuwa na kinyongo naye kwakuwa kila mmoja kwa sasa ana maisha yake na asiendelee kutaka kushindana naye.

Kwa upande mwingine, Nuh amesema girlfriend wake wa sasa ni wife material na atamuoa.


Tayari wawili hao wameshajichora tattoo za majina yao kuashiria kuwa wanapendana kwa dhati. Nuh amesema anadhani anaweza kuwa amempata ‘the one.’

“Kiukweli hapa nimefika,” alisema.

Nuh aliwahi kumvisha pete Shilole na kujichora tattoo ya jina lake ambayo hadi sasa anayo.

6/24/2016

NEWS:RICH MAVOKO NITA BIGAMSASA KIMOMBO CHANGU ILI NISIJE KUA.......(SOMA ZAIDI)

 Kiingereza ni lugha inayotupa tabu Watanzania wengi na hakuna anayebisha kuwa kimekuwa kikitukosesha fursa nyingi za kimataifa au kujikuta tukiumbuka.
Rich Mavoko ni mmoja wao na amesema atalazimika kufuata njia ya bosi wake, Diamond ili kujinoa zaidi kuepuka kuumbuka siku za usoni.

“Mwaka jana nilienda London, nikakutana na mtu anaongea Kiingereza pale pale lakini mbona kuna vitu sivielewi anavyoongea, alikuwa ni mhindi ambaye amezaliwa kule kule. Anaweza kuuliza maswali mengi ukaelewa matatu,”
“Kizuri ambacho mimi nakijua usilete mbwembwe jibu unachokielewa kwa time aliyokuuliza, kwahiyo kuna umuhimu sana kwasababu hatuwezi kufika bila kujua hicho kitu,” ameongeza.

Rich Mavoko ana elimu ya kidato cha nne na amedai kuwa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu za kiuchumi.

Diamond naye amewahi kusimulia jinsi alivyowahi kuumbuka miaka kadhaa iliyopita wakati Kiingereza chake kilikuwa cha kuchechemea hali iliyomfanya apate hasira ya kujifunza. Leo hii hitmaker huyo anakipiga kimombo kama kawaida!

NEWS:VANESSA MDEE ATAJWA KUWANIA TUZO ZA NIGERIA......(SOMA ZAIDI)

Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee jina lake limeingia kwenye headlines baada ya kutajwa katika moja kati ya tuzo kubwa Nigeria Entertainment, Vanessa ametajwa kuwania tuzo zinazoitwa Nigeria Entertainment Awards.

Jina la muimbaji Vanessa Mdee limetajwa katika kipengele cha kuwania tuzo ya muimbaji bora wa kike, katika kipengele hicho Vanessa anawania tuzo hiyo na wasanii wengine saba kutoka nchi mbalimbali, Nigeria Entertainment Awards zitafanyika New York Marekani, September 4 2016

NEWS:AFANDE SELE- NINA WANAWAKE SITA NA WOTE NIKO NAWAPIMA TU KWENYE MAM.....(SOMA ZAIDI)

Msanii wa muziki na mwanasiasa kutoka mji kasoro bahari, Afande Sele amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye hatarajii kuoa kwani bado yupo yupo sana ingawa anakiri wazi kuwa yupo na mahusiano na wanawake kama sita hivi ambao wanamsaidia kumtunzia

watoto wake huku akiangalia kati ya watu hao alionao yupi anastahili kuwa malkia.
Afande Sele alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya Eat Africa Radio na kusema kwa sasa yeye kusema atafunga ndoa itakuwa ni uongo mkubwa kwani watu alionao anaona bado wanapimana maana wao wanampima yeye na yeye anawapima wao na kuona yupi anastahili kuingia ndani kama mke.

"Niwe mkweli tu hilo wazo la kuvuta jiko sina, namshukuru Mungu nimepata watoto wawili naweza kwenda nao vizuri na kuwalea, kusema nifunge ndoa leo au kesho utakuwa uongo sababu ndoa si kusema mwanamke kuchukua nyanya tu gengeni,lazima nipate mwanamke amabaye atakuwa na vigezo vya kuwa na mimi atajua nini maisha ambayo mimi nayahitaji, atanielewa tabia zangu za nje na ndani hivyo sidhani kama ni rahisi kupata mke kwa kipindi hiki ila najivunia kuwa na marafiki ambao wanasaidia kulea watoto wangu, wanawapenda watoto zangu hicho nashukuru" alisema Afande Sele.

"Nipo kwenye kupima nawapima na wao wananipima mimi, mimi na marafiki wa hivyo wakati ukifika nikiona yupo anafaa kuwa na mimi nitakuwa naye lakini niwe mkweli, siko mwenyewe au kusema natumia sabuni hapana mimi na warembo kama kawaida, wananisaidia kukaa na watoto wangu, wanaheshima. Maana mimi ni kama mfalme hata mfalme Suleman alikuwa wa wake zaidi ya mia tatu kwenye nyumba yake, hata mimi wapo kadhaa ila hawazidi sita" aliongeza Afande Sele

NEWS:HOSPITAL YA MUHIMBILI DSM KUANZA KUTOA CHAKULA KWA WAGONJWA KUANZIA MWEZ........(SOMA ZAID)

Tamko kutoka wizara ya Afya imeamua kuanzisha mradi katika Hospitali taifa ya Muhimbili kwa kuanzisha mradi wa kuwasaidia wagonjwa na kuimarisha huduma zao.
Msemaji mkuu wa hospitalini hapo ameamua kufanya mradi huo kwaajili ya kusaidiana na wagonjwa ,ndugu na hasa wale wenye kipato cha chini.

"Kuanzia julai mosi,Tutaanza kutoa huduma hii kwa kuwapa wagonjwa chakula cha asubuhi mchana na usiku pasipo kuangalia ni mjonjwa na siku ngapi,hivyo tunaanza huduma hiyo kwa kuwapa chakula maalum"Alisema (Bw.Aminiel aligaesha)
Tumeshaandaa jamo hilo na halitokuwa kwa muda,Tunafanya hivyo ili kuwasaidia ndugu wa wagonjwa amabao wanapata shida ya kuja kuwaona ndugu zao kila siku na kupoteza kiasi fulani cha pesa,hivyo tutafanya hivyo kuwasaidia wale walioko mbali amabao wanajikuta wanatumia pesa nyingi kuja na wakati mwangine inafika hadi sh.10,000/= ikiwa kama nauli mbali na pesa utakazo tumia kwa kupiga chakuala cha mgonjwa.
Hivyo basi kuanzia july mosi huduma huyo itaanza.

NEWS; WEMA SEPETU, NATAMANI KUONANA NA DIAMOND TUONGEE TUYAMALIZE ILA KAMA.........(SOMA ZAIDI)

Mshindi wa Miss Vodacome mwaka 2015,mwanadada mrembo Wema sepetu amekuwa ni mtu maarufu kati ya warembo walioko nchini Tanzania licha ya kuandamwa na skendo za kila aina.

 

Wema isack amesikika akiongea na watu kuwa anatamani kuonana na diamondi wala japo kwa lisaa limoja tuliongee jambo amablo lipo katikati yetu linalo pelekea tunashindwa kupeana sapoot.

"Hakuna mtu aliekuwa hajui mahausiano yetu mimi na Naseeb lakini tulitengana na kila mtu akapata nafasi ya kufanya jambo lake licha ya timu zetu kuwa bado zina sinto fahamu.Ili watu tuishi vizuri na kwaamani kwa kupata manuufaa mkubwa ni lazima watu tupeane sapoot,Mimi nilikodisha ukumbi kwaajili ya show ya Christian Bella pale 'King solomon',Lakini alipokuja naseeb nayeye akautaka ukumbi huo tenda kwa tarehe ileile niliyokuwa nayo maana msimamizi wa pale alimwambia kuwa huu ameukodisha sepetu et'aaaaaah kumbe yule mi nalipia mara mbili zaidi'.Sasa hii ukiiangalia vizuri sio njema kwasababu tunashindwa kupeana sapoo" Alisema wema.

6/21/2016

NEWS; JE WEWE NI SHABIKI WA DIAMOND PLATNUMZ? SOMA HII KUJUA LINI ANAKUPA VIDEO HII.....(SOMA ZAIDI)

Hii imekuwa video iliyosambaa zaidi mitandaoni baad aya kutolewa kama tangazo kuwa msanii Diamond Playnumz anatoa kazi yake mpya aliyofanya na wasanii wa kimataifa kutoka Nigeria P Square.
Leo Diamond ameandika haya Katika Ukurasa wake wa Instagram:
"My People!!!!!!!!! Subscribe to my Youtube Channel now so that you can be the first one to watch the HIT from SIMBA ft P-SQUARE!!!! (Najua unakiu kias gani....haya Jiunge na Channel yangu ya YOUTUBE sasa ili uwe mtu wa kwanza kushuhudia Mshine yangu Mpya Nilowashirikisha P-SQUARE! ) Cc @peterpsquare @rudeboypsquare #SimbaKaseMa"
Hii ni miongoni mwa collabo zilizosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa bongo fleva,nyingini ni pamoja na collabo yake na Neyo na WizKid.

NEWS; NUH MZIWANDA APATA CHOMBO KIPYA AMSAHAU SHILOLE.......(SOMA HABARI ZAIDI)

Nuh Mziwanda Baada ya Kumpata mpenzi mpya amejikuta amerudia alilofanya kwa Shilole la Kujichora Tatoo Mkononi ya jina la mpenzi wake huyo mpya..

Nuh Amesema huyu wa sasa amekuja na gia kubwa sana kiasa anaamini anampenda kwa dhati, amempa sifa kuwa ni mwanamke anayependa marafiki zake sana tofauti alivyokuwa shilole...

NEWS:JWTZ LAKANUSHA KUIBIWA KWA KIFARU NA KUTOA TAMKO KWA V.......(SOMA ZAIDI)

Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)  limekanusha taarifa za kuibiwa kwa kifaru  cha jeshi zilizoripotiwa leo na gazeti la Dira  na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowowte huku  likisisitiza ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.

Akiongea na  waandishi wa habari leo  kukanusha habari hizo, msemaji wa jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema jeshi limesikitishwa sana na habari hizo za upotoshaji kwa kuwa zinachafua taswira ya jeshi na taifa kwa ujumla.

Amelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi mara moja na wakishindwa kufanya hivyo hatua Kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao

NEWS: BASI LA NBS KUTOKA DAR KWENDA TABORA LAPATA AJALI

 Basi la NBS linalotoka Dar es salaam  kwenda Tabora  limepata ajali mbaya maeneo ya Chakwale wilayani Gairo  mkoani Morogoro.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaarifu kuwa watu 5 wamefariki na 27  wamejeruhiwa katika ajali hiyo.

NEWS; WATU WATATU WAFARIKI KWA KULA MIOGO YENYE.........(SOMA ZAIDI)

Watu watatu wamefariki dunia baada ya kula mihogo inayodhaniwa kuwa na sumu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema jana kuwa tukio hilo juzi saa tisa mchana katika Kijiji cha Kauzeni, Manispaa ya Morogoro.

Amesema watu hao ni kati ya watano waliokula mihogo hiyo, lakini wawili walinusurika baada ya kuwahishwa Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mzinga kwa matibabu.

NEWS;CHADEMA YAZIDI KUBANWA MBAVU NA POLISI KWAKUWA HAW

Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro jana liliwatawanya wahitimu wa vyuo vikuu kupitia umoja wa Chadema (Chaso), waliokuwa wamekusanyika mjini Moshi kwa ajili ya mahafali yao.

Dalili za ‘kibano’ hicho zilianza kuonekana asubuhi wakati polisi na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa wamejihami kwa mabomu ya machozi, walipozingira hoteli ya Keys inayomilikiwa na Philemon Ndesamburo.

Hoteli hiyo iliyopo maeneo ya Kwa Alfonsi nje kidogo ya mji wa Moshi, ndipo ambako mahafali hayo ambayo yalikuwa yahusishe wahitimu 70 kutoka vyuo vikuu vinne yalikuwa yafanyike.

Wanafunzi hao ni kutoka Chuo Kikuu cha Mwenge (Mwekau), Chuo cha Kikuu cha Ushirika Moshi (Mocu), Chuo Kikuu cha Masoka na Chuo Kikuu cha Tiba KCMC (KCMU Co).

Hata hivyo, polisi wakiwa na magari yaliyokuwa yakipeperusha bendera nyekundu, walivamia hoteli hiyo na kuwataka wahitimu hao kutawanyika kwa amani, kwa vile mikusanyiko ya aina hiyo imezuiwa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) mkoani Kilimanjaro, Dickson Kibona alilaani tukio hilo akisema hakukuwa na sababu yoyote ya kuzuia mahafali hayo.

“Wamezuia bila sababu yoyote na hii inakiuka misingi ya kidemokrasia, Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa,” adai Kibona.

Kibona alidai kama isingekuwa kuhofia maslahi ya kibiashara ya Hoteli ya Keys ambapo kulikuwapo pia watalii, wangegoma kuondoka kwa kuwa hawakuvunja sheria yoyote ya nchi.

Mmiliki wa hoteli hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, alisema ndiye aliyewashauri vijana hao kutawanyika kwa amani na kuwataka wasibishane na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema polisi walipata taarifa kuwa wahitimu hao wangekuwa na mkutano wa kisiasa ambao ulijificha kwa mwavuli wa mahafali.

“Tumewaita viongozi wao na kuwaeleza kuwa mikutano yote ya kisiasa imezuiwa na watawanyike. Walituelewa na wakatawanyika, lakini sisi bado tunaendelea kuimarisha doria mitaani,” alisema.

Hili ni tukio la pili kwa wanachama wa Chaso kutawanywa na Polisi ambapo juzi katika hoteli ya African Dream mjini Dodoma, wahitimu wa vyuo vikuu mjini Dodoma nao walitawanywa na FFU.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema Chadema inaendelea kuhifadhi kumbukumbu za matukio yote yanayoendelea nchini, ili kujenga ushahidi utakaojitosheleza pindi itakapoonekana ni mwafaka kuchukua hatua zaidi.

Alifafanua kuwa chama hicho kinatambua hila zinazofanywa na Serikali kwa kulitumia Jeshi la Polisi, na kuwa wanatambua amri zinazotolewa na watendaji wa chama tawala kupitia wakuu wa mikoa na wilaya.

Alisema wanao ushahidi wa matukio yote utakaotumika muda wowote, watakapoamua kuishtaki Serikali ndani au nje ya nchi

NEWS;YANGA YASHIDWA KUTUSUA MBELE YA WAARABU HIVYO KWEN.........(SOMA ZAIDI)

Mabingwa wa soka la Tanzania bara Yanga SC wameanza vibaya kampeni zao za kuwania kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya MO Bejaia ukiwa ni chezo wa Kundi A.

Yassin Sahli alifunga bao pekee kwenye mchezo huo na kuipa pointi tatu MO Bejaia iliyokuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani Stade de I’Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria.


Matokeo hayo yanaiacha Yanga katika nafasi ya tatu huku TP Mazembe wakiwa ndiyo vinara wa Kundi baada ya kushinda mchezo wao kwa magoli 3-0 dhidi ya Medeama ambayo inaburuza mkia.

Mazembe na MO Bejaia zinapointi sawa (pointi tatu) lakini TP Mazembe anaongoza kundi kwa tofauti ya magoli wakati Yanga na Medeama zikiwa hazina pointi lakini Yanga inakaa nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli. Medeama imefungwa magoli matatu wakati Yanga wameruhusu bao moja pekee.


Mchezo ujao wa Yanga utakuwa nyumbani (Dar es Salaam) June 28 itakapowaalika TP Mazembe kwenye uwanja wa taifa.

NEWS;UKIFANYA BIASHARA HII LAZIMA UWE TAJIRI KAMA UTAAMUA KU......(SOMA ZAIDI)

MAKALA HII IMEANDIKWA NA MESHACK MAGANGA WA IRINGA TANZANIA.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza ujasiriamali. Ninaandika makala hii kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kuniletea mafanikio makubwa.

Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa kuuza vocha na  kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo yachuo. Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa Iringa mjini, baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya.

Na baadaye nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambaye pia anajishughulisha sana na kilimo cha miti. Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini Kalenga, nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba, leo nina ekari nyingi.

Albert sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu mimi:- “UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSss! UNAWEZA KUFA MASIKINI! Nina rafiki yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, "Sanga nimeamua kuanza kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu ishirini na tano, (25,000?/=).

Nikamwambia "Kupata ekari moja si chini ya laki sita na wewe una tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!", Sikumwelewa! Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo moja linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango. Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua Tsh. 7,000/=.

Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja. Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/= (laki nane). Alipokuja na fedha hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine akairudisha shambani.

Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia” Akaendelea kwa kusema:-

Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa.

Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala. Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama mbao.Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho. Miti ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake.

Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000).

Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni thelathini na mbili (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji (demand) wa mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi  laki moja na 20 elfu (120,000) na laki moja, kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja  na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea na umri wa miti unayotaka.

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne.

Uponunua mashamba haya kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo. Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako.

Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning).

Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima. Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.

Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu.

Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa.  Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya uzalishaji katika ardhi yetu.

Inawezekana! Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie.

Yupo Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira, ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.

6/18/2016

NEWS;KALALA APATA CHOMBO KIMYA AMBWAGA MUNA LOVE RASMI KUTOK..(SOMA ZAIDI)


Habari ‘hot’ iliyotua kwenye meza ya gazeti hili inadai kuwa lile penzi lililokuwa gumzo mjini kati ya Mwanamuziki Kalala Hamza ‘Junior’ na msanii wa filamu za Kibongo, Rose Alphonce ‘Muna Love’ limevunjika na sasa jamaa huyo amehamishia majeshi kwa mwigizaji aitwaye Mamy Mushi.

Inaelezwa kuwa, sasa hivi Kalala na Mamy wamekuwa ni kama kumbikumbi kwani wamekuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali za kujiachia.Akizungumzia kumwagana na Kalala, Muna alisema kwa kifupi: “Ni kweli nimeachana na Kalala. Sasa kila mmoja ana maisha yake.”


Kalala ambaye kwa sasa anapiga mzigo kwenye Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ hakupatikana kuzungumzia penzi lake jipya ila Mamy alipozungumza na Ijumaa alikiri kumrithi Muna: “Penzi letu wala siyo la kificho, Muna na Kalala ilikuwa zamani, sasa ni zamu yangu.”

NEWS; DIAMOND PLATNUMZ KUNA WATU WANAJUA ETI MIMI NINA BIFU NA.......(SOMAZAIDI)

Mkali wa muziki na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amesema 90% ya bifu ambazo zinazungumzwa na waandishi wa habari na kukuzwa sio bifu za kweli.
Simba

Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni, Diamond amesema kuna bifu nyingi zinakuzwa na waandishi wa habari lakini kiundani unakuta sio bifu kweli.

“Mimi nikiangalia karibu 90% ya wasanii wa Tanzania ambao watu wanadhani wanamatatizo, sio kweli wanamatatizo,” alisema. Diamond. “Kuna baadhi ya vyombo vya habari vinatumia hiyo nyenzo ili kutengeneza maslahi binafsi, mimi nakwambia ukweli kabisa, kwa sababu watu wengi ambao wanasema wanamatatizo hawana matatizo, wangekuwa wana matatizo tungesikia mtu akisema mimi nikikutana na flani nitamtia ngumi ya meno,”

Aliongeza, “Ukitaka kuamini kama ni uongo, juzi tukilisikia kuna bifu kati ya Shilole na Vanessa lakini kesho yake wakafanya show, hamna ugomvi,”

Pia muimbaji huyo amevitaka vyombo vya habari kuandika habari ambazo zina tija kwa wasanii na taifa kwa ujumla.

“So kama tulivyowaomba mwanzo, tunaviomba vyombo vyetu, na tunawaomba sana sana mtutengenezee umoja kwa wasanii ili tuweze kusaidia familia zetu. Watu wanapogombana tunatia vita katika sanaa, familia, watu kulogana, tuwapumzishe nao waganga wanachoka, tunapeleka hela za bure,” alisema Diamond.

NEWS; WABUNGE WAWILI WAPIGWA STOP KUKANYAGA KWENY........(SOMAZAIDI)

Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.

Mbune Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.

Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

NEWS;BARUA KWA MBOYE NA WABUNGE WOTE WA UKAWA KWAKU......(SOMA ZAID)

Kama ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania mbinu ya wapinzania kutoka njee ya bunge kwa sababu mbali mbali haikuanza leo. Na tangu wameaanza kuitumia mbinu hii haijawahi kuwasaidia au hata kueleweka kwa wananchi badala yake sisi wananchi ndio huwa tunapata hasara.

Kwa mara ya Kwanza wapinzani walitoka njee ya Bunge wakati raisi Kikwete alipoingia madarakani kwa mara ya pili kwa kile walichokidai kuwa ni kutomtambua. Walitoka njee wakati wa kuhutubia bunge na kulifungua bunge.

Je waliposusia bunge mwisho wa siku hawakuja kumtambua raisi Kikwete?? jibu ni NDIO wakikuja kumtambua na walivunja rekodi kupiga hodi ikulu kuomba busara za raisi kuliko vipindi vingine vyote.Tuliwashuhudia wakiburudika na juice mara nyingi tu Ikulu wakipata picha ya pamoja nk.

Mara ya pili tunawaona upinzani ukitoka njee kususia bunge la katiba. Mwisho wa siku bunge liliendelea na katiba pendekezwa ikapitishwa bila kuwa na mawazo mbadala ya wapinzani ndani ya katiba ile inayosubiria kupigiwa kura.

Mara ya tatu upinzani unatoka njee kupinga matokeo ya uraisi yaliyompa raisi Magufuli ushindi. Wanatoka siku ya raisi kulifungua bunge kama walivyotoka kipindi cha Kikwete. Raisi analifungua bunge na baada ya hapo bunge lilelile lililopewa uhalali na rais Magufuli baada ya kulifungua wapinzani wanarudi na kulitumia. Na hata sasa wapinzani wameshamtambua raisi Magufuli kuwa ni raisi halali na aliyechaguliwa kihalali.

Mara ya nne ni hili la kumkimbia Dr Tulia. Katika hali ya kawaida nilifikiri wangelifanya hivi kwa siku moja tu. Mpango wa kususia kila siku kumetuathiri sana sisi wananchi kuliko kulivyomuathiri Dr Tulia. Tena wapinzani wanatoka njee kipindi muhimu kabisa ambacho walipaswa kuombea majimbo yao miradi ya kimaendeleo toka kwenye bajeti ambayo itapitishwa muda mfupi ujao.

Upinzani umetoka kwenye mstari wa kujenga hoja hadi kususia kususia mambo ya ajabu ajabu.Nakiri kabisa kuwa kilichoijenga kambi ya upinzani nchini ni hoja zao nzito miaka ya 2005-2015.

Sote tunakumbuka jinsi upinzani ulivyopata umaarufu kwa kujenga hoja za kukataa ufisadi, kudai katiba mpya, swala la Buzwagi, na hata juzi juzi swala la ESCROW. Kafulila pamoja na kutukanwa tumbili alisisimama kidete hadi akafanikiwa kuwangoa kina Warema bungeni na wengineo. Nataka nikuonyeshe nguvu ya hoja ilivyo na mantiki kuliko hii zomea zomea na kutoka nje ya bunge.

Katika nchi zote za jumuiya ya Madola Tanzania upinzani ndio unaongoza kwa kuthaminiwa kuliko nchi zote. Thamani hii upinzani umeshindwa kuutambua na kuutumia kujijenga badala yake wamekimbia na kinachowakimbiza ni kanuni walizojiwekea wenyewe.

Ni Tanzania tu katika ukanda huu Kambi rasmi ya upinzani inatambulika bungeni, kuwa na baraza la mawaziri kivuli, na baadhi ya kamati nyeti zinazogusa maslahi ya Taifa kuwekewa kanuni lazma ziongozwe na upinzani kama PAC nk.

Hii ni fursa ambayo upinzani walipaswa kuitumia kujitangaza kuliko kuzurura njee ya viwanja vya bunge. Inauma sana kuona wanakosea na hawataki kujirekebisha.

Naamini si wabunge wote wa upinzani wanataka kutoka njee ya Bunge lah hasha. Prof Elton Mayo aliwahi kutoa nadharia ya Hawthorne Effect, nadharia ya kisaikolojia ambapo mtu hufanya jambo kwa kuwa tu kuna mtu anayemsimamia kufanya hivyo au anafanya tu kwa kuwa anajua anaonekana anachokifanya. Hivyo unafanya jambo si kwa kuwa unapenda kulifanya ila unafanya kwa kuwa kuna sababu zinakufanya ufanye.Nikiangalia huu utoto anaoufanya Mbatia pamoja na uelewa wake wote naona madhara ya mob psychology.

MBOWE nakuomba usitumie tena mbinu hii haiwajengi inawabomoa.

Ole Mushi.

MwanaCCM mwenye kujali maslah mapana ya nchi.

NEWS:BELL 9 NAMKUBALI SANA MR BLUE NDIO MANA NIMEMUWEKA KWENYE.......(SOMA ZAIDI)

Msanii Belle nine amesema amkubali sana rapper Mr. Blue, kwani ni msanii ambaye amaeonyesha njia kwa vijana wengi kwa kitendo chake zha kuanza muziki akiwa mdogo.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Belle 9 amesema Mr. Blue ni rapper mzuri si kwa kuanza muziki akiwa mdogo, bali pia alishawahi kufanya naye kazi na kufanya vizuri.

“Mr. Blue ni rapper ninayemkubali alianza muziki akiwa na umri mdogo na kutuhamasisha wengi, hata nilipofanya naye kazi ya we ni wangu alifanya poa ni ikawa kazi nzuri”, alisema Belle 9.

Belle 9 ambaye ameachia remix ya wimbo wa 'burger, movie, selfie' amesema kuamua kushirikisha wasanii watano kwenye wimbo huo, ni idea aliyoipata baada ya watu wengi kumpigia simu kutaka remix au refix, na kaumua kuifanyia kazi mwenyewe kwa kuchanganya ladha tofauti tofauti.

“Unajua baada ya kuitoa burger, movie selfie, watu wengi walinipigia wanataka kufanya remix, cover, refix, nikaona niifanyie remx, na kuamua kuwashirikisha wasanii tofauti tofauti”, alisema Belle 9.

NEWS:RAIS MAGURULI CCM YAIVA KAMATI KUU YA CHA......(SOMA ZAIDI)

Maandalizi ya CCM kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti wa chama hicho ili ashike kofia zote mbili, yataanza kesho katika kikao cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

Taarifa kuhusu kikao hicho iliyotiwa saini na msemaji wa chama hicho, Christopher ole Sendeka ilisema: “Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM itafanya  kikao cha kawaida siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kitafanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete.”

Japokuwa taarifa hiyo haikueleza ajenda za kikao, habari kutoka ndani ya chama zinasema kikao hicho cha siku moja kinatarajiwa kujadili masuala mbalimbali, ukiwamo mchakato wa makabidhiano ya kiti hicho katika mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika mwezi ujao.

Kipindi cha uongozi wa chama kwa Kikwete kitamalizika mwakani, lakini imekuwapo desturi kwa rais mpya kuachiwa kofia hiyo mapema, hivyo Rais Magufuli anatarajiwa kurithi mikoba ya uenyekiti mwezi ujao.

Vilevile, kikao hicho kinatarajiwa kuhitimisha hoja zinazodaiwa kuibuka katika vikao vya ndani vya chama hicho kwamba CCM inataka kuvuruga utaratibu uliodumu kwa muda mrefu wa mwenyekiti kumwachia kijiti Rais aliyeko madarakani.

Madai kuhusu mkakati huo wa ndani yalisambazwa katika mitandao ya kijamii yakimnukuu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, lakini Ole Sendeka alisema hana sababu yoyote ya kumjibu kiongozi wa dini.

Februari 5, mwaka huu Kikwete alipokuwa anazungumza na wazee wa Manispaa ya Singida alisema sherehe za mwaka huu za maadhimisho ya miaka 39 tangu chama hicho kuanzishwa zilikuwa za mwisho kwake akiwa mwenyekiti, kauli ambayo iliashiria ataachia mapema uenyekiti.

Kwa desturi, wenyeviti wa CCM huwa wanaachia madaraka yao kabla ya muda wa uongozi wao kumalizika.

Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alikabidhiwa chama na Alhaji Ali Hassan Mwinyi mwaka 1996 badala ya 1997 na Mkapa alimkabidhi Kikwete kiti hicho mwaka 2006 badala ya 2007.

Kulingana na kalenda ya chama hicho, Mkutano Mkuu wa CCM kumchagua mwenyekiti unapaswa kufanyika mwaka 2017, lakini utafanyika mwaka huu kuendeleza utamaduni wa kung’atuka mapema.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa kinachoendelea sasa mikoani na wilayani ni maandalizi ya mkutano huo mkuu yanayosimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Bara, Rajabu Luhwavi kwa niaba ya Sekretarieti.

“Kikao hicho cha Kamati Kuu ndicho kitakachojadili ajenda za mkutano huo sambamba na kupanga tarehe ya kufanyika kwa mkutano mkuu,” zilieleza taarifa hizo.

Dk Magufuli anatajwa kuwa uongozi wake ndani ya CCM utakuwa wa kasi ya aina yake kutokana na hatua mbalimbali za ‘utumbuaji majipu’ anazozifanya ndani ya Serikali tangu Novemba 5, alipoapishwa kuwa Rais.

NEWS: MH MAJALIWA ASUSIWA FUTARI NA KAMBI PINZANI KWENYE MUE.......(SOMA ZAIDI)

Wabunge wa vyama vinavyounda Ukawa jana walisusia futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ikiwa ni mwendelezo wa hatua za kususia shughuli zote zinazoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Riziki Ng’wale, alisema wamechukua hatua hiyo kutokana na Dk Tulia kuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo.

“Dk Tulia ndiye mgeni rasmi katika shughuli hiyo ya kufuturisha na sisi tumeamua kuwa hatutashiriki shughuli yoyote inayoongozwa naye,” alisema muda mfupi baada ya kutoka katika kikao cha wabunge wa kambi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alisema wamekubaliana wabunge wote wa kambi ya upinzani waliofunga watakwenda kufuturu majumbani kwao.

“Tumekubaliana hatutakwenda kufuturu bungeni na kila mbunge atakwenda kufuturu nyumbani kwake,” alisema.

Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha wapinzani kilichoketi chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia.

Futari hiyo ilitangazwa na Dk Tulia tangu juzi na kusisitizwa jana baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa mchana kuwa ingefanyika kwenye viwanja vya Bunge ambako wabunge wote walialikwa.

Kwa siku zaidi ya 10 sasa, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk Tulia kwa sababu hawana  imani naye.

Hali hiyo imefanya bajeti kuu kwa ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuchangiwa na wabunge wa CCM tu baada ya Dk Tulia kuongoza vikao kila siku, akiingia asubuhi na jioni

NEWS: DEWJI AJIPANGA KUISAIDIA TANZANIA KWA KUTOA AJIRA KWA VIJANA WENY.......(SOMA ZAIDI)

Miongoni mwa mambo yanayoifanya Tanzania kuwa masikini ni watu wengi kutokuwa na kipato cha uhakika na cha kutosheleza mahitaji muhimu kwa maisha.

Takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha kuwa utafiti uliofanyika mwaka 2014 umebaini nguvu kazi ya Taifa ni watu milioni 22.3 kati ya idadi ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni 45.

Kati ya nguvu kazi hiyo ya watu milioni 22.3, wenye ajira ni 20 milioni na wasio na shughuli yoyote ya kuingiza kipato ni milioni 2.2.

NBS inasema kuwa kwa kadri uchumi wa Tanzania unavyokua ndivyo na idadi ya watu wasio na ajira inavyopungua.

Takwimu nyingine zinaonyesha kuwa kila mwaka vijana 850,000 wanamaliza masomo na kuingia katika soko la ajira na miongoni mwao asilimia tano ndio wanaofanikiwa kupata ajira kwenye sekta rasmi. Wengi wao hubakia wakizurura mijini kutafuta ajira miaka kadhaa na miongoni mwao pia hujiunga katika sekta isiyo rasmi, wakijihusisha na shughuli za ujasiriamali.


Rais John Magufuli amekuwa akihimiza shughuli za kiuchumi ili kuisukuma Tanzania katika uchumi wa kati, ambao Watanzania wengi watakuwa na ajira na vipato vizuri.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni kuhimiza uwekezaji, kufufua viwanda na kuhamasisha ukuaji wa viwanda vya ndani kwa kudhibiti uingiaji wa bidhaa kutoka nje.

Rais Magufuli anaona wazi kuwa sekta ya uzalishaji nchini inasuasua. Lengo lake ni kuona sekta ya uzalishaji viwandani inachangia zaidi ya asilimia 15 ya pato la Taifa na kuongeza asilimia 40 ya ajira nchini. Katika mkutano na wafanyabiashara wakubwa nchini, Dk Magufuli aliwahakikishia kuwa Serikali yake itakuwa bega kwa bega nao katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakua.

Katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanafaidika na kukua kwa uchumi, amekuwa akiisafisha Serikali yake juu ya vitendo vya rushwa, ufisadi na uzembe katika uwajibikaji.

Wakati wafanyabiashara wakihimizwa kushirikiana bega kwa bega na mikakati ya Serikali ya kuinua uchumi na kupambana na umaskini, Mfanyabiashara Mtanzania, bilionea mdogo Zaidi Afrika, Mohammed Dewji ameahidi neema kwa Watanzania.

Mtandao wa Forbes; unaoandika taarifa za watu bilionea duniani, unamnukuu Dewji akisema kuwa anatarajia kuzalisha ajira 100,000 kabla ya kufikia 2020.

Katika mpango huo wa ajira, anasema nafasi nyingi zitachukuliwa na Watanzania. Mpaka sasa Dewji kupitia kampuni zake ameajiri Watanzania 28,000.

Mfanyabiashara huyo ambaye amefanikiwa kutunukiwa zawadi mbalimbali kutokana na umahiri wake kibiashara, akifanikisha mpango huo atatoa ajira 100,000.