Gazeti la JamboLEO limeripoti kuwa Serikali inakusudia kufanya utafiti
kwa kupima virusi vya UKIMWI (VVU) nyumba kwa nyumba kuanzia ngazi ya
kaya, ili kupata takwimu sahihi kuhusu hali ya maambukizi mapya ya
ugojwa huo ulivyo sasa nchini.
Aidha gazeti hilo limeongeza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa ambapo alisema utafiti huo utakaotumia
teknolojia ya kisasa, unalenga kupima viashiria na matokeo ya UKIMWI
nchini, ili kujua ni kiwango gani Tanzania imepiga hatua katika kupamban
na ugonjwa huo.
Gazeti hilo limemnukuu Dk Albina Chuwa akisema
”utafiti huo utafanyika kwa kutumia sampuli wakilishi ya kaya takribani
15, 800 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa kufikia walengwa 40, 000
wakiwamo watoto wasiopungua 8, 000′

No comments:
Post a Comment