Msanii
wa muziki wa Hip Hop, Chidi Benz amefunguka na kueleza jinsi wadau wa
muziki nchini wanavyosababisha wasanii wa muziki kuingia kwenye matumizi
ya Madawa ya kulevya.
Rapper huyo ambaye ameachana na matumizi ya Madawa ya kulevya hivi
karibuni, ameiambia BBC kuwa wasanii wengi wanaingia kwenye Madawa ya
kulevya baada ya kupata stress za kubaniwa kwenye muziki.
“Watu wanamsongo wa mawazo, mashabiki wetu hawajui sisi jinsi
tunavyodeal na watu ambao wanatufikisha kwao, wadau wa muziki, wadau wa
muziki ni watu tofauti sana na wanafanya vitu vibaya sana,” alisema
Chidi. “Wachache wapo wanaosaidia vizuri, lakini ni wengi wanaoharibu na
wanaharibu sana sana, yaani mtu anakuwa na kisasi na wewe na yupo
tayari kukufanyia kitu chochote, akushushe, akupinguze mpaka umalize
pesa zote na usipingwe hata wimbo wako mmoja,”
Pia rapper huyo alisema wasanii wengi wanabaniwa kutokana na migongano
ya kimaslahi katika kazi au kushare mademu na wadau wa muziki.
“Huu muziki tunaoufanya na haya maneno tunayoyaimba, kuna wale ambao
wanachukulia starehe na kuna wengine wanachukulia unawasema au mabinti
zao wanatupenda sisi wasanii. Unakuta kuna binti amekupenda wewe msanii,
kumbe yule ana mtu mwingine au mdau, sasa huyo mtu akisikia kwamba
Chidi Benz anadeal na mtu wake, hawezi kuelewa kwamba mtu wake ndio
anamfuata Chidi Benz, ila yeye atakufanya kitu chochote kile ili
akuumize au akuharibu na ‘akustopishe’ maendeleo yako. Na inawezekana
yule mtu wewe haukudeal naye ila anakupenda tu kishabiki na anawaambia
marafiki zake hivyo lakini marafiki zake inatokea wakaibadilisha na
wakaiweka kimapenzi, tayari una vita na mtu wake ambaye anamwangalia,”
alisema Chidi.
Pia rapper huyo amedai kilichomwingiza yeye kwenye matumizi ya Madawa ya
kulevya ni kutochezwa kwa ngoma zake kwenye redio na runinga hali
ambayo ilimfanya ajione mpweke

No comments:
Post a Comment