Kiingereza ni lugha inayotupa tabu Watanzania wengi na hakuna anayebisha
kuwa kimekuwa kikitukosesha fursa nyingi za kimataifa au kujikuta
tukiumbuka.
Rich Mavoko ni mmoja wao na amesema atalazimika kufuata njia ya bosi
wake, Diamond ili kujinoa zaidi kuepuka kuumbuka siku za usoni.
“Mwaka jana nilienda London, nikakutana na mtu anaongea Kiingereza pale
pale lakini mbona kuna vitu sivielewi anavyoongea, alikuwa ni mhindi
ambaye amezaliwa kule kule. Anaweza kuuliza maswali mengi ukaelewa
matatu,”
“Kizuri ambacho mimi nakijua usilete mbwembwe jibu unachokielewa kwa
time aliyokuuliza, kwahiyo kuna umuhimu sana kwasababu hatuwezi kufika
bila kujua hicho kitu,” ameongeza.
Rich Mavoko ana elimu ya kidato cha nne na amedai kuwa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu za kiuchumi.
Diamond naye amewahi kusimulia jinsi alivyowahi kuumbuka miaka kadhaa
iliyopita wakati Kiingereza chake kilikuwa cha kuchechemea hali
iliyomfanya apate hasira ya kujifunza. Leo hii hitmaker huyo anakipiga
kimombo kama kawaida!


No comments:
Post a Comment