Msanii wa muziki na mwanasiasa kutoka mji kasoro bahari, Afande Sele
amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye hatarajii kuoa kwani bado yupo
yupo sana ingawa anakiri wazi kuwa yupo na mahusiano na wanawake kama
sita hivi ambao wanamsaidia kumtunzia
watoto wake huku akiangalia kati ya watu hao alionao yupi anastahili kuwa malkia.
Afande Sele alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya Eat Africa
Radio na kusema kwa sasa yeye kusema atafunga ndoa itakuwa ni uongo
mkubwa kwani watu alionao anaona bado wanapimana maana wao wanampima
yeye na yeye anawapima wao na kuona yupi anastahili kuingia ndani kama
mke.
"Niwe mkweli tu hilo wazo la kuvuta jiko sina, namshukuru Mungu nimepata
watoto wawili naweza kwenda nao vizuri na kuwalea, kusema nifunge ndoa
leo au kesho utakuwa uongo sababu ndoa si kusema mwanamke kuchukua
nyanya tu gengeni,lazima nipate mwanamke amabaye atakuwa na vigezo vya
kuwa na mimi atajua nini maisha ambayo mimi nayahitaji, atanielewa tabia
zangu za nje na ndani hivyo sidhani kama ni rahisi kupata mke kwa
kipindi hiki ila najivunia kuwa na marafiki ambao wanasaidia kulea
watoto wangu, wanawapenda watoto zangu hicho nashukuru" alisema Afande
Sele.
"Nipo kwenye kupima nawapima na wao wananipima mimi, mimi na marafiki wa
hivyo wakati ukifika nikiona yupo anafaa kuwa na mimi nitakuwa naye
lakini niwe mkweli, siko mwenyewe au kusema natumia sabuni hapana mimi
na warembo kama kawaida, wananisaidia kukaa na watoto wangu,
wanaheshima. Maana mimi ni kama mfalme hata mfalme Suleman alikuwa wa
wake zaidi ya mia tatu kwenye nyumba yake, hata mimi wapo kadhaa ila
hawazidi sita" aliongeza Afande Sele

No comments:
Post a Comment