Mwanaume
1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na
utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo
mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza
kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya
mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama
viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa
muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda
mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia
vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na
kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster".
Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani
mwako.
Sababu za kukosa nguvu za kiume
Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una
maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa
kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema,utakuwa bora kama
chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima
yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya
uzazi kwa mwanaume.Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni
ya TestosteroneKupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za
kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda
mahusiano na ndoa.
1. Blueberry

Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi
hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini.
Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia
mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za
kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia
kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye
mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze
kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
2. Mtini (Figs)

Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni
kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi
cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa
hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.
3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)

Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika
katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za
kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu
ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi
hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume,
udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.
4. Karanga

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na
kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa
damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
5. Vitunguu saumu

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa
damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume
ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
6. Ndizi

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo
kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na
nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo
cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi
(libido).
7. Chocolate

Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu
ina viambato vyaphenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni
kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi
na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako
yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona
kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa.
Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa
kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama
ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.
Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko,
lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo
hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri
uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa
kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.
Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku
kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya
ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na
kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri
wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi,
kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa
makini.
Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni
vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa
mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni
hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua
tatizo la nguvu za kiume.

No comments:
Post a Comment