Header Ads

NEWS:RAISI SHEIN ATEUWA WAKUU WA MIKOA ZANZIBAR ......(SOMA ZAIDI)

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar imesema walioteuliwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini na Magharibi ambaye anakuwa Ayoub Mohamed Mahmoud na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja Vuai Mwinyi Mohamed.
Taarifa hiyo imesema  Wakuu wa Mikoa ambao Mikoa yao haikutajwa katika taarifa hii  wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.
Halikadhalika Rais Shein amemteua Marina Joel Thomas kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Silima Haji Haji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A anakuwa Hassan Ali Kombo, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B anakuwa Issa Juma Ali, Mkuu wa Wilaya ya Kati  Mashavu Sukwa Said, Mkuu wa Wilaya ya Kusini Idrissa Kitwana Mustafa na Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Salama Mbarouk Khatib.
Aidha Wakuu wa Wilaya ambao Wilaya zao hazikutajwa katika taarifa hii  wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.
Uteuzi wa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya umeanza leo.
Viongozi wote walioteuliwa wanatakiwa waripoti Ikulu, Mjini Unguja, siku ya Jumanne tarehe 24 Mei 2016 mchana tayari kwa kuapishwa.
 

No comments

Powered by Blogger.