Pages

7/30/2016

SIMBA YAKARIBIA KUMKABIDHI TIMU MO DEWJI

Mfanyabiashara Mohamed Dewji aongea na wanahabari. Aiomba Klabu ya Simba imuuzie asilimia 51 ya hisa kwa bilioni 20 ili alete mafanikio. “Kama unataka mafanikio kwenye mpira, hakuna zaidi ya fedha. Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata uwanja wa mazoezi. Alisema Dewji

Amesema bajeti ya Yanga na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji.

WASTARA, NUSURU MIMBA INITOE ROHO

Siku chache zilizopita, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma alikiri na kufunguka kuwa ni mama kijacho baada ya kunasa ujauzito lakini taarifa za kusikitisha zilizolifikia gazeti hili mapema wiki hii zimedai kwamba, mimba hiyo imechoropoka katika mazingira ambayo yalitaka kuutoa uhai wake.

Chanzo makini ambacho ni ndugu wa mwigizaji huyo kilichoomba hifadhi ya jina kilidai kuwa, kweli Wastara alikuwa na mimba lakini haikuwa riziki kwani imechoropoka katika mazingira ya ajabu.

“Baada ya kuzinguana na Sadifa (Khamis Juma) Wastara aliamua kuchukua hamsini zake. Baadaye aligundua amenasa na tulipomuuliza alisema si ya mtu mwingine zaidi ya mumewe Sadifa.

“Sasa, hivi karibuni alikwenda Msumbiji kufanya biashara zake za madini. Akiwa kule, akajiwa na hali f’lani mbaya ambayo ilimuweka kwenye wakati mgumu sana.

“Alichodai ni kwamba mimba imemsumbua sana na nusura imuue, tukamuuliza ameamua kuitoa au imetoka yenyewe? Hakutujibu chochote,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:

“Siku chache baadaye alinitumia SMS na kuniambia anamshukuru Mungu anaendelea vizuri. Hata alipotua Bongo, sikumsikia tena akizungumzia habari ya mimba na hata kwa kumuangalia tu ilionesha kwamba imechoropoka.

IJUMAA LAMSAKA WASTARA

Baada ya kunasa ubuyu huo, Jumatatu iliyopita, Ijumaa lilifanya jitihada za kumsaka Wastara kupitia simu yake ya kiganjani lakini mara kadhaa ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Siku iliyofuatia paparazi wetu alimpigia tena. Pia haikupokelewa na baadaye msanii huyo akatuma SMS aliyoandika ‘tuma meseji’.

Ijumaa: Mimi ni Mwandishi wa Ijumaa, naitwa (mwandishi anajitambulisha), kuna habari kuwa mimba yako ambayo ilikuwa inadaiwa ni ya aliyekuwa mumeo imetoka, kuna ukweli wowote?

Wastara: Nani kawaletea hizo habari?

Ijumaa: Ni vyazo vyetu, tukaona ni busara kukuuliza wewe ili kupata ukweli.

Wastara: Jamani niseme tu kwamba napitia kipindi kigumu sana kwa hiyo naomba uniache.

Ijumaa: Kipindi gani kigumu? Au ndiyo kutokana na mimba hiyo kuchoropoka?

Wastara: Hujui niko kwenye hali gani, kwa hiyo niache, muda wa kulizungumzia hilo ukifika nitasema.

Chanzo:GPL

JUX NA VANESSA MDEE WAZIDI KULA BATA WAISHI KIZUNGU- WASUBIRI KUTANGAZA NDOA

Wanamuziki, Vanessa Mdee na mpenzi wake Juma Jux ‘Jux’ baada ya manenomaneno kuzagaa kuwa wameachana juzikati wapenzi hao walionekana kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara kisha kwenda kula bata kwenye hoteli ya bei mbaya ya Singita.

Akipiga stori na safu hii juzi akiwa Serengeti, Vanessa alisema kuwa, wameamua kwenda huko kwa mapumziko ya siku nne ikiwa ni sehemu ya kufanya utalii wa ndani na wamekula bata za kutosha.

“Ni mambo ya utalii wa ndani, tumekuja huku kupumzika kidogo, siyo lazima kwenda nchi za nje kwa mapumziko, humuhumu Bongo kuna sehemu unakwenda na unajisikia furaha,” alisema mwanadada huyo.

Singita ni hoteli ya kifahari iliyopo mkoani Mara ambayo inaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.

WAALIMU WAMVUA NGUO NA KUPIGA VIBOKO NA MWINGINE KUMPAPASA SEHEMU NYETI MBEYA

VITENDO vya ukatili wa kijinsia na dhuluma dhidi ya watoto wa kike vimekuwa vikishamiri kila siku pamoja na kuwepo kwa taasisi za kutetea haki za wanawake  na kuanzishwa kwa madawati ya Kijinsia kwenye vituo vya polisi nchini.

Msichana wa kidato cha Nne mwenye umri wa miaka 17,(jina tunalo) anayesoma shule moja ya sekondari ya Kata mkoani Mbeya amekumbwa na kadhia ya kuvuliwa nguo zake za ndani na kucharazwa bakora zisizo na idadi na walimu wanne wa shule hiyo.

Tukio hilo ambalo limeripotiwa katika kituo kidogo cha  Polisi Mbalizi wilaya ya Mbeya kwenye jalada la uchunguzi namba MBI/IR/967/2016 na kuwekwa kwenye taarifa yenye namba MBI/RB/2653/2016 linadaiwa kuwahusisha walimu wanne akiwemo Mkuu wa shule hiyo pamoja na walimu watatu.

Akizungumza huku akiwa na maumivu makali katika Hospitali Teule ya Ifisi ambako amelazwa akipatiwa matibabu, mwanafunzi huyo alisema kuwa aliitwa na mwalimu wa nidhamu aliyemtaja kwa jina la Neema Mwaikenda aliyekuwa pamoja na Mkuu wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Mariamu Mwanisenga na mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili.

Alisema walimu hao walianza kumuadhibu kwa viboko visivyo na idadi huku akiwa amechojolewa nguo zake ambapo mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili akaanza kumshikashika sehemu zake za siri.

‘’Wakati naadhibiwa na walimu wote, huyu mwalimu wa kiume alianza kunishika  huku chini,na kunitaka niwataje wanaume zangu,nikawa nabana miguu wakazidi kunishambulia kwa vibao na mateke na fimbo,’’alisema mwanafunzi huyo.

Alisema sababu zilizosababisha aadhibiwe ilikuwa ni utoro na kuwa siku moja alipokuwa shuleni alioneshwa na walimu fimbo na kuelezwa kuwa fimbo hizo zitamuishia mwilini ndipo akaogopa kufika shuleni kwa siku tatu.

Anafafanua kuwa siku aliyofika shuleni ndipo alipokutana na kadhia ya kupigwa na walimu wanne hadi  alipowaponyoka walimu hao na kukimbilia mitaani na kujificha.

‘’Niliwaponyoka walimu nikakimbilia kwenye nyumba ya jirani na shule nikajificha hadi jioni na baadaye kwenda nyumbani, kesho yake mama na dada walinichukua na kunileta hospitali,’’alisema.

Mwandishi wa habari hizi alifika shuleni anakosoma mwanafunzi huyo kwa nia ya kukutana na uongozi wa shuleni hiyo ambapo Makamu Mkuu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwansanga alikataa kuelezea chochote.

‘’Mie sijui lolote kwanza mie sio msemaji wa shule, kwahiyo sijui lolote juu ya taarifa mnazohitaji,’’alijibu Makamu Mkuu wa shule na kuondoka zake.

Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Mkoa Charles Mwakalila alisema kuwa adhabu aliyopewa mwanafunzi huyo ni kubwa kupitiliza kwa kuwa zipo taratibu za adhabu kulingana na makosa na kuwa mwanafunzi anapaswa kupigwa viboko vitatu na viboko visivyozidi sita au adhabu mbadala.

‘’Adhabu aliyopewa ni kubwa, tutafuatilia na waliokiuka taratibu watachukuliwa hatua za kinidhamu,’’alisema Mwakalila.

Naye Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari alipoulizwa juu ya tukio hili alidai kuwa halijafika ofisini kwake na kuwa kwa sasa yeye yupo kikazi wilayani Chunya na mara atakapofika ofisini atafuatilia na kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika wa tukio hilo.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mariamu Mtunguja ambaye alifika Hospitalini alikolazwa mwanafunzi huyo alisema kuwa amemuangalia mwanafunzi huyo na kuona namna ambavyo damu imevilia kwenye sehemu zake za makalio na kwenye mapaja.

Mtunguja alisema kuwa kitendo kilichofanywa na walimu hao ni cha kinyama ambacho hakipaswi kuvumiliwa na kuwa mara itakapobainika atahakikisha walimu hao wanachukuliwa hatua za kinidhamu.

Muuguzi Mkuu Msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimati Sanga alisema kuwa mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo Julai 21 saa 7:00 mchana ambapo alipatiwa matibabu na kulazwa kutokana na majeraha na damu iliyovilia mwilini sehemu za makalio na mapaja.

‘’Ameshambuliwa sehemu za mapaja, damu na masikio yake hasikii vyema kutokana na kipigo, anaendelea na matitabu hapa hospitali,’’alisema Sanga.

NINAFURAHA SANA TANGU NILIPOTOKA CCM

Lowassa kupitia ukurasa wake wa Facebook ameelezea furaha yake namna ambavyo ameimarika zaidi baada ya kujitoa ndani ya CCM hadi sasa ambapo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

''Nina furaha kutimiza mwaka mmoja toka nilipojitoa CCM na kujiunga na CHADEMA.Uamuzi ule haukuwa rahisi,lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu nilifanya hivyo. Nilifanya uamuzi wa kihistoria katika nchi yetu'' Amesema Lowassa.

Ameongeza kuwa watanzania bado wanataka mabadiliko na hali hiyo imezidi kuthibitika kuwa wananchi hawawezi kuyapata ndani ya CCM .

Amesema watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo na kwamba vyote hivyo watavipata ndani ya CHADEMA na UKAWA kwa jumla.

Aidha amewataka watanzania wanaomuunga mkono na ambao walihama CCM kwa ajili yake waendelee kumuunga mkono na kuiunga mkono CHADEMA

KIJANA MWINGINE AMTUKANA MAGUFULI KWENYE NOAH MWANZA

Mgomo wa daladala Jijini Mwanza umesababisha kijana mmoja Jijini humo kutamka lugha chafu ndani ya gari ambayo alipewa lifti limemsababishia kuishia mikononi kwa sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast dereva wa wa gari likitoa lifti Hassan Bushagama mkazi wa Buhongwa Jijini Mwanza asema alipofika eneo la Buhongwa akiwa na usafiri wake aina ya Toyota Noah kutokana mgomo wa daladala aliamua kutoa lifti kwa abiria aliowakuta hapo.

"Walipanda watu kama nane ambapo Dada mmoja akasema watu walivyo hawatakawia kusema Rais Magufuli ndiye anatakiwa aulizwe,kijana mmoja wa umri wa miaka kama 27 au 28 hivi akadakia akasema Rais ni '******** 'mzee mmoja akamwambia kijana tengua kauli lakini akakataa na kusisitiza ,abiria wakataka kumpiga nikawaambia mwacheni tumpeleke 'polisi " Amesema Bwana Bushagama.

Bushagama ameendelea kusema kwamba "Baada ya hapo niliendesha gari langu hadi kituo cha polisi tulipofika pale nikawaambia polisi hali halisi askari akawahoji abiria wakaelezea hali hiyo na yeye alipoulizwa akasema ,amesema hivyo lakini hakujua kama ingepelekea kufika huko.

Aidha Bushagama ameongeza kuwa wameamua kusitisha kazi zao na kuonesha uzalendo ili kuonesha kwamba Rais hawezi kutukanwa namna hiyo.

Kwa upande wake Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwama kijana huyo amejitetea na kusema kwamba alisema alimaanisha wanaogoma wanajifanya wapumbavu lakini Rais ni ******** zaidi yao jambo liliwakasirisha wenzake na kuamua kumfikisha kituo cha Polisi.

Kamanda ameongeza kuwa suala hilo tayari limefikishwa Polisi kitachoendelea ni ushahidi ukitosheleza kijana huyo atapelekwa mahakamani.

HIKI NDO KINACHOWAFANYA WANAWAKE WANAKUWA BUSY NA SIMU MUDA WOTE

Msichana akitaka PERUVIAN HAIR mpya wala
hahangaiki sana...Anaingia kwenye PHONEBOOK yake
anachagua Madanga yake 20 anayoyaamini kwamba
hayawezi kumuangusha...AnaCOMPOSE Meseji
Tamuuu ambayo kila danga likipokea linahisi hiyo ni
Meseji yake peke yake. "Babe Mambo,Nimekumiss leo hadi nimekuota yaani
nimeamka So Wet I really miss my Pompolimpo,pole
na kazi mme wangu I wish I was there nikumassage
na Ulimi hadi usinzie..Leo Niko zangu tu home sijatoka
nlikuwa naangalia Muvi mara LUKU imekata hapa na
sina hata Salio.Una Sh 30,000 unitumie ninunue Luku babe wangu?Please maana kutoka mpaka ATM saa
hizi usiku.Love you xoxoxo"
Akimaliza Anatengeneza BROADCAST LIST
anawaweka yale Madanga humo halafu anatafuta
Option inaitwa SEND TO MANY,anafowadi lile meseji
TWAAAAP!!Anauchuna kama dakika 5 hivi,meseji za Muamala zinaanza kutiririka kutoka Ukonga mpaka
Tegeta,Sinza mpaka Makongo Juu
"Imethibitishwa umepokea 30,000 kutoka kwa Rajabu
Kistuli"
"Imethibitishwa umepokea 32,000 kutoka kwa Justine
Kipipa" Nusu saa tu kashakusanya LAKI 6 kesho yake
anaamka anaenda dukani kwa @heavenhairtz @
heavenhairtz
anaagiza Peruvian yake ya Inchi 6 jioni unamkuta
NEWS CAFE anawaka huku anakunywa Milkshake ya
Vanilla. We unabaki kujiuliza Demu wa 1st year ana iPhone 6s
kaipata wapi na Bodi ya Mikopo haijaingiza
BOOM,wenzio wana MABOOM BINAFSI wanaCLICK tu
hela kibwena.
Demu akiamua Kupauka ni Maamuzi binafsi tu,Wana
Mbinu hawa Viumbe Balaa,kufa njaa labda awe Mgoloko wa Tandahimba amekuja juzijuzi na Fuso la
Mafenesi ila watoto wa mjini hawaishiwi!

7/29/2016

MSAJILI WA VYAMA AITOLEA MANENO MAKALI CHADEMA

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali  tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayokataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.

“Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.

Nakuongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.

Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).

Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.

Jaji Mutungi ametoa rai kwa  Viongozi wa Vyama vya Siasa  waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.

Katika tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa zitahusika.

KIM KADASHIAN AMUANIKA MTOTO WAKE WA MIEZI SABA AIKIWA NA KANYE WEST

MKE wa rapa maarufu Kanye West kutoka Marekani, Kim Kardashian amemuonesha mtoto wao Saint West kwa mara ya kwanza mbele ya umati.

Kim amemwonesha mwanaye huyo wa pili mwenye umri wa miezi saba wakati wa kipindi cha Keeping Up With The Kardashians kinachoruka kwenye runika kikielezea maisha halisi ya Kim Kardashian na familia yake.


ALSHABABU WAIVAMIA KENYA WAANZA NA KITUO CHA MAWASILIANO

Washukiwa wa kundi la Al-Shabaab mapema leo Alhamisi wameshambulia na kulipua mtambo wa mawasiliano ulioko katika mji wa Fino, Lafey katika kaunti ndogo ya Mandera nchini Kenya.
Afisa mkuu wa Polisi huko Lafey, Bosita Omukolongolo, amesema kuwa kisa hicho kilitokea saa nane usiku.

Afisa huyo wa Polisi anasema kuwa walikabiliana vikali na wanamgambo hao, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa upande wa polisi waliokuwa wakiulinda mlingoti huo wenye vifaa vya kupeperusha mawasiliano.

Kundi la Al- Shaabab, ambalo lina makao yake nchini Somalia, limehusika na mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na mauaji nchini Kenya na mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki na upembe wa Afrika.

PAPA AISHIWA NGUVU NA KUANGUKA, DOKTA AKATISHA TAMAA.

POLAND: Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, ameanguka ghafla wakati akiwa anaongoza misa, baada ya kujisikia vibaya.
Inadaiwa Papa husumbuliwa na tatizo la maumivu ya miguu na mgongo

KAJALA KUANGUSHA MACHOZI GEREZANI KWA MUMEWE

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ hivi karibuni amekwenda kumlilia mumewe, Faraji Chambo anayetumikia kifungo cha miaka kumi na mbili gerezani.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala, mwanamama huyo alitinga kwenye Gereza la Ukonga, Dar alikofungwa mumewe ambapo alipata nafasi ya kumjulia hali kisha kumwaga machozi akimuonea huruma anavyosota gerezani hasa akikumbuka walivyokuwa wakiishi kabla ya msala huo.

Katika safari hiyo, Kajala aliongozana na mwanaye, Paula Paul na mdogo wake Kajala ambao ndiyo waliokuwa wakimtuliza staa huyo ambaye alisababisha mumewe naye kutokwa machozi.
Akizungumzia ishu hiyo, Kajala ambaye wiki iliyopita alizindua filamu yake kali ya Sikitu alisema kuwa ni utaratibu wake wa mara kwa mara kwenda kumjulia hali mumewe huyo ila mara zote huwa anakwenda kimyakimya.

“Huwa nakwenda mara nyingi tu sema ndiyo hivyo huwa sipendi kuongozana na msururu mrefu, namshukuru Mungu anaendelea vizuri,” alisema Kajala. Machi 2013, Kajala na Faraji walihukumiwa ambapo Kajala alitakiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya shilingi milioni kumi na tatu na mumewe miaka kumi na mbili au faini ya shilingi milioni mia mbili kwa kosa la kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar.

KajalacropHarusiHata hivyo, Faraji alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ gerezani huku Wema Sepetu ‘Madam’ akimlipia Kajala faini ya shilingi milioni kumi na tatu, iliyomnusuru kwenda jela.

Chanzo:Global Publishers

TUNDA WA YOUND DEE WA MWAGANA RASMI TUNDA AACHA UJUMBE MZITO

MUUZA nyago macha-chari Bongo, Tunda Sebastian amefunguka kumwagana na mwandani wake wa muda mrefu, ambaye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ na kusema ameamua kujiweka kando kwenye maswala ya mapenzi.
Akipiga stori na Showbiz Xtra baada ya kumbananisha kuhusiana na tetesi za uhusiano wake kuvunjika kutokana Young D kubaini anatoka na mwanamuziki mwenziye (jina kapuni) ndipo akaeleza kuwa, ishu hiyo haina ukweli ila ameachana na mwandani wake huyo kwa sababu ambazo hawezi kuzianika kwa sasa.

“Hayo ya kutoka na huyo msanii si kweli na kuhusu Young D nimeshaachana, sifikirii kuwa na msanii yeyote na sihitaji mpenzi kwa sasa,” alisema.

TP MAZEMBE YAIPA MATUMAINI YANGU KUPATA USHINDI KWENYE MICHUANO

Maombi na furaha ya watanzania wote wazalendo ni kuona Yanga ikifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika CAF, licha ya kuwa nafasi yao kwa sasa inatajwa kuwa ndogo, lakini Yanga wanayo nafasi ya kusonga mbele licha ya kuwa na point moja na wapo mkiani.
Safari ya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya CAF inamlazimu ashinde mechi zake zote mbili zilizosalia za MO Bejaia atakayocheza nyumbani na mechi dhidi ya TP Mazembe atakayocheza ugenini, huku akiombea mechi ya mwisho kati ya MO Bejaia ya Algeria dhidi ya Medeama imalizike kwa sare ya aina yoyote ile.




TP Mazembe bado imeendelea kuipa matumaini Yanga baada ya mchezo wa leo kufanikiwa kuifunga MO Bejaia kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Rainford Kalaba dakika ya 62, kwani kama TP Mazembe angefungwa leo Yanga wangekuwa rasmi wameaga michuano hiyo wakiwa wamesalia na michezo yao miwili mkononi.

MAUMIU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA

Habari zenu jamani,
Mwenzeni ninatatizo yaani toka nijue mapenzi sijawahi kufurahia tendo hilo. Kila nikifanya mapenzi napata maumivu makali mno muda mwingine nahisi maumivu hadi kwenye kizazi. Nikimaliza tu maumivu siyapati mpaka nikifanya tena. Nifanyeje jamani, msinitukane tafadhali.

Karibuni kwa ushauri

CHADEMA WATANGAZA KUPAMBANA NA UDIKTEKTA (UKUTA)

Leo Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya kikao chake katika Hoteli ya Bahari Beach Ledger Plaza.
Mojawapo ya Maazimio ya Kikao hicho ni kuundwa kwa kile walichokiita Umoja Wa Kupinga Udikteta Tanzania(UKUTA). Tuweke Kumbukumbu sahihi, Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoketi siyo Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Hii ina maana kwamba maazimio ya kuundwa kwa UKUTA ni matakwa ya Chama kimoja yaani CHADEMA. Ikumbukwe kuwa UKAWA uliundwa kwa makubaliano ya vyama vinne vya CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD. Hakuna namna yoyote ya kuwashawishi Watanzania kuwa hiki wanachokiita UKUTA ni Umoja, Umoja lazima ushirikishe pande watu zaidi ya mmoja au zaidi ya vikundi viwili au zaidi ya vyama viwili.

Mtazamo: Kabla ya UKAWA, Kambi rasmi ya Upinzani iliundwa na chama kimoja cha CHADEMA. Ni katika kipindi hicho ambapo Chadema na CUF walikuwa na msuguano mkubwa hadi kupelekea CHADEMA kuwaita CUF , CCM B huku CUF wakiwaita CHADEMA chama cha MASHOGA.

Baada ya Chadema kuondokewa na Makada wake maarufu walioshiriki kikamikifu kukijenga chama wakiongozwa na Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, CHADEMA kiliyumba sana na kutafuta kila namna ya kukinusuru na anguko kuu. Ndipo Mungu aliposikiliza maombi yao na bila kutarajia, Ibrahim Harouna Lipumba akaibuka na wazo la kuundwa kwa UKAWA wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

CHADEMA wakaingia kwenye umoja huu kwa malengo makubwa ya kufufuka jambo ambalo CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD hawakujua. Haraka sana, Mbowe akaenda kutangaza kulivunja baraza kivuli lililokuwa na Wabunge wa Chadema pekee na kuunda jipya lenye kujumuisha Wabunge wa UKAWA. Ni katika umoja huo wa wajanja CHADEMA na mambumbumbu wa CUF, NCCR na NLD uliokipaisha chadema na kwa ujanjajanja hio CUF, NCCR na NLD wakajikuta wanamuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA huku viongozi wa CUF, NCCR na NLD wakitumiwa kama vibaraka na wale wa CHADEMA. NCCR, NLD na CUF vimebaki majina.

Uamuzi wa CHADEMA leo wa kuuda UKUTA si chochote wala si lolote. Hizi ni hila tu vinafanyiwa vyama vya NCCR, CUF na NLD. Chadema wameona wameshajiweza, wanaamua kujivua GAMBA kutoka katika mikono ya UKAWA ili wajitegemee
Swali ni je CUF, NCCR na NLD wanalijua hilo? Wako tayari kuitwa washirika wa UKUTA wakati UKUTA umetokana na maazimio ya KAMATI KUU YA CHADEMA? Je UKUTA hautawapoteza viongozi makini kama ambavyo UKAWA ukiwapoteza akina Dr. Slaa na Prof. Ibrahim Harouna Lipumba

7/27/2016

WEMA SEPETU AVUNJA RECODI BONGO MASTAA WAMSHANGAA HUKO INSTAGRAM.

Baada ya Mwanamuziki Diamond Platnumz Kuvunja Record ya kuwa msanii wa kwanza kufikisha wafuasi Million mbili kwenye Instagram Africa Mashariki , sasa Wema Sepetu nae amekuwa mwanamke wa kwanza kufikisha idadi hiyo ya followers million 2 kwenye mtandao wa Instagram,

PETITMAN WAKUACHE AMRUDIA ESMA DADA WA DIAMOND PLATNUMZ.

Utata uliokuwepo kati ya wapenzi wawili Petitman na mama watoto wake umekwisha baada ya vuta nikuvute ya familia hizo mbili. Mama mzazi wa Petitman amewahi kusikika akisema kuwa hamtaki Esma kuwa mkwe wake kutokana na vitendo vyake.
Pia walakini mwingine wa mapenzi haya ulikuwa mgumu pale Madam Wema Sepetu alipotengana na Diamond Platnumz kipindi kile na kupelekea kukosa ushirikiano kwa kutokea makundi mawili kati ya Petiti na madam na upande wa Diamond Platnumz na mdogo wake Esma

Wadau wengi wanasema kurudiana kati ya Petitman na mdogo wa Diamond ni kwa sababu sasa hivi Petit hayupo tena na Wema kitendo kilichomfanya Esma kurudiana kiurahisi na baba watoto wake kwa kuwa hakukuwa na kipingamizi tena.

Hata hivyo Petitman usiku wa juzi mbele ya camera za eNewz na umati wa watu alisema “sioni haja ya kuendelea kuchepuka na wanawake wengine kwa kuwa nimeona kuwa na mademu wengine ni kujipa stress tu, kwa kifupi nimezima simu feki na nimerudiana na mzazi mwenzangu ili tuweze kumlea mweznetu kwa pamoja”.

AUNT EZEKIEL, AKIMBILIA GYM AFOHIA KUTEMWA NA MOUZE IYOBO

Staa wa filamu, Aunt Ezekiel aliye katika mapenzi na Dansa Moses Iyobo, ameamua kukimbilia gym kwa ajili ya kupunguza unene unaomuandama ili kulinusuru penzi lake.
Akizungumza na Za Motomoto News, Aunt amesema ameanza mazoezi ya nguvu kila asubuhi ili aweze kupunguza mwili aendane na mpenzi wake kwani mwili wake ni mkubwa kuliko wa mwenzie.


“Daah, nimeona nitapoteza penzi langu bure, nimekuwa mnene kumpita baby kitu ambacho siyo sawa, nilikuwa na kilo 87, hivi sasa nimepunguza kilo sita,” alisema.

7/25/2016

JAMAA AINGIA NA BODABODA KWENYE MWENDO KASI ..MMMMH DAR NOUMA SANA

Bado haijafahamika vizuri nini kiliendelea mpaka wahusika wa Mabasi ya Mwendo kasi pamoja na dereva kuruhusu piki piki kuingia kwenye basi la mwendo kasi sambamba na Abiria...
Picha hii leo umekuwa ikizunguka sana mitandaoni na kila mtu kuuliza kunani?

RAIS SHEIN WA ZANZIBAR AANZA KUTUMBUA MAJIPU UCHUNGU, AFUATA NYAYO ZA JP MAGUFULI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amefuta uteuzi wa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Hafidh Ussi Haji huku akimteua Khadija Shamte Mzee, kuchukua nafasi hiyo.


Pia, taarifa ya Ikulu inaonyesha Dk Shein, amemteua Amour Hamil Bakari kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuchukua nafasi ya Abdi Khamis Faki ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.



Vilevile, Dk Shein amemteua Umi Aley kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali; Said Bakar Jecha na Sebtuu Mohammed Nassor wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakati Ali Saleh Mwinyikai ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.

Wengine walioteuliwa ni Maryam Hamdan kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni, wakati Maryam Abdulla Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani Zanzibar na Profesa Ali Seif Mshimba,
 ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Zanzibar. Uteuzi huo unaanza Julai 25.

LULU, HIKI NDIO CHAMA CHANGU JAMANI...

Alipoulizwa yeye shabiki wa chama gani cha siasa?, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alijibu hivii; "Mimi sina chama, ndiyo maana hata katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, sijaonekana kwenye jukwaa lolote. Miye naamini kura ni siri na nilifanya hivyo ili nisifungamane na upande wowote." Alifanya vizuri au alichemka?

LULU, MIMI NA MAMA KANUMBA HATUNA CHUKI KATI YETU.

STORI zilivuma na bado vuguvugu linaendelea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu uhusiano wa staa wa kike katika filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mama Kanumba, Flora Mtegoa kuwa siyo mzuri kama zamani.
Watoa habari wa mjini, wanadai kuwa mama Kanumba na Lulu kwa muda mrefu sasa hawapikiki chungu kimoja kama ilivyokuwa zamani.

Lulu alikuwa mchumba wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ambaye alifariki dunia Jumamosi ya Aprili 07, 2012, nyumbani kwake, Sinza – Vatican jijini Dar es Salaam.

Mbali na mitandao ya kijamii kukuza kinachoitwa bifu kati ya mtu na mkwewe huyo, magazeti mbalimbali yalipata kuripoti kuhusiana na kuwepo kwa kutokuelewana baina yao.

Katika mahojiano na My Style ya Swaggaz ndani ya Mtanzania Jumamosi, Lulu alifunguka mengi kuhusiana na madai ya bifu hilo, akikiri kuwepo lakini akasema kuwa kwa sasa imebaki stori tu.

Akizungumzia hilo anasema: “Ni kweli kuna wakati  kulitokea kutoelewana kidogo na naweza kusema ni jambo la kawaida. Jamani binadamu kutofautiana mitazamo wakati fulani si kitu cha kushangaza.

“Lakini hayo mambo yalishaisha kabisa. Mimi na mama Kanumba tupo vizuri sana kwa sasa. Sina ugomvi naye,  tunaelewana na tunaishi vizuri kabisa. Mikwaruzano ya mwanzo iliisha na tunaendelea vyema.”

Lulu anawaangushia lawama watu wenye tabia za kukuza mambo mitandaoni ambao hawamtakii mema kwa kuzusha kuwa bado wana bifu.

“Tatizo kuna watu hawana kazi za kufanya, kazi yao kushinda mitandaoni na kutunga habari za uongo au kukuza mambo ambayo hayapo. Watu waache, mimi sina tatizo na mama Kanumba.

“Yule ni mtu mzima, nawezaje kuwa na bifu naye? Ninachoweza kusema ni kwamba kulikuwa na kupishana kauli kidogo, lakini hayo mambo yameshaisha, watu wasijaribu kuendelea kukuza,” anasema Lulu ambaye ni mshindi wa Tuzo ya  Africa Magic Viewer’s Choice Awards katika kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu ambayo mama Kanumba pia ameshiriki.

MY STYLE: Unapenda kuishi vipi wewe kama staa?

LULU: Kama binti napenda maisha mazuri ndiyo maana najituma ili niweze kufanikiwa. Kama nilivyosema huwa sipendi uzushi na ugomvi, ndiyo maana ninapozushiwa au kutukanwa mara nyingi huwa nanyamaza kwa kuwa sipendi malumbano na watu. Napenda amani.

MY STYLE: Unajivunia nini katika sanaa yako?

LULU: Nimefanikiwa kimaisha nashukuru, pili najivunia kupata tuzo ya kimataifa kule Lagos, Nigeria. Kwangu ni mwanzo mwema na mwanga mzuri mbele yangu.

MY STYLE:  Lulu ana tofauti gani na waigizaji wengine wa Bongo?

MY STYLE: Lulu ni Lulu hawezi kuwa mtu mwingine na mtu mwingine hawezi kuwa Lulu, nadhani hiyo ndiyo tofauti.

MY STYLE: Unazungumziaje skendo zinazokuandama katika mitandao ya kijamii na wale ambao hukushushia matusi?

LULU: Nachukulia kama changamoto tu katika kazi kwani kuna mambo mengine nahusishwa nayo ila siyajui. Ila ninachojua, hao wanaonitukana ndiyo haohao mashabiki wangu, sema wanajibalaguza tu lakini moyoni wananikubali.

MY STYLE: Wewe ni shabiki wa chama gani cha siasa?

LULU: Mimi sina chama, ndiyo maana hata katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, sijaonekana kwenye jukwaa lolote. Miye naamini kura ni siri na nilifanya hivyo ili nisifungamane na upande wowote.

MY STYLE: Una ushauri gani kwa mastaa wenzako?

LULU: Tushirikiane na kufanya kazi kwa ufanisi, tuongeze juhudi ili tuweze kurudisha hadhi ya soko la filamu kama lilivyokuwa awali.

NEWS, JACKLINE WOLPER AHAMIA CCM RASMI AMTEMA LOWASA

Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper aliyakuwa akimuunga mkono Edward Lowassa katika uchaguzi Mkuu 2015, ametangaza kujiunga na CCM rasmi jana


Wolper alikaribishwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete baada ya kutangaza kujiunga na CCM.



Kitendo hicho kilifanyika katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika jana Julai 23, mkoani Dodoma.

KIKWETE, AMKABIDHI MAGUFULI MAJIPU YA CCM

Mwenyekiti mstaafu wa CCM Dkt Jakaya Kikwete, amekabidhi nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kwa Dkt John Pombe Magufuli, huku akimtaka kushughulikia baadhi ya mapungufu yanayokitia hasara chama ikiwemo kuokoa mali za chama.


Kikwete ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Tanzania, ametoa hotuba yake ya mwisho kama mwenyekiti wa chama hicho leo katika mkutano mkuu maalum uliofanyika mjini Dodoma, na kutoa onyo kwa watu wote wanaoshikilia mali za chama kwa manufaa yao binafsi.


Akitaja baadhi ya mali hizo, Jakaya Kikwete amesema kuna wanachama ambao wamejimilikisha viwanja vya chama hicho bila utaratibu rasmi na kuwapa tahadhari ya kuvirejesha katika chama haraka.


Amemtaka mwenyekiti mpya mpya wa chama hicho kushughulikia suala la viwanja ambavyo bado havijapewa hati ili viendelezwe na kugeuzwa kuwa vitega uchumi na kuongeza wigo wa mapato ya chama.


“Mkoa wa Dar es salaam pekee una viwanja 279 lakini ni 45 pekee ndivyo vina hati angalau UVCCM wanajitahidi kujenga majengo ya vitega uchumi na kuna wazee wengine wa chama wameamua kujimilikisha viwanja vya chama, sisemi kwamba ni MAJIPU hapana, nawakumbusha ili viwanja hivyo viendelezwe, chama kipate mapato”
Aidha Kikwete amewakumbusha wakuu wa wilaya kuwa wanapaswa kutambua mojawapo ya jukumu walilonalo ni kulinda maslahi ya chama katika ngazi ya wilaya.


“Kuna wakuu wa wilaya wamesema eti wao ni wasomi na kwamba siasa haiwahusu, lakini wajue kuwa wao ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya, hivyo wajue kuwa wamewekwa kule kwa makusudi kama kiungo kati ya chama na serikali”
Amesisitiza kuwa ana imani kubwa kuwa Dkt Magufuli anatosha na ataweza kukisimamia vizuri chama hicho

NEWS, MH JP MAGUFULI ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM

Katika Mkutano Mkuu wa CCM unaoendelea leo mjini Dodoma, CCM wamemchagua Rais John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa tano wa Chama cha Mapinduzi.....

MZEE MAKAMBA, GWAJIMA NAAMINI ANALAANA KWA KUMTUKANA KADINALI

Mzee Makamba anadai kuwa Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo. Na kwa tafsiri ya kiafrika mtu mwenye laana siku zote hufanana na mtu aliyechanganyikiwa. 

Ayafanyayo huwa kituko kwa wanaomzunguka, huwafanya watu waingiwe na huruma.
Lakini naamini lengo la Mzee Makamba kumsema Askofu Gwajima ni kumuongezea uadui miongoni mwa wanajamii kwa kuanzia na watu wanaosali kwake. Lengo jingine ni kumchongea kwa Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM.

JK, KIUKWELI HAIKUWA RAHISI KUMSHAWISHI JPM KUWA MWENYE KITI WA CCM

Mwenyekiti wa CCM anayemaliza muda wake anasema kuwa alitumia kila aina ya ushawishi ili Magufuli akubali kumpokea kijiti kabla ya Novemba 2017. Anasema kuwa alimuendea Ikulu kumshawishi ampokee kijiti. Hata hivyo, Rais Magufuli alimjibu kuwa ana mambo mengi ya kushughulikia ndani ya CCM hivyo haoni kuwa ni muda muafaka wa yeye kubeba dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa CCM.

 Kikwete anasema kuwa pamoja na maelezo yake ya kina, hakika Magufuli hakukubali kubeba dhamana hiyo. Mwisho na kwa lengo la kukata mazungumzo hayo, Rais Magufuli alimkaribisha ugali na hivyo jitihada zake zikagonga mwamba.


Anasema kuwa kutokana na hali hiyo, alimtuma Makamu Mwenyekiti Philip Mangula akamshawishi Rais kwani uzee ni dawa. Baada ya mwezi na nusu, Mangula akarudisha jibu kuwa Rais amekubali kuwa Mwenyekiti wa CCM na ndipo tarehe ikapangwa.

Kikwete anasema kuwa hata yeye alimkatalia mzee Mkapa mwaka 2006 kwa sababu kama hizo hizo ambazo. Hata hivyo anasema kuwa tofauti na 2006 ambapo hakukuwa na magazeti chonganishi na mitandao ya kijamii, mwaka huu wamemtungia uongo kuwa eti yeye anang’ang’ania madaraka na kwamba hataki kumkabidhi madaraka Magufuli. Shabaha yao ni kuchochea mfarakano na baada ya kuona CCM ni moja. Anawaomba wana CCM kuwa wamoja kwa vile wapinzani wao kila wanachokamata hakikamatiki.

Anasema kuwa kama angekuwa hataki kuachia nafasi, baada ya awali Rais kusema kuwa hana haraka ya kuwa mwenyekiti wa CCM, asingemtuma mzee Mangula. Aliamua kumtuma mzee Mangula kutokana na umuhimu wa kofia mbili kwa chama na serikali. Anasema kuwa mfumo huu wa kofia mbili una faida kubwa kwa chama na walioasisi mfumo huu waliona mbali. Anasema kuwa yeye hakutaka guu lake liote tende kwa kufanya maamuzi ya kutenganisha kofia.

VIGOGO WA MISITU WOTE NI MAJIPU WATUMBULIWA

SERIKALI imemuondoa katika nafasi yake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda na wakurugenzi wenzake, katika jitihada za kufumua na kusuka upya shirika hilo.



Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza hatua hiyo ya serikali jana alipokutana na vyombo vya habari na kuongeza kuwa, watumishi wengine 41 wamehamishwa vituo vya kazi.



Alifafanua kuwa hatua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lililotaka kufumuliwa na kusukwa upya kwa TFS ili kuongeza ufanisi.



Kutokana na hatua hiyo, Waziri Maghembe alisema Profesa Dos Santos Silayo ameteuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, wakati Kamwenda anahamishiwa Chuo cha Viwanda vya Misitu kilichopo Moshi.



Aidha, Mwanaidi Kijazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali za Misitu na Nyuki, yeye amekwenda kuwa Mhifadhi Mkuu Amani Nature Reserve na nafasi yake inachukuliwa na Zawadi Mbwambo.



Waziri Maghembe alisema Mohamed Kilongo aliyesimamishwa kazi Januari 5, mwaka huu uchunguzi umeonekana hana hatia na hivyo anaendelea kuwa Mkurugenzi Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu.



Alisema Wizara imeamua Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Gladnes Mkamba ahamishiwe Idara ya Mipango makao makuu na nafasi hiyo kuteuliwa Dk Ezekiel Mwakalukwa, kuwa Kaimu Mkurugenzi.



Aidha Monica Kagya aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, anakuwa Mtafiti Mwandamizi Idara ya Nyuki (Tawiri). Alisema Kagya ni mtaalamu wa masuala ya nyuki, hivyo atahamishiwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, ili ashughulikie utafiti wa masuala ya nyuki.



Pia alisema katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa anakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Herman Kerayo ambaye anahamishiwa Idara ya Mipango Makao Makuu.



Profesa Ramadhan Kideghesho, yeye anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Mweka wakati Mabula Misungwi aliyekuwa Meneja Mradi Selous, anakwenda Chuo cha Wanyamapori Pasiansi na nafasi yake inachukuliwa na Jaffary Lyimo, huku Robert Mande akipelekwa kuwa Kaimu Mkurugenzi msaidizi Uzuiaji Ujangili.



Waziri Maghembe alisema Majjid Ally ameteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Leseni, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Haji Mpya ambaye amehamishiwa Shamba Jipya Songea kuwa Ofisa Misitu Alisema Julai 18, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikutana na viongozi na watumishi wa Wizara hiyo na watendaji wakuu na watumishi wa TFS na kuagiza kufumuliwa na kusukwa upya kwa wakala huo.



Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alitaka kuondolewa kwa utitiri wa vituo vya ukaguzi na kuwekwa vituo vichache na kuondolewa kwa ofisi za makontena yanayotumiwa na ofisi ya TFS, badala yake watumishi wanaofanya ukaguzi wasimame mahali pa wazi ili kuondoa mianya ya rushwa na kuweka uwazi katika utendaji.

HAKUNATENA KUTUMIA MAFUTA YA 'KY' NI MARUFUKU.

Mjadala mkali umeendelea nchini Tanzania Kufuatia waziri wa afya wa nchi hiyo kupiga marufuku utumiaji na usambazaji wa vilainishi vinavyotumiwa na wapenzi wa jinsia moja.


Waziri huyo wa Afya Ummy Mwalimu hapo juzi alitanganza kupiga marufuku vilainishi hivyo kwa madai kwamba vimekuwa vikitumiwa vibaya na wapenzi wa jinsia moja na hivyo kusababisha kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi.



Hata hivyo muda mfupi baada ya marufuku hiyo raia wa nchi hiyo walikuwa maoni tofauti.
Mjadala huu uliibuka siku chache baada ya kauli ya hiyo ya waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alipozungumza na waandishi wa habari kuthibitisha kuzuiwa usambazaji wa vilainishi hivyo akidai kuwa inatumika kwa namna ambayo sio sahihi.



Wananchi wa nchi hiyo wengi wanataka suala hilo kujadiliwa kwa upana na serikali ifahamu wapi penye tatizo ili liweze kutatuliwa.



Vilainishi hivi vinavyotajwa kuwa chanzo cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kuhusishwa zaidi na watu wa mapenzi ya jinsia moja.



Hata hivyo,Wataalam wa masuala ya afya wanathibitisha kuwa yapo matumizi mengi yatokanayo na vilainishi hivi iwapo vitatumika ipasavyo. 

MO DEWJI AAMUA KUUGAWA UTAJIRI WAKE KWA WASIO JIWEZA

MKURUGENZI Mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Mohammed Dewji, ameungana na matajiri wakubwa duniani, kutangaza azma ya kugawa nusu ya mali zake kusaidia jamii.


Taarifa kutoka mtandao mashuhuri duniani wa Forbes, imesema kuwa Dewji, ambaye ni bilionea kijana kuliko wote barani Afrika, ameingia katika kundi la matajiri hao ambao wametoa ahadi ya kutoa nusu ya mali zao, kusaidia jamii.



“Baada ya kushuhudia umasikini mkali wakati nikilelewa, siku zote nimekuwa nikijisikia kuwajibika kutoa kwa ajili ya jamii yangu,” amesema Dewji katika barua yake ya kutangaza ahadi hiyo, ambayo ameiweka wazi kwa waandishi wa habari.



Alishukuru wazazi wake kwa kumuunga mkono na kumjengea moyo wa kusaidia jamii na kipekee katika wajibu wake kwa dini yake ya Uislamu wa kutoa na kujali wahitaji na jamii.



Bilionea huyo anakuwa Mtanzania wa kwanza kuungana na matajiri duniani, Bill Gates na Warren Buffett katika kutangaza nia hiyo tangu 2010 na kushauri watu wengine wenye uwezo kujitolea kwa ajili ya jamii.



Kundi la matajiri waliokwisha kutangaza nia hiyo ya kutoa sehemu ya mali zao kwa jamii, limeshafikia 155 kutoka nchi 17, ambapo Juni mwaka huu, kundi hilo linalotambuliwa kwa jina The Giving Pledge, lilitangaza kupata wajumbe wapya 17.



Wajumbe wa mwanzo wa kundi hilo ni pamoja na Eli Broad na mkewe Edythe, John Doerr na mkewe Ann pamoja na mmoja wa wamiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg na mkewe, Priscilla Chan.



Mtandao mashuhuri wa Forbes, umemkadiria Dewji kuwa anamiliki mali zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.1, akiongoza kundi la makampuni ya METL nchini Tanzania, linalojihusisha na biashara za viwanda vya nguo, vinu vya unga na viwanda vya mafuta ya kula, huku kinywaji chake cha Mo Cola, kikiuzwa bei rahisi kuliko kununua Coca-Cola

7/23/2016

JE? WAJUA KUWA POMBE INASABABISHA UGONJWA WA SARATANI. ANGALIA IWANGO VYA KUNYWA.

Watafiti wa afya kupitia jarida la Addiction wamedai kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya unywaji wa pombe na aina saba za saratani.

Aidha wataalamu hao wamegundua kuwa saratani ambazo imegunduliwa zina uhusiano mkubwa na unywaji pombe ni pamoja na saratani ya mdomo na koo, saratani ya kikoromeo, saratani ya ini, saratani ya utumbo mpana, saratani ya matumbo na saratani ya matiti.

Aidha mwezi Januari mwaka huu, afisa mkuu wa afya kutoka nchini Uingereza alitoa tahadhari kuwa unywaji wa pombe kwa kiwango chochote kile kina madhara ndani ya mwili.

Mpaka sasa watu zaidi ya laki tano wanakadiriwa kufa kutokan ana ugonjwa wa saratani kwa mwaka 2012 pekee. Hata hivyo mpaka sasa bado haijabainika kibaiolojia uhusiano wa pombe na saratani inatokeaje


ANDIKA EMAIL YAKO HAPO CHINI KIWE NAKUTUMIA HABARI ZOTE INBOX

KIKWETE AMTINGISHA MH. MAGUFULI KWENYE CHAMA

JAKAYA Kikwete, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anayemaliza muda wake amemtahadharisha mwenyekiti mtarajiwa wa Chama hicho John Magufuli kwa kumweleza kuwa uenyekiti ndani ya CCM siyo lelemama kwani wajumbe wasipoelewa wanachokitaka, wanakuwa wakali sana, anaandika Dany Tibason.
Mbali na kumpa tahadhari hiyo pia alikiri kuwa mwaka jana chama hicho kilikumbwa na misukosuko mingi ambayo ingeweza kukifanya chama hicho kuanguka kwani kilikuwa na mafisi wengi ambao walikuwa wakisubiri mkono udondoke ili washibe
Ametoa kauli hiyo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho ambayo ajenda ilikuwa moja tu ya kujadili na kupitisha jina la mwenyekiti ambalo litapelekwa katika mkutano mkuu kwa lengo la kupigiwa kura.

Kikwete amesema CCM ilikuwa ivunjike wakati wa kipindi kigumu cha uchaguzi wa mwaka jana lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumeweza kukaa imara na kukitafa chama kutovunjika.
“Tunasema kikao kama hiki hatumwi mtoto tunakuja wenyewe kikao cha leo ni kikao cha kihistoria, kwa mamna mbili kwanza ni kikao changu cha mwisho, nikija kwenye NEC ni pale mtakapo niharika lakini tulikubaliana kwamba wazee hao wameishatumikia vya kutosha na tuwaache wapumzike utaratibu wa hapo nyuma ukimaliza uenyekiti unakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu na halmashauri kuu.

“Siku moja Mzee Mkapa akasema bwana mbona sisi wazee mnatusumbua sana mnatuita kila siku na sisi tumeishakuwa wazee tunakaa mpaka saa saba usiku kwa hivi sasa tuacheni, ndipo niliposema hatuwezi na tukaamua kuunda baraza la wazee.

“Tukaona hatuwezi kuwaita kila siku lakini tunawatengenezea baraza la wazee ambalo ni baraza la ushauri kimsingi linahitajika kwa jambo muhimu sana kama ilivyo kuwa mwaka lakini nilijadiliwa nikaambiwa JK hataki wazee lakini nikasema huo ni uhamuzi wa busara kabisa” amesema Kikwete.
“Kuna maswala mkubwa ya chama chetu na uhai wake kama ilivyokuwa mwaka wa jana, eeee chama chetu kilikuwa kimekaa katika msukosuko mkubwa mnaingia hapa watu wanaimba hiki wanaimba kile mjadala mkali lakini nikasema tutavuka tu maadamu tupo ndiyo changamoto ya uongozi.

“Na maadamu CCM haikuvunjika mwaka wa jana haitavunjika tena, maana mafisi yalikaa hapa yanasubiri mkono udondoke lakini haukudondoka na maadam haukudondoka mwaka wa jana CCM haidondoki,”amesema Kikwete.

Amesema rais atakuwa mwenyekiti na wakati mwingine kuna wakati kikao kinakuwa kigumu kwani wajumbe wanataka kutendewa haki wa wasipopata haki zao wanakuwa wakali sana.
Amesema halmashauri kuu ni kikao Muhimu cha uongozi pale ambapo hakuna mikutano ya chama amesema kamati kuu ni kikao cha kusimamia shughuli muhimu za chama na NEC ni kikao cha juu cha kutoa viongozi.

Amesema wajumbe wa vikao ni wepesi sana kusifia lakini wanakuwa wakali sana pale ambapo mambo yanaenda vibaya hivyo kiongozi ni lazima kumsikiliza na kujua nini ambacho wajumbe wanataka.

Amesema wajumbe hao wanakuwa wakali kwa kuwa wanataka mambo ndani ya chama yaende vizuri ili nao ndani ya chama waweze kujivunia.
Mbali na hayo amesema wajumbe wanatakiwa kushirikiana na mwenyekiti mpya ili kukifanya chama kuweza kusonga mbele zaidi.

chaanzo .udspecialy.

 andika email yako nikutumie story kila siku

NYANGUMI AIBUKA NA KUTAKA KUZAMISHA MELI YA WATALII AUSTRALIA

Ni mandhari ya kupendeza sana... Utadhani maonyesho..
Ni wakati nyangumi mmoja aliporuka juu kutoka ndani ya maji ,mita chache tu kutoka mahali boti moja ya watalii ilipokuwa inapita.

Nyangumi kumi na wawili walikuwa wakiogolea karibu na ufuo wa pwani ya kaskazini mwa Sydney nchinI.


Ulikuwa wakati wa msimu wa nyangumi hao kuhama kutoka sehemu moja ya bahari ya Australia hadi nyengine.

John Goodridge ni mmoja waliokuwa wakitazama mwenendo wa nyangumi wakati alipopiga picha hiyo yakuvutia akiwa katika boti nyengine umbali wa mita 500.

‘Kwangu mimi , lilikuwa tukio la kufurahisha, na kuchekesha lakini najua kwaoyaaani watalii hao lilikuwa tukio la kushtusha kweli!


Nyangumi huyo alikuwa na uwezo ha kulitosa boti hilo na pamoja nayo maisha ya makumi ya watalii ,mnyama huyo alikuwa ni mkubwa sana.
Maelfu ya nyangumi wanaelekea Queensland ambako msimu ni baridi zaidi huko.

Viumbe hao wa kuvutia wanatarajiwa kurudi tena bahari ya Antarctic kutoka Septemba hadi Novemba.
"Mara nyingi nyangumi huwa wanashangaa kuona boti baharini lakini ni nadra kwamba wataziandama na kuruka ruka karibu ya vyombo vya baharini
Kwani wakati nyangumi huyo alipofanya hivyo boti lao liliyumba utadhani ni kifiniko cha chupa baharini' John Goodridge ameelezea

7/22/2016

JUVENTUS YATHIBITISHA POGBA ATATUA MAN U MSIMU HUU.

Jose Mourinho ametoa kidokezo cha karibuni zaidi kwamba Manchester United wanataka kumnunua tena Paul Pogba kutoka Juventus ya Italia.

Mourinho amesema “mmeona moshi, jueni kuna moto”.
United wanadaiwa kutoa £100m, ambayo ni rekodi ya dunia, kumnunua mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 23.



Pogba aliondoka Old Trafford mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 19.
Manchester United walilipwa £800,000 pekee na klabu hiyo ya Italia.


Image copyright Getty
"Sitawafanya kuwa watu wasiojua na kutaka kuwaonesha kwamba hatujaribu kumnunua mchezaji mmoja,” amesema Mourinho.
Meneja huyo kufikia sasa amenunua wachezaji watatu: beki Eric Bailly kutoka Villarreal, kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund na mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kumnunua Pogba, Mourinho alisema: “Tulijiwekea malengo matatu, tulipata watatu na tutampata huyo wa nne.”