Mourinho amesema “mmeona moshi, jueni kuna moto”.
United wanadaiwa kutoa £100m, ambayo ni rekodi ya dunia, kumnunua mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 23.
Manchester United walilipwa £800,000 pekee na klabu hiyo ya Italia.
Meneja huyo kufikia sasa amenunua wachezaji watatu: beki Eric Bailly kutoka Villarreal, kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund na mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic.
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kumnunua Pogba, Mourinho alisema: “Tulijiwekea malengo matatu, tulipata watatu na tutampata huyo wa nne.”

No comments:
Post a Comment