Header Ads

PICHA 4;GARI ATAKAYO NUNUA DIAMOND PLATNUM 2016

Mwimbaji kutoka kwenye muziki wa bongofleva Diamond Platnumz alikaa kwenye Exclusive Interview ya DJ ALCHAMA na kuzungumza vitu vingi sana kuhusu maisha yake na muziki wake ambapo moja ya maswali aliyoyajibu kwa kujiachia na akiwa ana tabasamu ni kuhusu kununua gari la ndoto yake.
Platnumz alimwambia DJ  ALCHAMA >>> ‘Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekua ni muda mrefu, nafikiri ni muda wa kuwa na gari nililokua nalitamani siku zote, gari la ndoto yangu ni Rolls royce na ndio ninalotaka kulinunua mwaka huu wa 2016 na litakua na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida’
‘Mbali na kuwa msanii nimeshakuwa C.E.O sasa na kuna baadhi ya vikao ukija na gari ya kitoto huwezi kufanya dili vizuri, kuna baadhi ya sehemu siwezi kwenda naendesha mimi… pia siwezi kuendeshwa nikiwa nimekaa kwenye X6 naonekana kama muhuni tu… ndio maana nikipata Rolls royce inatengeneza heshima‘ – Diamond On DJ ALCHAMA





Powered by Blogger.