Pages

8/22/2016

DIAMOND PLATNUMZ,AZUNGUMZIA MTOTO WA PILI KWA ZARI

Mkali wa smash hit iitwayo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wake wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.

Taarifa hizo staa huyo alizitoa leo August 21, 2016 kwenye mtandao wake wa instagram na kuyaandika haya:
Ukiwa na Mwanamke Mzuri, Superstar, Ambae shilingi Mia miambili haimpigi chenga, Halaf ana akili, Akakuzalia Mtoto wa kike’‘Halaf mtoto nae Star, halaf akawa na Mimba yako Nyingine ya mtoto wakiume.. basi unajionea Mashia Muruaaaaaaaaaaaaaaaa๐Ÿ˜Š๐Ÿ˜„๐Ÿ˜๐Ÿ˜š๐Ÿ˜…Lol yani Hapa najikuta kama sjui Biligeti Mzee wa Kwio๐Ÿ˜Š๐Ÿ˜† ๐Ÿ˜˜๐Ÿ˜๐Ÿ’ž๐Ÿ’•๐Ÿ’ Mi nampenda huyu dada’– Diamond Platnumz

MTOTO WA BALACK OBAMA,ANASWA AKIVUTA BANGI!




Hivi karibuni, Malia alionekana akivuta bangi kwenye tamasha moja maarufu.

Kwa mujibu wa tovuti ya RadarOnline, vitendo vya hivi karibuni vya Malia vimemsononesha sana Obama anayemaliza muda wake mwaka huu kama rais wa Marekani.

Awali, video ilisambaa mtandaoni ikimuonesha Malia Obama, 18, akionekana kuvuta bangi kwenye tamasha la Lollapalooza huko Chicago mwezi uliopita.

Kisha Malia alihudhuria kwenye party iliyopo kwenye kisiwa ambacho familia yake ipo mapumzikoni iliyofungwa na polisi. Malia alihitimu mwaka huu kwenye shule maalum ya Sidwell Friends ya Washington, DC, na anatarajiwa kujiunga na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2017.

MR BLUE, NAJ WA BARAKA DA PRINCE ATANIZINGUA NA NDOA YANGU


Mr Blue na Mkewe Walda Katika Pozi 
Baada ya kuibuka kwa madai ya kuwa Mr Blue na Ex wake wa zamani Naj huwenda wakawa wanawasiliana, kumekuwa na vijembe vya maneno kutoka kwenye kambi ya Mr Blue ambavo vinahisiwa huwenda vikawa vinaelekezwa katika kambi ya Barakah Da Prince na Naj.
mr blue

Ilo limeibuka baada ya kipindi cha U-Heard cha Clouds FM kudai Barakah Da Prince ambaye ni mpenzi wa Naj, wiki chache zilizopita akiwa ameshika simu ya mpenzi wake huyo, alipiga mtu ambaye namba yake ‘iliseviwa’ Zai na baada ya Barakah kupokea alikuta sio mwanamke bali ni mwanaume ambaye alidaiwa kuwa ni Mr Blue.

Sakata hilo linadaiwa kuitikisa kambi ya Mr Blue, ambapo wiki hii rapper huyo alipost picha ya mke wake aitwae Walda na kuandika ujumbe wa kumfariji mpenzi wake huyo.

“Hakuna zaidi yako ndo maana nimekuoa,” aliandika Mr Blue kupitia instagram yake.

Baada ya kauli hiyo, Ijumaa hii mke wa Mr Blue ameonyesha kuguzwa na mambo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na kuamua kufunguka.

“Mke na mume hatutoi kiki endelea kuhangaika @mrbluebyser1988,” aliandika Walda instagram katika picha akiwa na mume wake.

Hata hivyo kambi ya Barakah Da Prince na Naj inaonyesha iko sawa kwani wawili hao wanaonekana kuwa na furaha.

KASIM MGANGA,TIP TOP WANANIKWAMISHA KIAINA

Msanii Kassim Mganga ambaye awali alikuwa ni moja kati ya wasanii kutoka katika kundi la Tip Top Connection amesema ukimya wa kundi hilo unamuumiza na kumgusa sababu yeye bado ni mwanafamilia wa Tip Top Connection licha ya kutofautiana kibiashara.

Kassim Mganga akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo alisema yeye bado ni mwanafamilia wa Tip Top Connection hivyo alikuwa anapenda kuona familia yake hiyo inaendelea na moto ule ule kama zamani.

“Unajua unapoongelea Tip Top Connection na Kassim Mganga ni kama familia, hivyo ile ni familia yangu japo tulipishana kwenye masuala ya biashara tu. Hivyo kama mwanafamilia wa Tip Top Connection ukimya wao unanigusa na kuniumiza sababu nilikuwa natamani kuona chama linaendelea na moto ule ule kama zamani” alisema Kassim Mganga

Mbali na hilo Kassim Mganga ameahidi kuja na band yake katika siku zijazo kwani anatamani kufanya muziki wa live kwenye show zake.

8/21/2016

MO DEWJI, KUANZA NA MISHAHARA SIMBA

MFANYABIASHARA anayetaka kununua hisa ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameanza kasi ya kuitumikia klabu hiyo ya Simba kwa kuanza kulipa mishahara ya wachezaji kuanzia mwezi huu huku suala la kununua hisa likitarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja.
Hatua hiyo ya Mo imekuja baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba kuridhia kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka wa sasa wa wanachama na kwenda kwenye mfumo wa hisa, kufuatia Mo kuhitaji kununua hisa asilimia 51.

Mohamed Dewji ‘Mo’ (kushoto)  akisalimiana na viongozi wa Simba.
Aidha, kamati itaandaa mkataba wa maridhiano ili kila upande uweze kutekeleza majukumu yake ambapo Mo alieleza kuwa ataisaidia timu hiyo huku akiwa anaendelea kusubiria mchakato wa hisa kukamilika.

Akizungumza na Championi Jumamosi, mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji Simba ambaye aliomba jina lake lifichwe, alisema Mo ataanza kuwalipa wachezaji mishahara kuanzia mwezi huu.
“Kwa sasa kuna kamati imepewa kazi ya kuwaelimisha wanachama juu ya suala hilo ili kuweza kufahamu faida gani watakayoipata juu ya suala hilo ili mwisho wa siku yafanyike maamuzi sahihi.


“Kwa kuanza, ataanza na kuwalipa mishahara wachezaji ambapo itaanzia mwezi huu na atapewa majina ya wachezaji wanaotakiwa kulipwa mishahara ili aweze kuwalipa wachezaji wote lakini jukumu alilopewa ni juu ya timu tu kwa sasa lakini mambo mengine yote yatabaki chini ya uongozi.
“Suala lake nadhani litachukua muda mrefu hata mwaka mmoja hadi kufikia kukamilika kwa mchakato mzima kufuatia kupata maoni mbalimbali na makubaliano kutoka kwa wanachama baada ya kupata elimu ya kutosha.

“Hata hivyo asilimia kubwa ya wanachama hawataki auziwe hisa kubwa ya asilimia 51 na badala yake auziwe asilimia 48,” alisema bosi huyo.

Alipotafutwa Msemaji wa Simba, Haji Manara kuzungumzia suala hilo, simu yake iliita bila ya kupokelewa hata katibu, Patrick Kahemele naye simu yake haikupokelewa.

Tayari Mo alishatoa msaada wa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia usajili, kiasi ambacho Simba ilikitumia kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji kadhaa nyota walionao hivi sasa.

IDRIS SULTAN AANZA KUJILAUMU KWA WEMA SEPETU

Msanii wa kuchekesha Idris Sultan amejitoa Rasmi katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kinachosemekana kuwa ni maji kumfika shingoni. Watu wa karibu wa Idris wanasema kuwa Mchekeshaji huyo maarufu Tz amekerwa na tabia ya mashabiki wake kumuita Shemeji wakati yeye Kula hali. Mmmmmh..!

Amesema kwamba yeye ana jina lake na kama angejua kama haya yote yatatokea leo basi asingekubali toka mwanzo kuitwa shemeji, amekasirishwa sana na matusi anayotukanwa pindi akiwaposti wanawake wengine hata dada zake. Pia wapo waliodai kuwa anatafuta kiki na anamuiga Justine Beiber kwasababu siku sio nyingi ataifungua tena na kuendelea na vichekesho vyake kama kawa.

Haya sasa Wenye shemeji mpo?

ZLATAN IBRAHIMOVIC' AREJESHA FURAHA MANCHESTAR UNITED

Ligi Kuu England iliendelea usiku wa August 19 kwa klabu ya Man United kuwakabribisha Southampton katika dimba lao la Old Trafford kucheza mchezo wao wa pili wa baada ya mchezo wao wa awali kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya AFC Bournemouth ugenini.

Zlatan lifunga goli la kwanza baada ya kupokea krosi maridhawa kutoka upande wa kulia na Wayne Rooney baadae tena Zlatan alifunga bao la pili kwa njia ya penati baada ya beki wa kushoto wa Man United Luke Shaw kufanyiwa madhambi na Jordy Clasie na mechi hiyo kumalizika kwa Man United kupata ushindi wa 2-0.

MH:TUNDU LISU AISHANGAZA MAHAKAMA...Kesi yake yavunja rekodi

Serikali imeendelea kupigwa mweleka katika kesi ya uchochezi dhidi ya mshitakiwa Tundu Lissu baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutupa pingamizi la Wakili wa Serikali wakitaka wakili Peter Kibatala kujitoa kumtetea mwanasiasa huyo.

Lissu, ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alipandishwa kizimbani Agosti 5, na kusomewa mashtaka matatu, mawili kati yake yakiwa ni ya uchochezi na moja la kuidharau mahakama.

Pigo la kwanza la upande wa mashtaka ni pale Lissu alipopangua hoja na kufanikiwa kupata dhamana, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza.

Jana ilikuwa ushindi mwingine kwa upande wa utetezi, baada ya Mahakama kutupa pingamizi la upande wa mashtaka lililotaka Kibatala ajitoe katika jopo la mawakili wanaomtetea Lissu.

Upande wa mashtaka ulioongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, uliweka pingamizi hilo kwa maelezo Kibatala ni shahidi wao kwa kuwa alikuwapo siku na mahali wakati Lissu akitoa maneno yanayodaiwa ya uchochezi.

Wakili Kibatala ambaye ni kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Lissu, alipinga hoja za Serikali za kutaka ajitoe katika kesi hiyo, mvutano ambao ulisababisha kesi hiyo kuahirishwa mara mbili.

Wakili Kibatala alipinga kuwa hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia wakili kumtetea mteja wake kwa sababu tu ya kushuhudia akitoa maelezo yake Polisi.

Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo la Serikali, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha anayesikiliza kesi hiyo, hakukubaliana na hoja za upande wa Jamhuri (mashtaka) na hivyo akalitupa pingamizi hilo.

Hakimu Mkeha alikubaliana na hoja za wakili Kibatala kuwa hakuna kifungu chochote cha sheria kinachomzuia kumtetea Lissu.

Alisisitiza kuwa Kibatala ataendelea kuwa wakili wa Lissu katika kesi hiyo na kwamba kama upande wa mashtaka ukimhitaji awe shahidi wao utalazimika kumuomba. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 19

8/20/2016

JIFUNZE HAYA KAMA NI MWANAMKE ULIYE SINGLE (Single girl)

1- Kamwe usisahau kumuomba Mungu wako kabla hujasema "YES" kwa yule unaedhani anapaswa kujenga maisha na wewe. Usikimbilie kuolewa. Kama utakimbilia kuolewa, utaikimbia ndoa na tena kwa majeraha makubwa.

2- Tambua lengo lako kabla hujaingia kwenye ndoa. Fanya biashara yoyote, tafuta shughuli ya kufanya. Usimsubiri mwanaume ndio useme unaanza maisha. Ongeza thamani ya maisha yako kwa kujenga maisha yako.

3- Usimkimbilie mwanaume kwa sababu ya pesa zake, magari, connection, cheo, kipaji, ucheshi, au background ya familia yake. Olewa na mwanaume aliye na hofu ya Mungu. Hapo utakua umekula BINGO...!

4- Jenga tabia ya kula vizuri kwa afya. Usile alimradi umekula. Kula vyakula vya kujenga mwili na uwe mlo kamili. Fanya mazoezi mara kwa mara kuepuka unene usio wa lazima.

5- Vaa vizuri. "first impression counts" hii inamaanisha kwamba muonekano wa mwanzo unamaana sana kwa mtu atakayekuona. Usiache maeneo yako ya siri yakaonwa na mwanaume yeyote, vinginevyo utawavutia wale wanaume wakware ambao sio waoaji.

6- Usililie au kulazimisha mwanaume akuoe. Wewe ni wa thamani mno kufanya hivyo. Usilazimishe ndoa kwa kumbebea mimba, wenzako wamefanya hivyo na leo wengi wao wanajuta. Wamebaki wakilea peke yao.

7- Tabia yako ndio Ndoa yako. Hiyo ndio itakayoamua mwanaume aishi na wewe au laa. Jitathimini tabia yako. Uzuri sio kila kitu, kama unajivunia na uzuri wako na unaamini kama ndio utakaokupa mume utapoteza nafasi yako kwa aliye mzuri zaidi yako kwa tabia na sura.

8- Usichoke kujifunza kupika, kujua kupika wali, ugali, mboga na chapati haitoshi. Jifunze zaidi, tizama vipindi vya mapishi, soma vitabu mbalimbali vya mapishi, tembelea page mbalimbali zinazofundisha kupika vyakula aina mbalimbali.

Wanaume mara nyingi wanapenda wanawake wanaojua kupika, wale ambao kila siku wana suprise ya aina mpya ya mapishi. Kwa sababu njia nyingine rahisi ya kutambua moyo wa mwanaume ni kupitia tumbo lake (chakula kizuri)

9- Usiishi kwa mazoea utakapoolewa, soma vitabu vya mahusiano, ndoa na familia. Ongea na wazazi wako na wazee wengine wakupe busara zao. Kupitia kwao akili itaweza kupanuka na kupata ufahamu wa nani haswa atapaswa kuishi na wewe.

10- Acha ushabiki kwenye mitandao ya kijamii mambo ya Team Zari, Team Wema, Team Chura, na mengineyo hayatakusaidia. Wenzako wana maisha yao, muda huo tumia kuhudhuria semina mbalimbali za ndoa, tembelea washauri wa mahusiano na ndoa.

ORIGINAL COMEDY, TAYARI TUMEMALIZANA NA POLISI...Soma ujue waliyojitetea

Baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kuwakamata baadhi ya wasanii wa Kundi la Orijino Komedi kwa kosa la kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za polisi, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Masanja Mkandamizaji amedai tayari wameshamalizana na jeshi hilo baada ya kuomba msamaha.

Mchekeshaji huyo ambaye kwa sasa yupo honey moon visiwani Zanzibar, amesema ameamua kutoa taarifa hiyo ili kuwaondoa hofu baadhi ya mashabiki pamoja na ndugu.

“Jamani asanteni kwa maombi na meseji zenu kuulizia juu ya inshu ya polisi, tunamshukuru mungu tumewaomba msamaha na wametusamehe hivyo imekwisha,” aliandika Masanja facebook.

Aliongeza, “Tumesema tulinogewa na harusi tukasahau kwenda kuomba kibali. Lakini akina Joti, Seki, Maclegan,na Wakuvanga wamepata kautamu kidogo kamahojiano. Na mimi ningekuwa kwenye jiji la Makonda ingenihusu,”

Wasanii hao walikamatwa na jeshi la polisi na kuhojiwa baada ya kuvaa sare zinazofanana ya za jeshi la polisi katika harusi ya msanii mwenzao Masanja Mkanadamizaji.

DIAMOND PLATNUMZ NA ALIKIBA ,HIZI NDIO TOFAUTI ZAO.....soma kuzijua.

KUNA vita ya maneno kati ya makundi mawili ya mashabiki wa Muziki wa Bongo Fleva, wanaowashabikia wasanii Alikiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kila upande ukidai mtu wao ndiye anajua zaidi kuliko mwingine.

Ni mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, mitaani na hata miongoni mwa wasanii wenyewe ambao kwa kificho au waziwazi, wamewahi kuzungumzia nani mkali katika wawili hao ambao wote ni vijana wenye asili ya Kigoma.

Alikiba ama King Kiba, ndiye wa kwanza kuingia na kupata jina katika Muziki wa Bongo Fleva, katikati ya miaka ya 2000 akiwa na singo yake ya kwanza, Cinderella ndiyo ilimfungulia milango, kwani alichomoza hadi juu ambako alidumu kwa muda mrefu.

Huenda Diamond amewahi kuimba kwa kuiga baadhi ya nyimbo za Alikiba, kwa sababu yeye alianza kupata jina mwaka 2009, mwaka ambao mwenzake tayari alishakuwa na albamu mtaani.

Unapotaka kufanya ulinganisho wa wawili hawa ni lazima uchague unataka kuwalinganisha nini, vinginevyo unaweza kujikuta umewekeza katika chuki au ushabiki, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa mfano, vigumu kupata idadi kamili ya mashabiki wa wasanii hao, ingawa mapokeo ya kazi zao yanaweza kumuongoza mtu kuelewa.

Kitu kimoja cha msingi ambacho wengi wanakubaliana ni kwamba Alikiba ana uwezo mkubwa wa kuimba na mwenye sauti nzuri kuliko Diamond. Msanii mmoja chipukizi, Ibrahim Kidugu ‘Wizzy Rapper’ katika kibao chake cha Kote Nisikike, kwenye mojawapo ya vesi anasema “Ali ni mwanamuziki, Nasibu Mfanyabiashara.”

Maana ya Wizzy Rapper ni kuwa Diamond anafanya biashara ya muziki, ndiyo maana anaonekana kuwa juu ya Alikiba ambaye anafanya muziki kwa mazoea.

Katika ubora wake, Alikiba aliwahi kukutana na mkali wa R&B duniani, R Kelly, katika projekti iliyoitwa One8, ambapo wakali nane wa Afrika walifanya ngoma moja iliyoitwa Hands Across Africa ambao walikuwa ni yeye, Fally Ipupa, 2Face, Amani, Movaizhaleine, 4X4, Navio na JK.

Licha ya Kiba kufika nyumbani kwa R Kelly, studio kwake, alishindwa kutumia ushawishi wa msanii huyo mkubwa ili aweze kumsaidia kuingia katika soko la Marekani. Mbaya zaidi, alishindwa pia kujitangaza kimataifa kupitia Fally Ipupa na 2Face ambao ni maarufu kuliko yeye.

Ambwene Yessaya ‘AY’ alimkutanisha Diamond na Davido wa Nigeria na akafanya naye Ngoma ya Number One Remix. Hapa kijana yule wa Tandale hakutaka kuishia kwa msanii huyo pekee, akaingia nchini humo na kufanya kazi na wasanii karibu wote wakubwa, wakiwemo waliofanikiwa zaidi, P Square.

Hiyo imempa Diamond kujulikana zaidi na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, kiasi cha wengi kuhitaji kolabo naye kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, Ivory Coast na kwingineko Afrika.

Alikiba haonekani kuwekeza akili yake yote katika muziki anaoufanya. Ni kama mtu ambaye anafanya muziki kwa kujifurahisha na siyo kufikia malengo ambayo mashabiki wake wangependa aende. Ana uwezo mkubwa nyuma ya Mic, lakini ameshindwa kuutumia ili kuliteka soko.

Kiba anaridhika au labda niseme, mvivu. Katika uhalisia ni makosa kumshindanisha na Diamond kwa sababu haoneshi kama ni mshindani wake. Alipokuwa katika ziara yake Ulaya, akaitumia nafasi adimu aliyoipata kukutana na marehemu Papa Wemba na kufanya naye wimbo.

Baada ya kuliweza soko la Afrika, Diamond anaonekana wazi kulitamani la Ulaya na Marekani na hii ndiyo sababu ya yeye kuwa msanii anayelipwa zaidi kuliko wote kwa sasa hapa Bongo.

Kiba hatafuti kolabo na watu wa nje kwa vile anadhani ataonekana anamuiga mwenzake, wakati katika maisha, kuiga vitu vizuri na vya maendeleo ni jambo la kupongezwa.

Hata hivyo, Kiba anayo nafasi ya kubadilika ili aweze kuwa mshindani wa kweli wa Diamond, vinginevyo asahau.

Chanzo:GPL

8/17/2016

HARMONIZE! AWAJIBU WANAOSEMA ANAM "COPY" DIAMOND PLATNUMZ.........

Msanii kutoka wcb, Harmonize amewabwatukia wale wanaomtupia maneno ya kishamba kuhusiana na yeye eeti anamkopi sana Diamond Platnumz



kupitia Mtandao wa kijamii wa Instagram kwenye akaunti yake ameyaweka wazi hayo,Msanii uyo baada ya kuonekana kwenye video ya INDE ya dully sykes.


"Mhhh copy! copy! copy!..... mwisho wa siku hata ukinya utaambiwa kunya kama wewe usimcopy @diamondplatnumz ebwana mzee #simbaa video ijayo wacha nianze kuvaa Dera maana nguo zote ushazivaa ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ #INDE in my BIO though๐Ÿ˜Š" Aliposti hivyo

8/15/2016

DUH! MAKONDA AIFAGILIA AWAMU YA TANO ,AIPONDA ILE YA JK

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ni bora kuliko serikali ya awamu ya nne, anaandika Faki Sosi.

Makonda ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika utawala wa awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amesema serikali iliyopita ilikuwa na matabaka kati ya viongozi na wananchi tofauti na ilivyo sasa.

Makonda alikuwa akizungumza leo katika kipindi cha Terminal cha Clouds Fm leo alasiri.
“Serikali ya sasa inafanya kazi nzuri zaidi. Kuna tofauti kubwa kati ya ya watawala na viongozi kwa sababu kiongozi anasifa ya kuwasikiliza anaowaongoza lakini mtawala hana sifa hiyo,” amesema Makonda.

Amejinasibu kuwa Mkoa wake wa Dar es Salaam umekuwa Mkoa wa kipekee kwani viongozi wanashirikiana na wananchi moja kwa moja.

KWELI SHILOLE NI 'JIKESHUPA' APATA DOGODOGO NYINGINE ........Huyu ni mdogo zaidi ya Mziwanda

Haya! haya! Tena yule mwanadada mwanamziki wa kizazi kipya 'Shilole' Amezua gumzo lingine tena huko instagram baada ya kutambulisha ki penzi chake kipya ambae naye ameonekana anaumri mdogo zaidi kuliko alivyokuwa Nuh Mziwanda.

kwa kuuskiliza vizuri nyimbo mpya ya Mtoto mdogo ya SHILOLE aliyomshirikisha Man fongo bigwa  wa singeli kwenye nyimbo hiyo imezungumzia mtoto mdogo mwenye nguvu kama za nyati...........mmmmh Shilole hii sasa ni balaa huwenda dogodogo ndio mafundi kwake.
hamadai na shilole wakiwa falagha.

OFISI ZA BUNGE KUHAMIA DODOMA SEPTEMBER MWAKA HUU.

Ofisi za Bunge zilizopo Jijini Dar es salaam zinatarajia kuhamishiwa Dodoma mwezi Septemba mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa agiza la Rais Magufuli la kuhamishia shughuli za serikali Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai jana na kusema kuwa kwa bunge suala la luhamia Dodoma siyo gumu kwa kuwa tayari makao makuu yake yako Dodoma.

Alisema tayari alikwishatoa maagizo kwa ofisi yake kuhakikisha kuwa kufikia mwezi Septemba kila kitu kinachofanyika Dar es salaam kifanyike Dodoma isipokuwa mambo  machache.

"Nimeagiza ofisi yangu ihamie dodoma mara moja kuanzia Septemba hii, watumishi wa bunge karibu wote watahamia Dodoma, masuala ya malipo yataangaliwa baadaye, kwa sasa ni kuhamia dodoma tu, ofisi tunazo huko" Alisema Ndugai

Kama sehemu ya mwanzo wa utekelezaji wa azma hiyo, tayari ofisi ya bunge imetangaza kufanyia Dodoma vikao vyake vyote vya kamati za bunge tofauti na ilivyokuwa umepangwa mwanzo na ilivyozoeleka kufanyikia Dar es salaam.

8/14/2016

PICHA: ZARI AJIACHIA AKIONYESHA UJAUZITO WAKE

Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akijiachia kuonyesha mimba yake, wanatarajia kupata mtoto wa pili na mpenzi wake mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz



BRAZIL YAICHAPA COLOMBIA YATINGA NUSU FINAL OLYMPIC

Timu ya soka ya wanaume ya Brazil, imeingia nusu fainali ya michuano ya Olimpiki baada ya kuwachapa Colombia, 2-0.

Goli la kwanza lilifungwa na mchezaji wa Barcelona, Neymar baada ya kupiga free-kick dakika 12 tu baada ya mchezo kuanza na Luan kuongeza la pili kipindi cha pili.

Brazil sasa itakipiga na Honduras Jumatano kwenye nusu fainali baada ya kuwachapa Korea Kusini, 1-0. Ujerumani itavana na Nigeria waliowafunga Denmark 2-0 na Ujerumani kuwafunga Ureno 4-0.

8/11/2016

HII NDIO FAIDA YA MCHUZI WA PWEZA KWA MWANAUME NA MWANAMKE....isome kujua undani zaidi.


Akizungumza na East Africa Radio katika kipindi cha East Africa Break Fast Prof. Kaale amesema taarifa za utafiti wa wanafunzi wa Muhimbili bado haujakamilika kwani umeishia katika hatua ya wanyama panya na majaribio kabla hayajaenda kwa binadamu lazima yafanyike kwa wanyama wenye mfumo unaofanana kwa kiasi fulani na binadamu.

"Mwanafunzi alinunua pweza akamchemsha mwenyewe, akawapa panya mchuzi akawafuatilia kwa muda wa siku 29 na aliwatenga panya katika makundi mawili kundi moja likapewa maji na lingine likapewa mchuzi wa pweza na mfumo wa ‘genetics’ unafanana sana na binadamu kwa zaidi ya asilimia 95 lakini hatuwezi kusema kwamba umethibitishwa kwa binadamu bila hatua zote kukamilika" Amesema Prof. Kaale

Prof. ameendelea kufafanua kwamba waliopewa supu walionekana kufanya tendo la kujamiiana mara nyingi kuliko wale waliopewa maji hivyo kisayansi huwezi kusema moja kwa moja kwamba tayari na kwa binadamu supu hiyo inaweza kufanya kazi.

Aidha Prof. Kaale ambaye ndiye alisimamia utafiti huo wa awali, amesema hatua zaidi juu ya utafiti huo zitaendele ili kuangalia tena wanyama wengine kabla ya majaribio ya kuja kujiridhisha kwa binadamu

SNURA, KAMA NISINGEKITUMIA KIUNO CHANGU NISINGEKUWA HAPA KIMUZIKI

Msanii Snura ambaye mara nyingi amekuwa akikumbwa na rungu la BASATA kutokana na video zake ambazo zinakuwa na utata, amesema mauno ambayo BASATA 'wanamind' ndio yamemfikisha hapo alipo.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Snura amesema mauno yake ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wake, kutokana na jinsi anavyoyamwaga akiwa jukwaani, na kuwavutia mashabiki wake.



"Nimeimba sana laini kiuno changu kimenisaidia sana kunitambulisha, ukisikia kuna show ya Snura jua mauno yanamwagwa kweli, na sijaanza leo nilianzia kwenye ngoma za asili", alisema Snura. Snura aliendelea kusema kuwa ingawa mauno hayo humpa wakati mgumu akiwa kwenye kazi zake kutokana na uchu wa baadhi ya wanaume wanaomsumbua, lakini amekuwa akijitahidi sana kujilinda ili asiharibu kazi yake.

"Usumbufu kiukweli upo,wengine wananipenda kweli wengine wananitamani, kikubwa nazingatia sana kazi yangu, nashinda sana vishawishi kwa sababu vile ninavyokatika wengine wanadhani nafanya promotion ya biashara", alisema Snura.

HARMONIZE AKANA KUCHUNWA PESA NA MPENZI WAKE.....




Mwanamuziki wa Bongo Flava anayesimamiwa na Wasafi, Harmonize, amekanusha kuchunwa pesa na mpenzi wake Jackline Wolper kutokana na mwanamke huyo kuonekana kuwa na maisha ya kifahari.

Harmonize amekanusha hayo kwa kusema “Nyumbani kwa Wolper kuna kaunta ambayo anaweza kunywa vinywaji atakavyo, pia sioni sababu ya mimi kupendeza na mwanamke wangu asipendeleze ni lazima nitahakikisha anapendeza kwa kuwa ninampenda”.

Harmonize pia alizidi kuweka wazi kuwa mapenzi yake na Wolper hajaathiri kitu chochote kwenye kusaidia familia ya kwao kwa kuwa hata kama asingekuwa na Wolper ni lazima angekuwa kwenye mahusiano.







“Siyo kwamba ninatumia pesa nyingi kumridhisha mpenzi wangu na kusahau familia yangu, Mama yangu na ndugu zangu wanapata pesa za matumizi kama kawaida kwa kuwa ninafanya kazi”.alisema Hrmonize.

ALIKIBA ATAPELI WAKENYE, SHADIDI WAKE APATIKANA, hii ni aibu kubwa

Kashfa! Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ anadaiwa kuwatapeli Wakenya baada ya kupewa Sh. Milioni 33 kwa ajili ya kushirikishwa kwenye wimbo kisha kuingia mitini, hali iliyosababisha shahidi wake, Rajabu Salum ‘Mchafu’ kutaitiwa, Risasi Mchanganyiko lina full data.
Kwa mujibu wa Mchafu ambaye ni meneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda na Billnas, alipigiwa simu na Wakenya hao kumuomba awaunganishe na Ali Kiba.

“Mmoja kati ya Wakenya hao ni mwanamuziki ambaye anaitwa Brown Mauzo, lengo lao kubwa lilikuwa ni Brown kufanya kolabo na Ali, hivyo nikawasiliana naye akakubali kwa sharti la kulipwa dola elfu 15 (zaidi ya milioni 30 za Kibongo).

“Walikuja Bongo, tukakutana nao Mlimani City, nikiwa shahidi wa Ali na wao walikuwa na wanasheria wawili. Wakaingia benki ili kutoa kiasi cha Sh. milioni 10 lakini wakaniomba wasitoe kwanza na kwamba nikabadilishe mkataba kwa kiasi hicho cha pesa watakachoanza nacho maana awali makubaliano ilikuwa ni kiasi hicho cha pesa (shilingi mil. 32) kwa ajili ya video, malazi na makazi.”

“Upande wa video, Ali alitaka dairekta asiwe Mbongo, hivyo tukampata Justin Campos wa Sauz. Kwa upande wa audio, Brown alimhitaji Prodyuza Manecky lakini Ali napo alikataa na kumtaka prodyuza wake ambaye ni Aby Daddy wa Chaiderz Records, hivyo akataka iongezwe tena shilingi milioni moja kumlipa prodyuza huyo, jamaa wakamaindi na kuondoka bila dili kufanyika.

 “Ali akaniambia nikaongee nao kwani hela ya prodyuza lazima ilipwe. Basi nikawafuata hotelini kuongea nao vizuri, tukaelewana wakapanga tuonane usiku, tukasaini na kumkabidhi Ali milioni 20 huku kesho yake wakiahidi kumalizia milioni 13 ili jumla iwe 33.

“Kesho yake, tukakutana studio kwa Aby, wakarekodi na kurudi nchini kwao kusubiri ikamilike. Baada ya siku chache jamaa wakawa wanahitaji wimbo wao.

“Wakatumiwa lakini hawakuridhika wakidai ulitengenezwa chini ya kiwango na haukuwa na ubora. Wakaja Bongo na kushauri ukaboreshwe kwa Man Water (Combination Sound), tukachukua mafaili ya wimbo huo kutoka kwa Aby hadi kwa Man Water.

Kufika huko, Man Walter akashauri irekodiwe upya, naye akahitaji hela nyingine. Ikabidi niwasiliane na bosi wa Brown, Kenya akatuma kiasi kingine cha shilingi milioni moja na nusu, Brown akaingiza tena sauti ikabaki kwa Ali.

“Kila akitafutwa Ali alikuwa akikwepa, akipigiwa simu ikawa hapokei. Siku alipopatikana akadai hawezi kuingiza mara ya pili.

Baadaye katika kupeleleza, tukaja kugundua kumbe Aby alipewa shilingi laki moja na nusu badala ya milioni moja. Aliposikia kwamba Ali amepewa pesa nyingi na yeye amepewa kiduchu, akapoteza morali ya kazi. Tulibishana sana lakini mwishowe, akakubali akaingiza.

“Baada ya kumaliza audio kibishi, jamaa wakawa wanahitaji namba ya pasipoti ya Ali na meneja wake ili wafanye michakato ya kusafirishwa kwenda kutengeneza hiyo video.

“Ikawa kila tukimfuatilia Ali tunaambiwa mara yupo Sauz na Barakah The Prince, mara amerudi yupo kwenye shoo za Bongo, tukimpigia simu anatupiga chenga, hapokei,” alisema Mchafu.
Imeelezwa kuwa, baadaye mabosi hao wa Kenya walipoona mambo hayaeleweki, walimkamata Mchafu kwa muda kama mmoja wa waliosaini mkataba na kwamba baada ya kuongea na Ali,
aliwataka wamlipe fedha aliyofanya wimbo kwa mara ya pili na Man Water, baadaye wakamuachia.
Hata hivyo, Mchafu baada ya kusikika kwenye moja ya redio Bongo akilalamika kwa aliyotendewa, Ali alimpigia simu na kumlaumu sana, baadaye akamwambia amekubali kutengeneza video hiyo ambapo Agosti 10, mwaka huu (leo), wanatarajiwa kusafiri kwenda ‘kushoot’ Sauz.
Baada ya madai hayo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Prodyuza Aby kutaka kujua kama kuna ukweli ambapo alifunguka;

“Kwa sasa sitaki kuongelea kabisa habari hizo ila ninachoweza kusema ni kwamba Wakenya hao walikuja kuchukua mafaili ya wimbo na kupeleka kwa Man Water.”

Baada ya kumsaka Kiba bila mafanikio, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta meneja wa msanii huyo, Seven Mosha ambaye alisema habari hizo hazina ukweli wowote.

“Ni uzushi tu huo, hakuna kitu kama hicho,” alisema Seven kwa kifupi na kuondoka hewani.

Source:GPL

KUFANYA MAPENZI NA BINAMU NI HALALI KENYA..mahakama yapitisha

Mahakama ya juu nchini Kenya imehalalisha ngono baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.

Mahakama hiyo imemuachilia huru mtu mmoja aliyekuwa amefungwa kwa kosa la kushiriki ngono na binamu yake mwaka wa 2014 kwa sababu sio makosa nchini Kenya.

Jaji wa mahakama ya juu James Makau, alisema katika uamuzi kuwa kujamiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya.

''Ibara maalum inachoshughulikia ngono ya maharimu hajata binamu kuwa mmoja wa wale ambao kujamiana nao ni haramu maksudi, kwa sababu baadhi ya jamii nchini Kenya zinaruhusu sio tu ngono bali hata ndo baina yao''

Jaji wa mahakama ya juu James Makau, alisema katika uamuzi kuwa kujamiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya.

''jamii ya wahindi, waislamu na baadhi ya makabila humuhumu Kenya hukubali ndoa baina ya mabinamu'' alisema jaji Makau.

Bwana huyo ambaye anatambulika kama WOO alikamatwa mwaka wa 2014 kwa kushiriki ngono na mpenzi wake wa kike ambaye pia ni binamu yake na akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.

''Kwa ufupi hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha kuwa ngono baina ya wawili hao ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo ninaamuru mtu huyo aachiwe huru mara moja'' hukumu ya jaji Makau

JADA WA BONGO MOVIE, APOTEZA KUMBUKUMBU....Watanzania waombwa kumuombea.

Msanii aliekuwa anachipukia na kuja kwa kasi kwenye tasnia ya uigizaji hapa nchini JADA.amepoteza kumbukumbu zake akiwa anashoot.

Mtunzi na msimamizi wa video nyingi za maigizo Leah Mwendamseke maarufu kama Lamata,aliyazungumza hayo wakati akihojiwa kwenye kipicha cha redio ya Magic Fm.

"Tulikuwa tumesha maliza vipande vyake na muda kidogo aliomba kwenda msalani hata hata baada ya yeye kwenda alichukua muda mrefu huko,tulipoenda kumuangalia tulimkuta ni kama mtu aliezimia na muda huo alikuwa ameanguka kwenye mlango wa choo.Baada ya kumpeleka kituo cha afya na baada ya kufumbua macho hakuyutambua kabisa na hata jina lake pia hakulijua. Hali yake bado haijawa sawa japo tunasubiri majibu ya dokta kutujuza zaidi,Mi nawaomba watanzania wamuombee zaidi ili rudi kwenye hali yake ya kawaida.

8/09/2016

JB ATANGAZA KUSTAAFU KUIGIZA MOVIE

Msanii wa kuigiza nchini JACOB STEVEN atangaza kustafu rasmi,Kufuatia mtandao wa kijamii wa Instagram msanii huyo aliandika maneno yaliyoashiria kuwa ni kuachana na kuigiza na kugeukia uongozaji tu. 

Jb aliejivunia umaarufu kwenye baadhi ya filamu zake za kucheza kama mwanaume mwenye msimamo ameyasena hayo kupitia kwenye ukurasa wake .

Chanzo: www.saluti5.com


POGBA ATOA YA MOYONI BAADA YA KUTUA MANCHESTAR UNITED

MANCHESTER UNITED imekamilisha usajili wake kwa kiungo wa kati akitokea JUVENTUS,Poul Pogba ambae ndio mchezaji wa pekee alievunja rekodi ya usajili duniani kwa sasa.

Club ya Manchestar united ndio timu iliyo mfungulia kingo huyo njia zamkujulikana zaidi kimataifa ,Baada ya kupelekwa Juventus na kuimarika zaidi katika kikosi cha kutegemewa katika timu hiyo.

Pogba ambae amekuwa nafuraha kubwa baada ya kurejea klabuni hapo na hata alipoongea kwenye mahijiano yake ya kwanza alipofika kwenye timu hiyo hakusita kuficha hisia zake.

 "Ninafuraha kurejea hapa.Siku zote imekuwa ni klabu yenye sehemu maalumu kwenye moyo wangu na ninajipanga kuitumikia vema chini ya Jose Mourinho.alisema pogba

Chanzo (www.saluti5.com) saluti5

"Nina furaha kurejea hapa. Siku zote imekuwa ni klabu yenye sehemu maalum kwenye moyo wangu na ninajipanga kuitumikia vema chini ya Jose Mourinho.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/08/alichokisema-paul-pobga-baada-ya.html
Copyright © saluti5
"Nina furaha kurejea hapa. Siku zote imekuwa ni klabu yenye sehemu maalum kwenye moyo wangu na ninajipanga kuitumikia vema chini ya Jose Mourinho.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/08/alichokisema-paul-pobga-baada-ya.html
Copyright © saluti5
"Nina furaha kurejea hapa. Siku zote imekuwa ni klabu yenye sehemu maalum kwenye moyo wangu na ninajipanga kuitumikia vema chini ya Jose Mourinho.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/08/alichokisema-paul-pobga-baada-ya.html
Copyright © saluti5
"Nina furaha kurejea hapa. Siku zote imekuwa ni klabu yenye sehemu maalum kwenye moyo wangu na ninajipanga kuitumikia vema chini ya Jose Mourinho.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/08/alichokisema-paul-pobga-baada-ya.html
Copyright © saluti5


NEW(AUDIO) SHILOLE FT MAN FONGO- MTOTO MDOGO ( LISTEN & DOWNLOAD)

Karibu kuipakuwa nyimbo mpya iliyomkutanisha (Shilole na Man Fongo a.k.a Hainaga ushemeji),MTOTO MDOGO ndio jina rasmi la nyimbo hiyo,Kuwa wakwanza kuipakuwa nyimbo hii.
https://mkito.com/song/12829?referrer=1ceb58d401eec06ee83554dc0b9e59f240e68bfe

8/08/2016

RAYMOND AIZUNGUMZIA STYLE YAKE MPYA YA NYWELE

"Nimeona comments nyingi kuhusu rasta nilizoweka lakini naomba watu waelewe kwamba haikuwa style yangu na wala sina mpango wa kufuga rasta nitabaki na style yangu moja tu maana nimeona jinsi nilivyowakwaza mashabiki wangu."- Raymond

Nini maoni yako?

DIAMOND PLATNUMZ ANALIPA FADHILA KWA CHID BENZ

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond Platnumz amesema anafanya hivyo kwa Chid Benz kutokana na kitendo alichomuonyesha kabla hajawa maarufu, kukubali kufanya naye collabo ya wimbo wa ‘nalia na mengi’, bila kumzungusha na kumtoza hela kama ilivyo kwa wasanii wengine.

“Mimi nimefanya collabo na Chid, kipindi hicho nilimwambia, hakunitoza hata sh. kumi wala hakunizungusha hata kidogo, ndio maana linapokuja suala la Chidi nakuwa wa kwanza, wakati mimi namfuata Chidi, Chidi hasa nikajua atanikatalia kwanza mimi mbana pua, lakini hakunizungusha na wala hakuniomba hata mia”, alisema Diamond Platnumz.

Tujikumbushe hivi karibuni msanii Chid Benzi alipata matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, na Diamond alichukua jukumu la kumpeleka hospitali na kumbadilisha damu, kabla hajapelekwa rehab kupata tiba ya urahibu

WAZAZI WAMUUWA MTOTO KWA KIPIGO.. KISA KIKO HAPA

MWANAFUNZI aliyekuwa akisoma Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Zimba, Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Susana Kauzeni (15) ameuawa baada ya kupigwa na wazazi wake wakimtuhumu kuwa ni mtoro sugu wa shule.

Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (Shule za Msingi), Peter Fusi amesema kuwa mwanafunzi huyo alizikwa kijijini humo Julai 23, mwaka huu.

“Baba na mama yake walichangia kumpiga binti yao huyo wakimtuhumu kuwa ni mtoro sugu wa shule pia nyumbani amekuwa haonekani. Baba yake mzazi amekimbia baada ya kufanya uhalifu huo huku mama yake akiwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi,” alieleza Fusi.

Fusi alieleza kuwa kuanzia Agosti 3 na 4, mwaka huu alitembelea baadhi ya shule za msingi zilizopo kwenye Bonde la Ziwa Rukwa ikiwemo Shule ya Msingi Zimba kufuatilia kazi ya utengenezaji wa madawati mapya kwa ajili ya shule za msingi pia kufuatilia takwimu sahihi za wanafunzi ili kubaini wanafunzi hewa.

“Nilipofika kwenye Shule ya msingi Zimba, Mratibu Elimu Kata, Daudi Moga na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Fidelis Mwangurumba walithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ya mwanafunzi huyo,” alisema.

Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwangurumba, mwanafunzi huyo alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi watoro sugu shuleni hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

HIRIZI YA TIFFA YAIBUA MZOZO KWENYE SIKU YAKE YA KUZALIWA

Mtoto wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote Agosti 3, mwaka huu ametimiza mwaka mmoja lakini jipya lililoibuka ni kuhusiana na dawa ‘hirizi’ aliyovalishwa mkononi na bibi yake mzaa baba, Sanura Kassim ‘Sandra’, Risasi limenyetishiwa ubuyu.

Chanzo kutoka ndani ya familia ya mastaa hao kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, awali Tiffah alivishwa dawa hiyo lengo likiwa ni kumkinga na matatizo lakini Zari alipokwenda Sauzi akamvua kwa kuwa yeye si ‘muumini’ wa mambo hayo.

tiffaIkadaiwa kuwa, baada ya Zari kumvua walikaa muda mrefu bila Tiffah kuwa na ‘kadawa’ hako hali iliyomfanya mtoto huyo achelewe kutembea.

“Unajua ile dawa ina mambo mengi kwa watoto, inamsaidia kumkinga na matatizo lakini pia inamfanya atembee haraka, sasa walipoivua ikamfanya achelewe kutembea,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:

“Hali hiyo ilisababisha Zari na Diamond kutofautiana na mwisho wakakubaliana hirizi irejeshwe mkononi mwa Tiffah ndipo mtoto huyo alipoanza kutembea.”

Ikaelezwa kuwa, kuanza kutembea kwa Tiffah kumeibua furaha upya kwenye familia hiyo kwani walishaanza kuwa na hofu hasa ikichukuliwa kuwa, Zari ana mimba nyingine na anatarajiwa kujifungua Desemba, mwaka huu.

Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Diamond na alipopatikana alisema kuwa ni kweli mtoto wao ameanza kutembea lakini si kwa sababu ya dawa hiyo aliyofungwa mkononi.

“Hayo mambo ya kumvalisha na kumvua Tiffah ile dawa ya mkononi ni uamuzi tu lakini huwezi kusema ina uhusiano na kutembea kwake,” alisema Diamond.

TAKUKURU YAFAFANUA INSHU YA AVEVA SIMBA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imefunguka rasmi sababu za kumshikilia na kumweka ndani Rais wa Simba, Evans Aveva.
Aveva alishikiliwa tangu juzi Jumatano na kulala ndani kwenye Kituo cha Polisi cha Urafiki jijini Dar kabla ya kutolewa kwa dhamana Alhamisi huku chanzo cha yote kikiwa ni baada ya Takukuru kubaini alifanya uchepushaji wa fedha za mauzo ya fowadi, Emmanuel Okwi walizolipwa Simba na Etoile du Sahel dola laki tatu ambazo zilitolewa kwenye akaunti ya klabu na kuhamishiwa kwenye akaunti yake kabla ya kuanza kusambazwa huku nyingine zikihamishiwa katika akaunti moja ya nchini Hong Kong.

Msemaji wa Takukuru, Tunu Mlei ameliambia Championi Jumamosi kuwa kutokana na mazingira hayo, walihisi uwepo wa rushwa hivyo kuanza kuchunguza.

Tunu amefunguka huku akisisitiza kuwa iwapo atabainika na makosa katika sheria ya uchepushwaji, anaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani.

“Kwa sasa bado tunaendelea na uchunguzi na kwa mujibu wa sheria zetu haziniruhusu kusema nini kinaendelea kwenye uchunguzi,” alisema.

“Muda wa kuwachunguza itategemea. Kuna process (mchakato) zake. Kwa sasa tupo katika sheria No.11 kifungu cha 29 ya mwaka 2007 inayohusu uchepushwaji wa fedha, tukimaliza uchunguzi kazi yetu ni kupeleka faili kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka nchini, ndiye mwenye kuamua kesi iende mahakamani ama la.”

Akafunguka zaidi kuwa kwa sasa wanafanya kazi na Serikali ya Hong Kong.
“Kama unavyojua uchunguzi unahusishwa na nje ya nchi kwa kuwa kuna hela zimekwenda Hong Kong, hivyo tunashirikiana na serikali ya huko kujua zilikwenda kufanya kitu gani,” aliongeza.
Tunu amesema iwapo uchunguzi utabaini kuna mazingira ya rushwa, sheria itachukua mkondo wake lakini sheria ya uchepushaji wa hela pia ina adhabu yake.

“Kama nilivyosema tupo kwenye sheria ya uchepushaji, ambayo pia ina adhabu yake lakini siwezi kuisema maana vifungu vinaweza kuongezeka kulingana na uchunguzi utakavyofungua mambo mengine,” alisema Tunu.

Licha ya mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage kusisitiza Etoile du Sahel kuilipa Simba fedha hizo muda mrefu, viongozi chini ya Aveva wamekuwa wakiruka kimanga wakisema bado hela hiyo haijaingia kwenye akaunti zao.

Simba ilimuuza Okwi mwaka 2013 wakati wa utawala wa Mwenyekiti Ismail Aden Rage, hata hivyo hakukaa sana kabla ya kwenda SC Villa ya Uganda, kisha Yanga kabla ya kurejea Simba ambako alikaa msimu mmoja kabla ya kuuzwa kwa dola 110,000 kwenda SonderjyskE ya nchini Denmark, mwaka juzi.

MASOMO YA SAYANSI SASA YATAKUWA MASOMO YA LAZIMA MASHULENI

SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Tanga  na Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na mamia ya walimu wa elimu ya msingi kwenye mafunzo ya muda mfupi kuhusu mtaala mpya wa kufundishia wanafunzi wa darasa la tatu na nne.

Alisema hivi sasa nchi imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa kati ambao ni wa viwanda, hivyo suala la sayansi haliwezi kuepukwa kwa sababu ni wakati sasa wa kuwa na wataalamu wengi wa fani za sayansi watakaoweza kutosheleza mahitaji ya sekta ya viwanda nchini.

Alisema kutokana na uhaba wa wataalamu wa sayansi nchini kwenye maeneo mengi, wizara imeamua kuanzia sasa wanafunzi wote wa elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, watalazimika kusoma masomo ya sayansi na kufanya mtihani wa masomo hayo, na kwamba baada ya matokeo kutoka ndipo watafanya uamuzi ama wa kuendelea nayo au la.

Hatua hii kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, itamlazimisha mwanafunzi kusoma kwa bidii ili kuhakikisha anafaulu masomo hayo ingawa hivi sasa wanafunzi walio wengi wanadai masomo hayo ni magumu, ndiyo maana wanachagua kusoma masomo ya sanaa.

Alisema ili kuhakikisha azma ya serikali ya wanafunzi wanapata vitendea kazi vya masomo hayo, Sh bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwenye shule zote za sekondari nchini ili kuwepo na zana za kufundishia kwa ajili ya masomo ya sayansi.

"Mafunzo ya vitendo sasa sio mbadala ni lazima, na yatafanywa kama sehemu ya masomo na wanafunzi wote watalazimika kuyafanya kwa vitendo ili wawe na uelewa wa walichosoma kwa manufaa ya taifa,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuona kiwango cha elimu kinachotolewa nchini kina hadhi sawa na elimu itolewayo na mataifa mengine ili kupata wataalamu wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya soko hata kama sio wote wataajiriwa ila hata wale wasiopata ajira wajiajiri kupitia elimu waliyopata.

Aliwataka walimu waliohudhuria mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia uwezo wao na elimu waliyopata kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya taaluma ya ualimu ili kuwajengea msingi mzuri wa elimu wanafunzi wa shule za msingi.

Akizungumzia kauli ya Profesa Ndalichako, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAMANGOSCO), Mahmoud Mringo alisema ni uamuzi mzuri ila umekuja kwa kuchelewa kwa sababu mahitaji ya wataalamu wa sayansi nchini ni makubwa kuliko idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo.

Alisema pamoja na uamuzi huo mzuri uliochukuliwa na serikali, lakini bado kutakuwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo, maabara na maktaba na kwamba hali hiyo inaweza kusababisha mahitaji ya walimu hao kutoka nje yakaongezeka.

Katibu wa Tamangosco, Benjamin Mkonya alisema ni hatua nzuri ingawa utekelezaji wake utakuwa na changamoto nyingi kwa sababu hali halisi ya mazingira ilivyo nchini.

Alisema ikiwa serikali inadhamiria kutekeleza azma hiyo ni vyema kipengele cha vigezo vya shule kuwepo ambavyo vimeainishwa ndani ya sheria ya elimu nchini, vikaangaliwa ambavyo ni uwepo wa maabara ya kutosha, maktaba yenye vifaa na walimu wa kutosha.

Alisema iwapo vigezo hivyo vikiangaliwa shule ambazo hazijakidhi vigezo hivyo zikafutwa na vifaa vilivyopo kwenye maabara na maktaba hizo zikaongezwa kwenye shule zenye vifaa hivyo ili kusaidia utekelezaji wa azma hiyo ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Walimu washiriki wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo ambayo walisema ni mazuri na yameongeza kiwango chao cha uelewa na kuwaongezea mbinu za ufundishaji sambamba na kukuza morali ya kazi zao.

Pamoja na kushukuru, wameomba wizara hiyo iangalie jinsi ya kuweka posho kwa baadhi ya maeneo ya kazi, hususan kwenye vituo vya kazi vilivyopo pembezoni na kwenye mazingira magumu ili kuwajengea walimu motisha wa kufundisha maeneo hayo.

Walimu waliohudhuria mafunzo hayo ni 480 wanaotoka halmashauri za Bumbuli, Mji wa Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

MH.JANUARY MAKAMBA, KUNA ADUI MWINGINE AMEONGEZEKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba amesema tangu nchi ipate uhuru miaka 50 iliyopita, maadui watatu ambao ni maradhi, umaskini na ujinga wapo pale pale lakini kuna adui wa nne aliyeongezeka.
makamba

Ameyasema hayo Ijumaa hii jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua ripoti ya hali ya kipato cha uchumi Afrika Mashariki iliyotolewa na Taasisi ya Society for International and Development (SID).

Alimtaja adui huyo kuwa ni tofauti kubwa ya usawa kati ya walichonacho na wasichonacho.

“Katika safari ya nchi yetu tumepata wazungu wapya ambao ni Waafrika wenzetu. Watu wanaishi maisha mazuri sana, watoto wao wanapata elimu nzuri sana, sasa hivi tofauti imekuwa ni kubwa sana,” alitoa mfano huo Makamba.

“Kama nchi inataka kujenga taifa la watu walio sawa hakuna budi kukabiliana na suala hilo, kwani usawa katika fursa ndiyo nyenzo muhimu ya kukabiliana na usawa katika jamii,” aliongeza.

8/07/2016

MANCHESTER UNITED YATWAA KOMBE LA FA CUP

Kuelekea kuanza kwa michuano ya ligi kuu ya England, jioni ya leo wamemenyana na mahasimu wawili kati ya MANCHESTER UNITED na LEICESTER CITY, mechi iliyokuwa na burusani ya aina yake na kudhihirishia mashabiki kuwa kocha Jose' Mourinho ataendeleza ubabe wake wa kuchukua vikombe.

MANCHESTER UNITED ilianza kutikisa vyavu kupitia kinda wake mahiri Jesse Lingard goli lililodumu mpaka mapimziko ya mchezo 45(half time) na kufuatia dakika chache kufuatia makosa ya umakini kwa Mouri Fellain mchezaji mahiri na mwenye uwezo mzuri wa kucheza na nyavu Jamie Vardy alinyanyua makwapa ya mashabiki hao wa Leicester city,Jambo lilolopelekea Mourinho kubadili mgumo na kuchezasha viungo wengi zaidi jambo lilio zaa matunda kwa mashetani wekundu kwa kupata goli zuri kutoka kwa foward wao mpya Zlatan Ibrahimovic ,aliefunga kwa kukandamiza kwa kichwa mpira wavuni.

Jumamosi ya tarehe 14/8 ligi ya EPL inaanza rasmi ambako hapo pia utaendela kuona uhondo wa timu zote za ligi hito usajili mpya na mambo mengine mengi wakati huo mchezaji na kiungo wa Ufaransa atakuwa anakamilisha usajili wake kuelekea MANCHESTER UNITED.




8/05/2016

SHAMSA FORD,NIPO TAYARI KUOLEWA KUANZIA SASA

BAADA ya kutolewa barua ya uchumba na mpenzi wake mpya, Chidi Mapenzi, mwigizaji, Shamsa Ford, amefunguka kwamba wakati wowote atafunga ndoa na mwanaume huyo kwa kuwa mipango yao imeshakamilika.

Shamsa aliliambia MTANZANIA kwamba licha ya kupitia katika changamoto za wapenzi wengi, mpenzi wake huyo wa sasa ndiye aliyeonyesha ushawishi hadi kutaka kumuoa.

“Kwa hatua hii najivunia, hadi mwanaume akushawishi muoane huyo ana nia njema na heshima kwangu,” alisema Shamsa.

Pia Shamsa aliwaeleza wapenzi wa filamu zake kwamba wataendelea kupata burudani zake hata kipindi atakachokuwa ameolewa.

8/04/2016

DIAMOND PLATNUMZ AMFUNGA GOLI LA PILI ZARI WASUBIRI KUTWAA KOMBE DISEMBA

Mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.

Muimbaji huyo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume.
“Yah kweli mimi ni baba kijacho,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena “Natarajia Mama Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa kiume,”

Aliongeza, “Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza tena mtoto mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto wetu wawili”
Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni atatimiza mwaka mmoja.

RAYMOND, KUFANYA KAZI NA CHIDI BENZI KWANGU NI KAMA BARAKA

Msanii Raymond ameelezea furaha yake baada ya kufanya kazi na msanii wa hip hop Chid Benz, na kusema kuwa kwake ni bahati kubwa sana.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Raymond amesema yeye kufanya kazi na Chid Benz ni heshima kubwa, kwani msanii huyo ana uwezo mkubwa na yeye bado ni mchanga kwenye game.

"Nilifurahi kupata nafasi ya mimi kufanya ngoma na Chid Benz, kwa sababu ni brother ambaye alikuwa anafanya vizuri kitambo, ni msanii mzuri kwa hiyo mimi kufanya naye ngoma naona ni nafasi ambayo nimeipata inanionyesha kabisa kwamba muziki wangu unaenda kwenye nuru, kwa sababu mpaka kaka zako ambao walikutangulia wanakubali kufanya kazi na wewe, ina maana wanakubali kazi zako", alisema Raymond.

Raymond aliendelea kusema kuwa kazi hiyo ambayo ameifanya na Chid Benz ni wimbo aliotokea kuupenda sana, na kuahidi video mashabiki wake hivi karibuni.

"Ngoma ya chuma ni ngoma ambayo naipenda sana achilia mbali mtu ambaye nimefanya naye, namshukuru sana mungu na napata coments nyingi na soon video inakuja", alisema Raymond

HUYU NDIO MWANAUME ATAKAE MUOA SHAMSA FORD

Mfanyabiashara wa nguo ‘Chidi Mapenzi’ yupo mbioni kufunga ndoa na mwigizaji Shamsa Ford baada ya hivi karibuni kumtolea barua mrembo huyo.

uigizaji huyo alikaririwa na gazeti la Mtanzania akisema kwamba licha ya kupita katika changamoto za wapenzi wengi, mpenzi wake huyo wa sasa ndiye aliyeonyesha ushawishi wa hadi kutaka kumuoa.

“Kwa hatua hii najivunia, hadi mwanaume akushawishi muoane huyo ana nia njema na heshima kwangu,” alisema Shamsa.