Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA anatarajiwa kufungua Kongamano la siku mbili
litakalo jadili na kutoa maoni juu ya mpango wa serikali wa kuongeza
ushiriki wa watanzania kwenye uwekezaji na uchumi
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Hamis Mwinyimvua amesema kongamano
hilo litafanyika kuanzia Alhamisi wiki hii jijini DSM ambapo washiriki
watajadili na kutoa maoni juu ya mpango wa watanzania kushiriki kwenye
uwekezaji na uchumi.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
–NEEC-, Beng’i Issa amesema kongamano litakuwa na washiriki 350 kutoka
sekta ya umma na binafsi.

No comments:
Post a Comment