Msanii Ruby ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Yamoto Band
unaofahamika kwa jina la 'Suu' amefunguka na kupinga kauli iliyotolewa
na maneja wa Yamoto Band, Mkubwa Fella kuwa yeye ana stress ndiyo maana
maana alishindwa kutokea kwenye video.
Akiongea na Planet bongo ya East Africa Radio Rubby amesema Yamoto Band
hawakuona umuhimu wake kwenye video hiyo ndiyo maana waliweza kushoot
video hiyo siku ambayo yeye alikuwa busy na mambo yake mengine, na
kusema kutokana na wao kutaka video hiyo ifanyike ndani ya siku hiyo na
kupinga wazo la kumsubiri kidogo inatosha kuonyesha kuwa hawakuona
umuhimu wa yeye kuwepo kwenye video hiyo, kwani angekuwa na umuhimu
wangeweza kumsubiri.
"Unajua siku ambayo wao walikuwa wakishoot video hiyo mimi nilikuwa na
mambo yangu mengine hivyo nilikuwa busy, niliwaomba kama wanaweza
wanisubiri kidogo nimalizane na hizo kazi zangu lakini wao wakafanya
video hiyo. Hilo linatosha kuonyesha sikuwa na umuhimu kwani ningekuwa
na umuhimu wangeweza kunisubiri, mimi sikukataa na nilikuwa na uhakika
asilimia mia nitakuwepo kwenye video ile sema kwa kuwa walikuwa na
haraka ndiyo maana imetokea hivyo." alisema Rubby
"Kiukweli mimi nimeumia sana maana Audio ile tumefanya muda mrefu na
waliweza kusubiri mpaka tukakamilisha iwaje kwenye video washindwe
kunisubiri, maana hii kazi tunasaidiana mimi niliwaambia niko busy
nisubirini wangeweza kunisubiri tu kisha tukafanya video pamoja"
aliongeza Rubby

No comments:
Post a Comment