Staa ‘the big name’ wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amegeuka
gumzo ukumbini kufuatia kupita mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa amebusti nido (matiti) kiasi cha
kuwafanya baadhi ya waalikwa ‘kumdiskasi’.
Tukio hilo la aina yake lilijiri usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita
ndani ya ukumbi wa sinema uliyopo Jengo la Quality Centre Barabara ya
Pugu jijini Dar ambapo staa huyo alikuwa akizindua filamu yake ya Sikitu
huku mgeni rasmi akiwa Waziri Nape.
Katika shughuli hiyo ambayo Wikienda lilikuwa ndani ya nyumba, baadhi ya
wapenyeza ubuyu walisikika wakinong’onezana juu ya matiti ya Kajala
namna yalivyokuwa yametuna kwenye gauni tofauti na alivyozoeleka kiasi
cha wengine kudai ameyabusti kwa kuyachoma sindano.
“Mh! Jamani mbona leo Kajala amebusti nido kiasi hiki? Si bure, kama
hajachoma sindano ya kubusti itakuwa si bure. Yaani unaambiwa watu
wanamkodolea mimacho hadi wanaduwaa,” alisikika mmoja wa mashabiki
aliowaalika kwenye sinema hiyo ambayo itakuwa gumzo mtaani.
Shuhuda mwingine alisikika akisema kuwa, Kajala aliwafanya hata wasanii
wenzake kumgeukia wakati anaingia ukumbini hasa wengi wao walikuwa
wamemkodolea jicho kifuani kwake kwa lengo la kutaka kuona namna
alivyokuwa amebusti nido.
Alipofuatwa Kajala kuulizwa kulikoni au nini kimetokea hadi akavimbisha
matiti kiasi hicho, hakuwa na la kusema zaidi ya kushukuru kwa kufana
kwa uzinduzi wa filamu yake hiyo.
“Hivi huna ‘engo’ nyingine? Huoni watu wanavyoifurahia filamu yangu?
Hayo ndiyo mambo ya kuniuliza,” alisema Kajala akisisitiza kuwa hataki
maswali zaidi.

No comments:
Post a Comment