Waangalizi wanasema maafisa wa serikali walianza kupambana na kile kinachoonekana kuongezeka kwa visa vya kuharibu picha ya rais katika vitabu vya wanafunzi shuleni.
Makundi ya vijana yamehojiwa kutokana na matukio hayo na idadi kubwa inakabiliwa na mashtaka.
Mwezi uliopita, zaidi ya wanafunzi mia tatu walitimuliwa shuleni katika mji wa Ruziba baada ya walimu kukuta vitabu vyenye picha ya rais vimeharibiwa kuandikwa ujumbe wa matusi.
Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikiwa masuala ya watoto UNICEF limelaani kukamatwa na kufukuzwa kwa watotot hao, na kusema shule zinatakiwa kuheshimiwa kama maeneo
salama kwa watoto.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi nchini Burundi tangu rais Nkurunziza kuamua kuwania muhula wa tatu kinyume cha katiba ya nchi hiyo hapo mnamo mwaka jana

No comments:
Post a Comment