SIMU ziliingizwa nchini zikiwa hazina kiwango kuzimwa rasmi kesho,
katika kuhakikisha kila mtu anatumia simu kiwango kwa usalama na ulinzi
wa nchi.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba
amesema kuwa katika uzimaji wa simu wameshatoa elimu juu ya simu hizo.
Kilaba amesema kuwa simu ambazo watu walibadilisha (Flash) nazo
zitazimwa kutokana na kufanya hivyo ni kosa la kisheria na mtu
anayefanya hivyo kifungo chake ni miaka 10.
Amesema hakuna kitu chochote kinachofanya simu zisiweze kuzimwa hivyo
watu wajiandae kwa zoezi hilo na simu zitakazozimwa wametakiwa
kuzihifadhi katika mazingira salama.
Aidha amesema wametoa elimu ya kutosha, hivyo kesho kutakuwa na mkutano
wa wadau mbalimbali wa makampuni ya simu, na wamiliki wa maduka ya simu
pamoja na mafundi katika kubadilishana mawazo wakati wa kuzima simu
feki.
‘’Simu feki kesho zitazimwa, hatutakuwa na mabadiliko ya kuongeza muda
au vinginevyo kutokana na elimu iliyotolewa juu ya simu ya feki ambazo
baada ya soko kushindikana mjini walipeleka vijijini’’amesema Kilaba .

No comments:
Post a Comment