Abdul Kiba amesema yupo tayari kujiunga na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kama hela itawekwa mezani.
Bifu la Alikiba na Diamond linaonekana kuathiri mpaka mfumo wa watu wa
pembeni wanaowazunguka wasanii hao japo kila mmoja anakubali kuwa hana
tatizo na mwenzake huku ukweli wa kila mmoja ukibaki moyoni mwake.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio,
Abdu Kiba alisema kuwa kama watakuwa na pesa za kutosha na makubaliano
mazuri anaweza kufanya kazi chini la Label hiyo [WCB].

No comments:
Post a Comment