Nyumba
moja iliyopo mtaa wa Kiseke wilayani Ilemela mkoani Mwanza imeteketea
kwa moto leo asubuhi na kuunguza vitu vingi huku wakazi wa nyumba hiyo
wakinusurika.
Taarifa
zinaarifu kuwa, nyumba hiyo imewaka moto baada ya mmoja wa watoto wa
familia hiyo kuamka asubuhi na kumwaga mafuta ya taa katika moja ya
chumba cha nyumba hiyo na kisha kuwasha moto.
Imeelezwa
kuwa, kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili amekuwa
akiwatishia kwa muda mrefu kuwachoma moto lakini wamekuwa wakimpuuza
kutokana na matatizo yake ya akili.
Baada
ya kumwaga mafuta na kuwasha moto, kijana huyo alitoweka na
kuwafungia ndugu wengine ndani ambapo majirani walifanikiwa kuwahi
kuwaokoa.

No comments:
Post a Comment